Diaspora: Nani yupo Moscow tuonane nipate kampani

Vipi mkuu, umeishakamata mtoto wa Kizungu?
Nipo vizuri sana nimebahatika kumpata mrembo wa kirusi ndo ananipa kampani kila kitu nmejiskia vile tu kama npo nyumbani hapa.
Watoto wa kirusi wameumbwa na kuumbika haswa ni rahisi kusahau kabisa kwenu.
Hapa anataka ajue hadi kiswahili eti nmekuwa mwalimu wa kiswahili mara hii.
 
Hahahaha! Huko ni hatari sana aisee! Nywele nyeupe au nyeusi?
 
Dah...hapo Moscow niliwahi kuishi Krivsck Town
 
njoo hapa Karibu lexis hotel pemben ya airport au nipm niuelekeze vizuri
 
Watanzania wanambwembwe jaman[emoji57] .Naangalia majibu mpaka raha.. Eti nlishawagi ishi huko kumbe hata paspot ya karatasi tu mtu hana.[emoji23] [emoji23]
 
Watanzania wanambwembwe jaman[emoji57] .Naangalia majibu mpaka raha.. Eti nlishawagi ishi huko kumbe hata paspot ya karatasi tu mtu hana.[emoji23] [emoji23]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] wanatumia Google alafu....
 
Watanzania wanambwembwe jaman[emoji57] .Naangalia majibu mpaka raha.. Eti nlishawagi ishi huko kumbe hata paspot ya karatasi tu mtu hana.[emoji23] [emoji23]
Kwani kuishi huko na kuwa na passport kwa zama hizi bado ni kitu cha ajabu sana mkuu? Wewe umetembelea wapi nje ya Tanzania?
 
View attachment 566354


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Mkurugenzi wa PPR Pascal Mayalla akiuliza suali katika mkutano na waandishi wa habari uliozungumzia Kongamano la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi Bi. Adila Hilali Vuai akijibu masuali yaliyoulizwa na wandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kongamano la kitafa litalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. (kushoto) Muandishi wa habari Rahma Suleiman wa Chuchu Fm Redio.
Picha na Makame Mshenga.
Wanabodi.

Declaration of interest. Japo mimi Paskali Mayalla sio mwana Diaspora, bali nimewahi kuishi nje kwa muda mfupi mfupi katika nchi mbalimbali, na nimewahi kufanya kazi tena sio kubeba box, bali kubeba zege ndani ya jiji la London, hivyo nina mwanga kidogo kuhusu diaspora, ila kwenye hili
Kongamano la Nne la Diaspora, litakalo fanyika Zanzibar, tarehe 23 na 24 Agosti, I have a role to play.

Hivyo hili ni bandiko la kuomba ushirikiano wenu, kwa ushiriki wako kwenye kongamano hili, physically or by proxy, ili kutoa mawazo yako Tanzania ikusaidiaje ili kukuwezesha wewe kuisaidia nchi yako.

Tanzania itajengwa na Watanzania wote wakiwemo wana diaspora. Kitu cha kwanza ni kuomba ushiriki wako physically kwa wale wenye nafasi to make it home, wajisajili kupitia
DIASPORA: Home Page
or
4TH Tanzania Diaspora Conference 2017 - Diaspora and SMEs ...

Kwa wale ambao hawatapata nafasi ya kuwepo physically, wanaweza kushiriki by proxy, kwa vile dunia sasa ni kijiji kimoja, wanaweza kushiriki by proxy.

Kwanza The Official Opening ya Kongamano lenyewe litatangazwa live za TV za Tanzania. Pili tutatangaza live kupitia video streaming kwenye youtube hivyo wana diaspora wote wenye nafasi wanaweza kufuatilia kupitia youtube, facebook, tweeter na mitandao ya kijamii.

Hapa naomba ushirikiano wako tujadiliane how to reach you out ili tupate maoni na mawazo yako, Tanzania ikusaidiaje wewe mwana Diaspora ili uweze kuisaidia nchi yako?.

Uzalendo sio kujiuliza "Tanzania Ikusaidie nini, bali ni wewe kujiuliza jee nimeisaidia nini nchi yangu Tanzania?". Kwa vile wana diaspora wengi wako nchi za nje na wamepata bahati ya kupata exposure kubwa, tunaomba mawazo yenu, Tanzania iwasaidieje ili muweze kuisaidia nchi yako Tanzania.

Natanguliza Shukrani.

Pascal Mayalla
+255 784 270403
pascomayalla@gmail.com
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…