Diaspora rudini nyumbani

Diaspora rudini nyumbani

Wimbo

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
866
Reaction score
625
Yapo mengi yatakayo washangaza, pale mtakaporudi, maisha hayo ya utumwa mliyonayo huko, ebu rudini nyumbani, huku nyumbani kumenoga, kama ni hizo kazi za kutunza wazee na kuosha vyombo mahotelini hata huku ziko rudini.

Wale ambao mlitusaliti baada ya kuelimishwa na Taifa tena bure mkakimbilia ulaya na Amerika kusaka hali bora na mishahara minono rudini huku kumeiva, ondoeni kizazi chenu katika maisha ya kubezwa na kuitwa manyani rudini nyumbani mbona tuko vizuri tu.

Rais Magufuli ameiteitengeneza Nchi usipime, njooni muyafaidi machozinya ya Watanzania tulimlilia Mungu akatupa kiongozi makini Nchi inakwenda kasi usipime.
 
Kinachowauma ni usaliti, walisomeshwa na nchi kwa fedha za walipa kodi halafu wakaona hawawezi kututumikia wananchi.
 
Kinachowauma ni usaliti, walisomeshwa na nchi kwa fedha za walipa kodi halafu wakaona hawawezi kututumikia wananchi.
Hakuna usaliti wowote kufanya kazi nje ya nchi.
Elewa dunia ya sasa imebadiĺika, watu wanaofanya kazi nje wanatoa mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya nchi kwa kutuma fedha za kigeni nyumbani.

Btw, una habari kuna vijana wengi wamesomeshwa na serikali kwa pesa nyingi na wako nyumbani hawana kazi?
Hao wanawatumikiaje waliowasomesha!
 
Kuna ndugu yetu aliondoka akaenda sweden kaishi miaka 24 akawa kutwa kututambia maisha yalivyo mazuri kule nk akipiga picha anavyo enjoy nk siku ikafika akafiwa na mama yake ikabidi arudi.Akakuta familia nzima wamnaenda mpokea akajua ohh kawaida!!

Kilichomshangaza akakuta ndugu zake wote wana magari.Akaambiwa msiba upo kwa mdogo wake wa mwisho .Kwenda hilo jumba alilolikuta hakuamini kama ni ya mdogo wake yeye miaka 24 kakaa ulaya yuko tu apartment anapanga hana cha kuonyesha!!!

Aliondoka kimya kimya baada ya msiba kurudi sweden ambako walishampa uraia.Sasa hivi hapigi simu email ukiandika hajibu!!!

anyway diaspora chumeni muje muwekeze kwenu msije sumbua watu mkifariki mnataka michango ya kusafirisha maiti itoke Tanzania
 
Wabeba boksi wengi wao wanahangaikia tumbo na rent maisha magumu sana kule
Yaan kila aliepo nje ni.mbeba maboksi.
According to data za wizara wengi waliopo nje ni wanafunzi na wafanya biashara.
Ni asilimia chache ambao wana permanent job huko.
Pamoja na baadhi ni walimu wa vyuo vikuu.

Sion haja ya kuponda watu walioko nje kisa wanatafuta life. Hiyo ni roho ya kimaskini
 
Kinachowauma ni usaliti, walisomeshwa na nchi kwa fedha za walipa kodi halafu wakaona hawawezi kututumikia wananchi.
Wengine wanasomeshwa na serikali nje ya nchi.
Na baadhi ya walimu wamepelekwa na serikal hii.kwenda kufundisha vyuo vya nje.
Uwe unafanya research kabla ya kuja ku project umaskin wako kwa watu waliopo nje. Na wao wana haki ya kutafuta riziki.
 
Kuna ndugu yetu aliondoka akaenda sweden kaishi miaka 24 akawa kutwa kututambia maisha yalivyo mazuri kule nk akipiga picha anavyo enjoy nk siku ikafika akafiwa na mama yake ikabidi arudi.Akakuta familia nzima wamnaenda mpokea akajua ohh kawaida!!

Kilichomshangaza akakuta ndugu zake wote wana magari.Akaambiwa msiba upo kwa mdogo wake wa mwisho .Kwenda hilo jumba alilolikuta hakuamini kama ni ya mdogo wake yeye miaka 24 kakaa ulaya yuko tu apartment anapanga hana cha kuonyesha!!!

Aliondoka kimya kimya baada ya msiba kurudi sweden ambako walishampa uraia.Sasa hivi hapigi simu email ukiandika hajibu!!!

anyway diaspora chumeni muje muwekeze kwenu msije sumbua watu mkifariki mnataka michango ya kusafirisha maiti itoke Tanzania
Huyo ndugu yako mmoja. Ha reflect matukio ya watu wote walioko nje.
Mbona wako wanaokuja kuzika na wanarudi nje kuendelea na kazi?
 
Tutumie nauli
Yapo mengi yatakayo washangaza, pale mtakaporudi, maisha hayo ya utumwa mliyonayo huko, ebu rudini nyumbani, huku nyumbani kumenoga, kama ni hizo kazi za kutunza wazee na kuosha vyombo mahotelini hata huku ziko rudini, wale ambao mlitusaliti baada ya kuelimishwa na Taifa tena bure mkakimbilia ulaya na Amerika kusaka hali bora na mishahara minono rudini huku kumeiva, ondoeni kizazi chenu katika maisha ya kubezwa na kuitwa manyani rudini nyumbani mbona tuko vizuri tu. Rais Magufuli ameiteitengeneza Nchi usipime, njooni muyafaidi machozinya ya Watanzania tulimlilia Mungu akatupa kiongozi makini Nchi inakwenda kasi usipime.
 
Huu uzi umekaa kimipasho sana. I'm still wondering how you can think without a brain.
 
Mtoa mada wewe mchawi.Sisi mdogo wetu yuko kwa bibi na anasomesha watoto watano sekondary kwenye ukoo wetu watoto wawili ni wa kwangu na mtu akifa kwenye ukoo rambirambi anatoa yeye .Mimi ndo mkubwa na nina madogo mengine Dar na Arusha laki yule wa ulaya ni msaada mkubwa kwetu.Mwaka jana kaniletea iPhone 8 alisema sio mpya lakini uku ni kama mpya....Wewe wacha UJINGA
 
Back
Top Bottom