Diaspora Vijana Watanzania wamlilia Rais Samia uraia pacha

Uhaini alipaswa awe behind bars choko baridi yule
 
Usalama wa nchi kwanza kwa hili Mimi siungi mkono hata kidogo
 
Hivi kwa nini topic kama hizi wanaoishi Tanzania huwa wanaongeaga kwa uchungu sana kuwaona waliopata uraia I wengine Kama wasaliti vile??

Kweli nakubaliana na mtazamo wako , baadhi ya wachache hawa wanaojiita wazalendo-ambao hawajavuka mipaka ya Tanzania katika kujadili hoja ikitumika emotion kali au kugubikwa na ukali wa chuki, wivu, kujiona dhalili basi ni vigumu kuona kitu chanya ambacho Diaspora ya kiTanzania inaweza kuchangia.
 
Umerogwa nini? Yule aliyekufa kwa kuombewa kifo na Askofu Mwamakula ulikuwa unamtetea hapa. Huyu naye unamtetea. Unatetea kila kitu. Tafuta mtu mwingine wa kuamini watu wa aina yako. Bendera kufuata upepo.
 
Hata Watanzania hawamiliki ardhi, serikali ndiyo inamiliki ardhi na siyo serikali bali ni Rais. Huu ni ujinga tuliokubali Watanzania. Ardhi ambayo mababu zetu walikuwa wanarithishana kwa karne na karne zilizopita, serikali ndiyo iliwapora Watanzania na ndiyo inamiliki sasa.
 

Bonge la pointi, katiba mpya lazima irudishe ardhi kwa mababu zetu, hili la Rais kuhodhi ardhi yote katika nchi ya mfumo wa Jamhuri / republic ndiyo tunaita usultani au ufalme katika joho la urais.

Ni nchi za kifalme ambapo ardhi ni ya watawala yaani mfalme/ malkia na hili sijui likiingiaje ktk nchi inayojiita Jamhuri. Na ndiyo maana watu wamebomolewa nyumba zao na ardhi kuporwa pale ilipompendeza mwendazake.

Hapa ndipo tunapoona katiba mpya ni jambo mtambuka muhimu inatakiwa kuchukua hoja nzuri kama za uraia pacha, umiliki wa ardhi, demokrasia, haki ya kuishi, uhuru, kutambua maendeleo ya watu n.k n.k
 

Kijitonyama,Mwenge
Dar es Salaam

Aomba Mh. Rais aingilie kati suala la ardhi yake, pia sera za uwekezaji kukosa uendelevu yaani kubadilika mara kwa mara na kuumiza wawekezaji

Babu alia kuporwa ardhi na serikali, ni mfano hai kuwa raia au wananchi hawamiliki ardhi hata kama waliipata kwa njia sahihi kabisa


Source : DarMpya TV
 
kushiriki katika ujenzi wa uchumi bila kificho au njia zisizo eleweka kisheria.

hawajasema wanataka kujenga uchumi.

wamesema wanataka kumiliki mali za Tanzania

Sasa kwa nini tumpe mtu ashikilie kiwanja Mbweni baharini sisi tubananishwe uswekeni Kijichi kwa Mfuga Mbwa wakati eneo zuri limeshikiliwa na Mmarekani sijui Mwingereza anaishi Sheffield, Uingereza ????

Over our dead bodies.

Tunapinga na kulaani.
 
Wewe Kijichi ushafika?
 
Wewe Kijichi ushafika?
Kitambo toka Kijichi ikiwa ni pori miaka kama 20 iliyopita

Kwani unakuona ni mbali sana au ?

Nilikuwa nina Coaster zinaanzia Tandika sokoni kwenda Kijichi, kwa nini nisifike Kijichi ?
 
Kitambo toka Kijichi ikiwa ni pori miaka kama 20 iliyopita

Kwani unakuona ni mbali sana au ?

Nilikuwa nina Coaster zinaanzia Tandika sokoni kwenda Kijichi, kwa nini nisifike Kijichi ?
Kijichi Kwa Mfuga Mbwa?
 
Kijichi Kwa Mfuga Mbwa?
Ndio, kama mita 200 kutoka shule ya Miande, kuna familia ilifuga mbwa na kupachikwa jina hilo na wenyeji. Lakini si kitongoji rasmi, na huenda historia hizi zikaenda zikisahaulika kama palivyo sehemu kama Makuti kwa Bi Nyau, sasa hivi paka hakuna na bibi alishakufa, na wakazi wengi wa Magomeni ya leo usikute hata hawapajui.

Tukirudi kwenye mada, kwa nini unauliza?

Hoja yangu haikueleweka nilipojieleza Kijiographia kuonyesha mbanano wa raia kwenye maeneo kama haya ?
 

Hiyo Kijichi Kwa Mfuga Mbwa umeitunga tu, hakuna mtu mwingine zaidi yako anayeijua.

Kijichi actually has some of the better places in Dar.

Which shows you don't know jack about Kijichi.

You are fibbing.
 
Hyphenated nationalities are abig NO!(in my opinion)
 
Mkuu, ikitokea huyo mmiliki wa kiwanja cha ufukweni Mbweni anaishi Manyoni Singida au Nzega Tabora, huku akiwa amewaacha wengine mmebanana huko "kwa mfuga mbwa" inakua ni sahihi ?
 
Usalama wa nchi kwanza kwa hili Mimi siungi mkono hata kidogo
Mkuu, inamaana nchi zote zilizoruhusu uraia pacha zinapitia changamoto za kiusalama ?

Unadhani kwa zama hizi za "dunia ni kijiji" kama nchi tunapaswa kushindwa kuhakikisha usalama wa nchi yetu eti kwa sababu baadhi ya raia wetu ni raia wa nchi nyingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…