Diaspora Hawatoi connection?

Mkuu unaandika mambo mengi nje ya mada.

Mosi, umesema uliniomba mimi connection nikakutolea nje, una uthibitisho wa hilo?

Pili, a connection is all about helping each other sio nawewe upitie msoto wangu ndo maana nataka kukusaidia.

Ulitaka kwenda nchi gani na kwa njia gani tuanzie hapo. Umesema visa na nauli kwako sio ishu.

Jikite kwenye mada.
 
wewe ni diaspora wa nchi gani mkuu ili nikija unipokee
 
Asante, hivyo vyuo vinavyotoa hizi post graduate mpaka ufike ndio navihitaji binafsi nimefuatilia poland gharama zao ziko reasonable bank statement ndio kipengele.
Vipi mawakala wa kazi huko na gharama zao!?

Mkuu nipo NA so ushauri wangu is somewhat biased. Siku zote nawaambia watu wajaribu kwanza USA au Canada wakishindwa ndo waanze nchi zingine.

Kwa US, angalia state universities vipo vyuo ambavyo ada ni hadi ufike for postgrads.

Sina uzoefu wa kuja kwa njia ya kazi. Wadau wengine watakuja kuchangia hili au mcheck EBM youtube kuna video kaongelea hilo in details.
 
Shukrani nitajaribu kuchek gharama zao USA na Canada
 
Mpaka kumuhifadhi??? huo sasa ndio uboya wenyewe na hio ni spoon feeding. Jiulize sie wengine tuliingia hapa bila mjomba wala shangazi wa kutuhifadhi na bado tulitoboa. Wabongo wavivu wa kufikiri na kimatendo pia.
Mbongo Mbongo tu, halafu unaonekana una roho mbaya kama mdudu!.
Kwahiyo kwasababu wewe uliingia bila mjomba au msaada wa kuhifadhiwa basi unataka na mwenzako apitie njia uliyopitia wewe?
Yaani kama wewe ulipata tabu ndo ukatoboa unataka mwenzio asisaidiwe ateseke kwanza kama wewe sio?
Nyie ndio hata familia zenu mnashindwa kuzipa huduma bora kisa mlipitia mateso wakati mnatafuta Mali, kwahiyo unataka na familia iteseke kama wewe kipindi kile.... Acha roho ya malipizi Kila binadamu ana njia zake za kutoboa.
 
Shukrani nitajaribu kuchek gharama zao USA na Canada

Kama plan yako ni kuzamia, gharama za chuo kwako ni irrelevant.

Wewe uwe na hela ya application, visa na nauli. Ukifika unachimba.

Regarding BS kuna namna watu wanacheza nazo hapo bongo, do your homework. Bongo hata mhuri wa magogoni unapata tafuta connection hapo hapo bongo.
 
Mkuu unampeleka mbali school izo nchi ni ghali aombe visit visa canada ajue french ata cha kuomba maji the rest is history
 
Mkuu unampeleka mbali school izo nchi ni ghali aombe visit visa canada ajue french ata cha kuomba maji the rest is history

Vizuri ndo maana tunashare ideas hapa. Sina uzoefu na visiting visa za CN ila kwa shule hahitaji kulipa ada since kasema yeye mpango wake ni kufika tu na kuingia mtaani.
 
Asante, hivyo vyuo vinavyotoa hizi post graduate mpaka ufike ndio navihitaji binafsi nimefuatilia poland gharama zao ziko reasonable bank statement ndio kipengele.
Vipi mawakala wa kazi huko na gharama zao!?
Bro mbele ni mbele tu ... Ila poland sio nchi ya kuishi otherwise uende kwa kuanzia kama njia tu
 
Chief unaandika mambo mengi ila hujibu maswali ya msingi.

Ulitaka kwenda nje kwa njia gani shule, matibabu, utalii, biashara au?

Ulitaka kwenda nchi gani?

Information gani unahitaji?

Okoa nguvu na muda.
 
Vizuri ndo maana tushare ideas hapa. Sina uzoefu na visiting visa za CN ila kwa shule hahitaji kulipa ada since kasema yeye mpango wake ni kufika tu na kuingia mtaani.
Mkuu mimi nmeenda ulaya kwa kusoma ndio hulipi ada lakini huwez pata hyo temporary permit bila kulipa ada na ili ubadili status moja kwenda nyingine lazima ulipe ada upate permit ndo mengine yaendelee ukitaka kusoma aya usipptaka sawa acha shule umebadili status tayar acha shule ujabadili status permit inakuwa revoked
 
Chief unaandika mambo mengi ila hujibu maswali ya msingi.

Ulitaka kwenda nje kwa njia gani shule, matibabu, utalii, biashara au?

Ulitaka kwenda nchi gani?

Information gani unahitaji?

Okoa nguvu na muda.
Kifupi nahitaji connection haijalishi ni njia gani nitatumia .kingine mm mtoto wa kimasikini baba ,mama ndo Mimi kusema kutembea nitakudanganya ingwa kama kusoma ikitokea poa .lkn tusipende kuwaktisha wengine tamaa
 
Nahitaji kujua ni lini tuliwasiliana kabla ya leo, una uthibitisho wowote ule? Ulete hapa tafadhali.

Ni wapi nilikukatisha tamaa. Leta risiti mkuu.
 
We nae acha gubu Mbona anasaidia watu sana na laana zako hazimpati
Ulitaka akupe pesa wapo wengi kawasaidia tu na sio lazima yeye kuna wengine pia wanaweza saidia
 
Mpaka kumuhifadhi??? huo sasa ndio uboya wenyewe na hio ni spoon feeding. Jiulize sie wengine tuliingia hapa bila mjomba wala shangazi wa kutuhifadhi na bado tulitoboa. Wabongo wavivu wa kufikiri na kimatendo pia.
Ukishakua mbele unajiona sio mbongo tena,na unaanza kutusema.

Sikatai madai yako lakini pia diaspora wengi tukiwauliza jambo mnaishia kutuambia tucheki websites za nchi husika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…