Wakuu nawasalimu,
Leo nimejikuta nawaza sana fursa walizonazo watanzania waishio nje ya nchi na namna ya kutatua changamoto za ajira kwa vijana
Kwanza naomba niwaalike watanzania wanoishi nje ya nchi kutufungua mawazo na kutupa uzoefu wa fursa mbalimbali zinazopatikana maeneo wanayoishi
Fursa inaweza kuwa kwenye:
- Kilimo
- Elimu
- Afya
- Usafiri
- Utalii
- Michezo
- Viwanda na biashara kadha wa kadha
Inawezekana pia umeona kitu Tanzania ambacho ni fursa nchi nyingine lakini hapa nyumbani tunakiona cha kawaida na kinyume chake pia. Nawakaribisha diaspora na vijana kubadilishana uzoefu na fursa mbalimbali zinazotuzunguka.