Imaginary fan base, Aslay ameshapotea na atabaki jina tu hata Beka Fleva kwa sasa ana impact zaidi ya Aslay. Kuitengeza brand na kuifanya iwe strong kumemshinda kabisa, lawama ziende kwa management yake. Marioo anaonekana kuwa na management strong lakini kuvuma na ku'maintain ni vitu viwili tofauti kabisa, let's give him time tuone ila kwa sasa anafanya vizuri.
Watu ninaoamini(kwa mtazamo wangu) wata'maintain kwa muda mrefu ni Harmonize na Rayvanny na kitakachowasaidia ni hatred baina yao kwani imegeuka driving force hasa wanavyochonganishwa na fans ukizingatia kuachana kwa Harmo na Kajala na couple ya Vanny na Paula ni vichocheo ukizingatia fracas yao wote hapo nyuma.
Hata rivalry ya Sadala na Kiba craftsman man Ruge aliitengeneza makusudi kuchangamsha game, hata back in the days Bongo movie ilichangamshwa na rivalry ya Kanumba na Ray baada ya Kanumba kufariki na rivalry kupotea game ikapooza.