Diaspora Vijana Watanzania wamlilia Rais Samia uraia pacha

Pole yao sana...

Ina maana kama umerithi ardhi alafu ukaja kua diaspora mbeleni automatic hizo ardhi zote huna haki nazo tena...
Unless uje kuziomba tena kama muwekezaji...
 
Kwa hili naunga mkono katika mambo mengi ya ovyo katika katiba ya tz na hili la kutoruhusu uraia pacha vizuri kuangaliwa tena kwa dunia ya sasa limepitwa na wakati
Wakati haupiti wewe ndio unapita. Kwenye masuala ya kitaifa hakuna kushindana hapa tunangalie maslahi mapana ya vizazi vyetu na si vinginevyo
 
19 year overseas and still kicking.

Nilishaacha kuiamini serikali ya CCM na agenda zake siku wakija kuamka watajua wanapata hasara kiasi gani.....

Jana wakati Jorge Luiz Frero "Jorginho" anafunga penalty kuwapeleka Azzuri fainali watu walipaswa kujua Jorginho ni mzaliwa wa Brazil na sio Italy!

Ipo siku wataamka
 
Mkuu, ikitokea huyo mmiliki wa kiwanja cha ufukweni Mbweni anaishi Manyoni Singida au Nzega Tabora, huku akiwa amewaacha wengine mmebanana huko "kwa mfuga mbwa" inakua ni sahihi ?
Ni sawa kwa sababu ni Mtanzania, anaishi Manyoni, Singida, moja

Mbilii, kiwanja chake cha Mbweni baharini atakuja kuishi mwanae Mtanzania, potentiallly.

Lakini huyo Mwingereza anaemiliki kiwanja Mbweni baharini, anaeishi Sheffileld, UK, kakishikilia ili nani aje kuishi ? Kwa nini tubananishwe kwenye squatters, Magomeni Makuti kwa Bi Nyau, halafu diaspora na matajiri wachache wamehodhi ardhi Mbweni baharini, tumekuwa Kenya ?

Over our cold dead bodies.

Lukuvi alishasema - labda abadilike aufyate mbele ya Rais mpya ambae hatakiwi kuwa na tamko juu ya ardhi ya Tanganyika tangia hapo- lakini Lukuvi alisema mtu anaemiliki real estate halafu hatumwoni, hatujui alipo, tusikie haishi hapa yuko sijui Dubai, tunakomba!

Hata awe Mtanzania. Sembuse Mswideni !!!
 

Kama wewe siyo mwanasiasa basi wanasiasa wanakuchuuza. Ukikomba mali ya mtu aliyejitambua basi utaishi maisha yasiyo na amani wewe pamoja na familia yako. Kumbuka wakati familia yako au wewe mwenyewe unapata purukushani, Lukuvi hayupo. Tena serikali unayoitegemea wala haitakusaidia ukipata matatizo.
 
It
Achana na uraia pacha hatutaki. Wapambane hukohuko kwao kupya. Uzalendo haugawanyiki. Uraia pacha ndio chanzo cha ujasusi wa mabeberu kufanikiwa hasa kuweza kuteka uchumi wenu.
 
It

Achana na uraia pacha hatutaki. Wapambane hukohuko kwao kupya. Uzalendo haugawanyiki. Uraia pacha ndio chanzo cha ujasusi wa mabeberu kufanikiwa hasa kuweza kuteka uchumi wenu.
Hao "mabeberu" uliowataja wameshindwa "kuteka" uchumi wa nchi gani kwa sababu hiyo nchi haina uraia pacha ?

Pia wameteka uchumi wa nchi ipi ambayo yenyewe ina uraia pacha ?
 

Mkuu unazo hoja kadhaa nzuri sana kwa ajili ya mjadala, ila ulivyosema Rais (wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) hana sauti yoyote juu ya ardhi ya Tanganyika, NGUVU ZIMENIISHIA KABISA.

Au ulimaanisha Rais wa TFF ?
 
