Diaspora Hawatoi connection?

Diaspora Hawatoi connection?

Sema kwanini msingeunda group wanaotaka kwenda nje then mkapata wazoefu wakuwaongoza hii ushaur through id ambazo hujui ni nan ni shughuli

Fuatilia pages za EBM anatoa consultation for a small fee. Sisi wengine tunapenda anonymity.
 
Naandika huu uzi baada ya kusoma na kusikia mara kadhaa kwamba diaspora wabongo hawatoi connection za kwenda nje compared to diaspora wa nchi kama Kenya, Nigeria nk. Mimi kama diaspora napinga hii notion vikali.

Hapa JF Kuna nyuzi zaidi ya 100 zinazojadili jinsi ya kwenda nje, a quick search mtu unapata majibu yote na bado watu tunachangia nyuzi kila leo. Mnataka connection gani zaidi?

EBM anatoa free knowledge on YouTube na bloggers wengine jinsi ya kwenda nje, hiyo sio connection? Tuwape bundle za kuingia youtube au?

Mimi binafsi nimeshirikiana na watu kadhaa toka kwenye forum hii hii toka walipoanza harakati zao za kwenda nje na sasa wapo mbele needless to say walifanya sehemu zao na mambo yao yakafanikiwa. Sasa urafiki umekua undugu. Tatizo ndugu zangu wamatumbi mnapotaka connection mnataka hao diaspora wawape hadi hela na passport wawatafutie. You have to play your part as well.

Kimsingi kwenda nje is as easy as ABC. Kupata connection ni vizuri but isn't everything. Mimi nilienda bila connection yeyote ile, maelezo yote yapo kwenye websites za nchi husika ila ni lazima uwe tayari kufanya sehemu yako pia, kuna watu wanadhani diaspora wana a magic code ya kwenda nje this couldn't be further from the truth. Ni lazima uwe tayari kufanya sehemu yako.

Wabongo wenzangu punguzeni kulalamika kiboya, JF Kuna more than 100 threads, YouTube ipo, website za nchi husika zipo, tunajitoa as much as we can but we can only do so much. Maisha yako ni jukumu lako, kusaidiana kupo ila sio wajibu.

Nipo around mazee.



Mkuu kwa mfano mimi nakualika wewe kama nani yangu au kwenye function gani?

Nadhani wengi mnadhani mualiko wowote tu unatosha kupewa visa ila hamjui ni lazima muwe na ukaribu na huyo mtu na wewe as a visitor uonyeshe upo well established nyumbani na utarudi ili upewe visa kigezo ambacho vijana wengi hawana maana ndo wanatafuta maisha. Kama haupo vizuri bongo kwa maana ya a stable job au business, assets, ndoa, watoto, na hela visa ya kutembea kwa mualiko ni mtihani.

Niseme tu diapora wanatumia internet hii hii kutafuta hizo internships na kazi mnazotaka wawajulishe sio kwamba wanaenda kwenye hizo organizations in person. Wewe muhitaji ni bora kuwekeza nguvu nyingi kuzitafuta hizo nafasi, ukikpata ndo mshauriane na mtu wako wa karibu aliyeko huko. Hao diaspora wana majukumu mengine hawawezi kuacha majukumu yao na kushinda online siku nzima kukutafutia internships na kazi. Tujiongeze hapa tuache uzembe na lawama za reja reja.

Hakuna mtu anaogopa kuwapa muongozo ila you're asking way too much hata kwa mambo yaliyo ndani ya uwezo wenu. Mimi sina muda wa kumtafutia mtu chuo, passport au internship huo muda sina kabisa Ila akipata nitamsaidia all the way through ndo maana nilisema lazima ucheze part yako as well hakuna mtu ataacha majukumu yake kukusaidia wewe kila kitu.



Hifadhi, kazi, viza ya muda mrefu ni hadi ufike nchi husika. You will cross that bridge when you get to it. Step 1 ni kupata visa ya kwenda, kama huna uhakika wa visa ya kwenda kwanini uanzie kuumiza kichwa kwa mambo ya mbele?

Ukifika swala la visa ya muda mrefu ni kupewa the right information tu actions zote ni juu yako. Diaspora hawatoi visa au work permit wao, hakuna sababu ya kunyimwa information.

Kuhusu hifadhi sijawahi kusikia mtu kafika kakosa hifadhi, watu wanafika kila siku wanapewa hifadhi na watu baki kabisa na maisha yanaendelea.

Hizi lawama zenu hazina msingi wowote ni lazima ujisaidie kwanza ili usaidiwe. Hii mentality ya kwamba diaspora watakufanyia kila kitu ni ujinga.
meandika bango reeeeefu. Unataka connection ipi?

Unataka kwenda kufanya kazi wapi au ipi tukufahamishe namna ya kufikia malengo yako, wacha porojo.
 
meandika bango reeeeefu. Unataka connection ipi?

Unataka kwenda kufanya kazi wapi au ipi tukufahamishe namna ya kufikia malengo yako, wacha porojo.

Umepanic rudia kunisoma.
 
Mkuu@Bufa nakukubali sana ulimsaidia jamaa mmoja anaitwa DIBAJI ayekuwa ameshida dv lottery.
 
Ndo zangu mkuu, piga miguu yote kama Zizu 😅
Dah nishafeli nilikua nakufatilia sana kaka kwenye issue za madini unazijua sana lengo langu nikipata kihela nikutafute unipe abc za hiyo biashara ili nisije pigwa ikiwezekana tuwe wote kabisa huko chimbo kama ungekubali, dah basi tena. Sema mwamba nakukubali sana kwenye kushare experience mbali mbali hujivungi.
 
Dah nishafeli nilikua nakufatilia sana kaka kwenye issue za madini unazijua sana lengo langu nikipata kihela nikutafute unipe abc za hiyo biashara ili nisije pigwa ikiwezekana tuwe wote kabisa huko chimbo kama ungekubali, dah basi tena. Sema mwamba nakukubali sana kwenye kushare experience mbali mbali hujivungi.

Nashukuru sana mkuu. Nipo nje kitambo ila nakuja bongo oftentimes sio kwamba nimesepa hivi Karibuni labda hukujua Hilo.

Reach out anytime kubalishana mawazo ya madini au anything that I can help with.

Bado sijaandika uzi wangu mwenyewe wa sekta ya madini labda nitaandika huko mbeleni kwa kina zaidi ila kuna nyuzi za wadau nyingi zinaingia in details nimeweka comments mbili tatu huko.
 
Nashukuru sana mkuu. Nipo nje kitambo ila nakuja bongo oftentimes sio kwamba nimesepa hivi Karibuni labda hukujua Hilo.

Reach out anytime kubalishana mawazo ya madini au anything that I can help with.

Bado sijaandika uzi wangu mwenyewe wa sekta ya madini labda nitaandika huko mbeleni kwa kina zaidi ila kuna nyuzi za wadau nyingi zinaingia in details nimeweka comments mbili tatu huko.
Sawa mkuu nimekupata, sema ngoja tupambane na sie tuje kwa biden one day kujitafuta zaidi. Passport ipo mchawi visa tuu.
 
Back
Top Bottom