Nchi haiongozwi kutoka kichwani, inaongozwa kwa mjibu Wa sheria na katiba.
Kwa hiyo swala la kulipa kodi siyo la hiari na wala halijaletwa na Magufuli lipo kisheria. Sasa Membe atuambie angekuwa rais yeye angeongoza kutoka kichwani mwake au kwa kufuata sheria za nchi??
Kumbuka kuna nchi ukikwepa kodi na ikagundulika Unanyongwa!!!
Hakuna nchi iliyoendelea kwa kuleana leana hivi.
Na ndio maana Watz wengi tulikuwa hatutaki rais Wa kuchukua fomu huku ameandama na Kundi la watu ,madhara yake ndio haya, hapa Membe ni lzm anatetea rafiki zake wameguswa..
Lkn Magufuli alishasema tokea mwanzo kuwa kutumbua jipu kuna maumivu, bahati mbaya halina dawa nyingine.
Membe acha tu augulie maumivu ya jipu ndio kupona kwake
Asante Mungu kwa kutuebushia mbali watu Wa aina hii kuwa viongozi wetu