warumi
R I P
- May 6, 2013
- 16,218
- 18,440
Leo nilikuwa nacheki movie mpya ya JB inaitwa DANIJA, movie imechezwa na JB mwenyew,Adam kuambiana,Gabo na muhusika mkuu wa hiyo movie anitwa DIANA KIMARO, dah huyu demu ki ukweli yupo vizuri sana, ukiachilia mbali mvuto wa shepu yake na sura nzuri, vile vile ni mkali sana kwenye uigizaji na anajua kujibeba, ana vitu vingi sana huyu dogo, hawa wakongwe wakibweteka tu dogo anawapiga bao, achilia mbali uzuri wake ila uwezo wake kwenye kuigiza ni mkubwa sana kuliko umri alionao, wengi uwa wanamfananisha na lulu kwa kuwa Mara nyingi wamekuwa wakiigiza wote, hata kwenye movie ya lulu ya FOOLISH AGE waliigiza wote, lulu pamoja na ukongwe wake kwenye game ila anasubiri kwa Diana, tukizungumzia kipaji haswa, Diana kabarikiwa kwa asilimia zote, kama akiwa serious kwenye game atafika mbali sana, ana vitu vizuri sana kwenye ubongo wake... jaribu kununua hii filamu ya DANIJA ujionee mwenyewe uwezo alionao nisizungumze sana.