Diaspora Hawatoi connection?

Diaspora Hawatoi connection?

Mkuu.tumetofautiana usitaka maisha au msoto uliopitia et watu wengine wapitie .huenda nikakosa visa lkn moyo nitamani na Mimi kufikia ulipofikia ww.kumbuka hata family zetu uchumi umetofautiana.kingine nikwambie mheshim kijana yeyote ambaye anandoto za kufanya maendeleo Fulani hvyo anapokuja kukuomba ushauli usimuone boya kumbuka kuna vijana kama yeye ambao wamekosa mawazo hayo ,wengine now wanaiba,vibaka,wahuni,nk

Mkuu unaandika mambo mengi nje ya mada.

Mosi, umesema uliniomba mimi connection nikakutolea nje, una uthibitisho wa hilo?

Pili, a connection is all about helping each other sio nawewe upitie msoto wangu ndo maana nataka kukusaidia.

Ulitaka kwenda nchi gani na kwa njia gani tuanzie hapo. Umesema visa na nauli kwako sio ishu.

Jikite kwenye mada.
 
Naandika huu uzi baada ya kusoma na kusikia mara kadhaa kwamba diaspora wabongo hawatoi connection za kwenda nje compared to diaspora wa nchi kama Kenya, Nigeria nk. Mimi kama diaspora napinga hii notion vikali.

Hapa JF Kuna nyuzi zaidi ya 100 zinazojadili jinsi ya kwenda nje, a quick search mtu unapata majibu yote na bado watu tunachangia nyuzi kila leo. Mnataka connection gani zaidi?

EBM anatoa free knowledge on YouTube na bloggers wengine jinsi ya kwenda nje, hiyo sio connection? Tuwape bundle za kuingia youtube au?

Mimi binafsi nimeshirikiana na watu kadhaa toka kwenye forum hii hii toka walipoanza harakati zao za kwenda nje na sasa wapo mbele needless to say walifanya sehemu zao na mambo yao yakafanikiwa. Sasa urafiki umekua undugu. Tatizo ndugu zangu wamatumbi mnapotaka connection mnataka hao diaspora wawape hadi hela na passport wawatafutie. You have to play your part as well.

Kimsingi kwenda nje is as easy as ABC. Kupata connection ni vizuri but isn't everything. Mimi nilienda bila connection yeyote ile, maelezo yote yapo kwenye websites za nchi husika ila ni lazima uwe tayari kufanya sehemu yako pia, kuna watu wanadhani diaspora wana a magic code ya kwenda nje this couldn't be further from the truth. Ni lazima uwe tayari kufanya sehemu yako.

Wabongo wenzangu punguzeni kulalamika kiboya, JF Kuna more than 100 threads, YouTube ipo, website za nchi husika zipo, tunajitoa as much as we can but we can only do so much. Maisha yako ni jukumu lako, kusaidiana kupo ila sio wajibu.

Nipo around mazee.
wewe ni diaspora wa nchi gani mkuu ili nikija unipokee
 
Asante, hivyo vyuo vinavyotoa hizi post graduate mpaka ufike ndio navihitaji binafsi nimefuatilia poland gharama zao ziko reasonable bank statement ndio kipengele.
Vipi mawakala wa kazi huko na gharama zao!?

Mkuu nipo NA so ushauri wangu is somewhat biased. Siku zote nawaambia watu wajaribu kwanza USA au Canada wakishindwa ndo waanze nchi zingine.

Kwa US, angalia state universities vipo vyuo ambavyo ada ni hadi ufike for postgrads.

Sina uzoefu wa kuja kwa njia ya kazi. Wadau wengine watakuja kuchangia hili au mcheck EBM youtube kuna video kaongelea hilo in details.
 
Shukrani nitajaribu kuchek gharama zao USA na Canada
 
Mpaka kumuhifadhi??? huo sasa ndio uboya wenyewe na hio ni spoon feeding. Jiulize sie wengine tuliingia hapa bila mjomba wala shangazi wa kutuhifadhi na bado tulitoboa. Wabongo wavivu wa kufikiri na kimatendo pia.
Mbongo Mbongo tu, halafu unaonekana una roho mbaya kama mdudu!.
Kwahiyo kwasababu wewe uliingia bila mjomba au msaada wa kuhifadhiwa basi unataka na mwenzako apitie njia uliyopitia wewe?
Yaani kama wewe ulipata tabu ndo ukatoboa unataka mwenzio asisaidiwe ateseke kwanza kama wewe sio?
Nyie ndio hata familia zenu mnashindwa kuzipa huduma bora kisa mlipitia mateso wakati mnatafuta Mali, kwahiyo unataka na familia iteseke kama wewe kipindi kile.... Acha roho ya malipizi Kila binadamu ana njia zake za kutoboa.
 
Shukrani nitajaribu kuchek gharama zao USA na Canada

Kama plan yako ni kuzamia, gharama za chuo kwako ni irrelevant.

Wewe uwe na hela ya application, visa na nauli. Ukifika unachimba.