Ardhi km ipo na haitumiki kuiletea maendeleo nchi, ni bora wauziwe diaspora waiendeleze iweze kuwa na tija

Tujifunze kwa wenzetu ghana ambao sheria zao za ardhi kidogo zimekuwa rafiki, now sekta ya real estate inakuwa kwa kasi sana na inachangia pato kubwa kwenye nchi. Na wamefanikiwa sababu wanunuzi wakubwa wa izo nyumba ni diaspora kwa sababu wazawa wengi kipato chao ni kidogo hawawezi kununua nyumba zenye thamani ya millioni 200

Sasa hpa kwetu sheria haziruhusu yaani hta ukijenga luxury apartments zenye thamani ya dola 300000 unapaswa kuwauzia wazawa na si wageni, sasa ndio ujiulize ni wazawa wangapi wana uwezo wa kununua apartment for almost million 700 za kitanzania? Kwa hyo utaona developers wana good product ila soko lipo very limited ndio sekta nzima ya real estate tanzania imedumaa.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Wasahau, tena huyu rais ambaye anaendeshwa na mfumo badala ya mawazo yake ndio wasahau kabisa. Kama mkwere alishindwa kwa huyu wasahau.
 
Unadhani zinataifishwa halafu anapewa mtu binafsi akae ? Kwani sisi wajinga ?

Nyumba za diaspora waliokana Utanzania na wanaishi nje ya nchi zinakombwa zinakuwa ofisi ya mganga wa mifugo wa wilaya.

Ukikana uraia wa Tanzania huna chako hapa, jijengeeni maisha huko huko mlipo Ulaya, Japan, Australia, Dubai... ukirudi tutakupa Visa ya siku 90 kama Mchina na Mhindi.
 

Kwa hiyo mganga naye maisha yake na familia yake hayana thamani kwako? Au wewe uko tayari kumtoa kafara ili uwakomoe diaspora?
 
Kwa hiyo mganga naye maisha yake na familia yake hayana thamani kwako? Au wewe uko tayari kumtoa kafara ili uwakomoe diaspora?

Achana nae ana vielement vya u narcissistic .....chuki kwa watanzania wenzake ndio hivyo,je wakija wageni huyu si atajinyonga?!
 
Uraia pacha ni muhimu sana mama samia ruhusu hii kitu
 
Kabla ya kukubaliana na hilo kwnz waeleze kwann walichaguwa uraia wa nje?
Hakuna uzalendo wa kweli kwenye uraia pacha..

uraia pacha ni sawa na mke kuolewa na waume wawili..
 
Kwa hiyo mganga naye maisha yake na familia yake hayana thamani kwako? Au wewe uko tayari kumtoa kafara ili uwakomoe diaspora?
Nimesema inakuwa ofisi ya maafisa wa wilaya

jengo la mwana diaspora limetwaliwa mazima, mchana kuna watumishi wanahudumia wananchi, usiku kuna SUMA JKT.


SERA YA ARDHI ya Tanzania inasema , kwa vile sisi Watanzania hatuna mahala pengine pa kwenda, ardhi ni kwa matumizi ya watanzania wote, sio kwa ajili ya kuhodhiwa na makabaila wachache.

NDIO MAANA TANZANIA huwezi kupata title dead kujenga residential ranch type zile za nyumba imezungukwa na li uwanja la kufugia farasi kama nyumba ya JR Ewing wa Marekani

HATUKUBALI!

SISI sio Kenya

Mida hii tuko kazini Tandahimba Gulioni, tunajenga nchi na tunatafuta mlo, the last thing we are thinking about is Uraia Pacha wa Diaspora waliohamia Uswizi! Kwa nini tuwape washikilie ardhi watu wanaishi Geneva ?????

Over our cold dead bodies!
 
Poor African soul. Kwa taarifa yako ardhi iliyokwisha kutumiwa na sisi wazalendo wa kuzaliwa hapa bongo haifikii hata nusu ya ardhi yote yenye kufaa kutumika tangu tupate uhuru.

Tunaiongelea ardhi wakati vichwani mwetu hatuna ubunifu wenye kulingana na ukubwa wa eneo tulilonalo!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…