Regarding BS kuna namna watu wanacheza nazo hapo bongo, do your homework. Bongo hata mhuri wa magogoni unapata tafuta connection hapo hapo bongo.
 
Kama plan yako ni kuzamia, gharama za chuo kwako ni irrelevant.

Wewe uwe na hela ya application, visa na nauli. Ukifika unachimba.

Regarding BS kuna namna watu wanacheza nazo hapo bongo, do your homework. Bongo hata muhuru wa magogoni unapata tafuta connection hapo hapo bongo.
Mkuu unampeleka mbali school izo nchi ni ghali aombe visit visa canada ajue french ata cha kuomba maji the rest is history
 
Mkuu unampeleka mbali school izo nchi ni ghali aombe visit visa canada ajue french ata cha kuomba maji the rest is history

Vizuri ndo maana tunashare ideas hapa. Sina uzoefu na visiting visa za CN ila kwa shule hahitaji kulipa ada since kasema yeye mpango wake ni kufika tu na kuingia mtaani.
 
Asante, hivyo vyuo vinavyotoa hizi post graduate mpaka ufike ndio navihitaji binafsi nimefuatilia poland gharama zao ziko reasonable bank statement ndio kipengele.
Vipi mawakala wa kazi huko na gharama zao!?
Bro mbele ni mbele tu ... Ila poland sio nchi ya kuishi otherwise uende kwa kuanzia kama njia tu
 
Kabisa mkuu yani tunakatishana tamaa .mfno kuna jamaa mdogo wake mfugale yy yupo USA na tyl ana uraia huko.nilipomcheki akasema life kule ngumu sana
Alfu anaanza kunitambia vitu ambavyo yy anamiliki kule kwa mda mfupi lkn nikimwambia nipe connection shida

Chief unaandika mambo mengi ila hujibu maswali ya msingi.

Ulitaka kwenda nje kwa njia gani shule, matibabu, utalii, biashara au?

Ulitaka kwenda nchi gani?

Information gani unahitaji?

Okoa nguvu na muda.
 
Vizuri ndo maana tushare ideas hapa. Sina uzoefu na visiting visa za CN ila kwa shule hahitaji kulipa ada since kasema yeye mpango wake ni kufika tu na kuingia mtaani.
Mkuu mimi nmeenda ulaya kwa kusoma ndio hulipi ada lakini huwez pata hyo temporary permit bila kulipa ada na ili ubadili status moja kwenda nyingine lazima ulipe ada upate permit ndo mengine yaendelee ukitaka kusoma aya usipptaka sawa acha shule umebadili status tayar acha shule ujabadili status permit inakuwa revoked
 
Chief unaandika mambo mengi ila hujibu maswali ya msingi.

Ulitaka kwenda nje kwa njia gani shule, matibabu, utalii, biashara au?

Ulitaka kwenda nchi gani?

Information gani unahitaji?

Okoa nguvu na muda.
Kifupi nahitaji connection haijalishi ni njia gani nitatumia .kingine mm mtoto wa kimasikini baba ,mama ndo Mimi kusema kutembea nitakudanganya ingwa kama kusoma ikitokea poa .lkn tusipende kuwaktisha wengine tamaa
 
Tena wewe nakutamani sana.mkuu omba nisije kufanikiwa yani popote ulipo nitajitahidi nikupate alfu nikusaidie ili nikuoneshe kuwa katika maisha tunategemeana .tena hata ukifa kabla yangu hakika nitatfuta kabuki lako liko wapi angalau hata nilijengee au kuweka maua.lengo kukuonesha kuwa hata wewe ulipo hapo umesaidiwa hvyo usiwakatishe vijana ambao wana mawazo chanya ktk jamii

Nahitaji kujua ni lini tuliwasiliana kabla ya leo, una uthibitisho wowote ule? Ulete hapa tafadhali.

Ni wapi nilikukatisha tamaa. Leta risiti mkuu.
 
Tena wewe nakutamani sana.mkuu omba nisije kufanikiwa yani popote ulipo nitajitahidi nikupate alfu nikusaidie ili nikuoneshe kuwa katika maisha tunategemeana .tena hata ukifa kabla yangu hakika nitatfuta kabuki lako liko wapi angalau hata nilijengee au kuweka maua.lengo kukuonesha kuwa hata wewe ulipo hapo umesaidiwa hvyo usiwakatishe vijana ambao wana mawazo chanya ktk jamii

We nae acha gubu Mbona anasaidia watu sana na laana zako hazimpati
Ulitaka akupe pesa wapo wengi kawasaidia tu na sio lazima yeye kuna wengine pia wanaweza saidia
 
Mpaka kumuhifadhi??? huo sasa ndio uboya wenyewe na hio ni spoon feeding. Jiulize sie wengine tuliingia hapa bila mjomba wala shangazi wa kutuhifadhi na bado tulitoboa. Wabongo wavivu wa kufikiri na kimatendo pia.
Ukishakua mbele unajiona sio mbongo tena,na unaanza kutusema.

Sikatai madai yako lakini pia diaspora wengi tukiwauliza jambo mnaishia kutuambia tucheki websites za nchi husika
 
Back
Top Bottom