Diaspora wa Kenya wafanya makubwa Marekani. Sisi Diaspora Wetu wanafanya nini cha kuonekana huko walipo?

Root cause ya tatizo ni mifumo yetu ya kimaisha, wenzetu Kenya wana access sana izi fursa za ughaibuni yaan mfano mdogo juzi tu hapa qatar WC 2022 wa kenya we gi walikuwa wana fanya kazi kule kama ma dereva ma steward ktk viwanja vya mipira, walinzi yaan
 
Well said. Mfano mwingine ni wa walimu wa kiswahili katika vyuo vya nje, wengi ni wakenya tena kwa mbali ukilinganisha na watanzania.
 
Hili swali ninajiulizaga sana na sijawahi kupata jibu, tunafanana na wakenya kwa mambo mengi sana! Lakini wapo mbele yetu kimaendeleo katika kila nyanja labda tunawapita kwenye music industry pekee.
Sijaijua sababu!!
 
Vipi Wakenya walio wekeza Tanzania na hawana Uraia pacha,, ndio matumaini.mnajipa?
Mkenya asiye na uraia pacha kaamua mwenyewe. Anaweza kwenda kokote kwingine kwenye uraia pacha akawa na uraia pacha.

Mtanzania hana option hiyo kabisa.

Yani ni kama watu wana option ya kupata mikopo.

Unaambiwa hii mikopo ni muhimu katika biashara, wape watu wako mikopo.

Unasema, vipi wanaofanya biashara bila mikopo?

Umeshindwa kuelewa tatizo, umeshindwa kuelewa suluhisho, umeshindwa kuelewa somo.

Halafu, hao diaspora mnaowasema na kuwanyima uraia pacha, mnapata wapi uhalali wa kuwasema ni wenu bado?

Yani watu wenu mmewatupa waende kuwa raia wa nchi za kigeni, uraia pacha hamtaki kuwapa, halafu bado mnataka waje wawekeze kwenye hiyo nchi yenu?

Wewe unaona hilo jambo liko sawa?
 
Chila hizi nchii duu especially Yemeni😂😂😂😂😂 Umenipanga mdogo wangu😂😂
 
mkuu nahisi tunachanganyana tu humu. Tanzania haina diaspora kwa sasa. Tuna wanafunzi au watumishi wa balozi wanaoishi nje ya nchi. Kenya wana raia wao wanaoishi huko ambao pia ni raia wa huko (duals), sisi hatuna. Hivyo hata wakifanya jambo wanajulikana kama raia wa huko Tanzania haihusiki. Mfano mzuri ni mtoto wa mzee Kimiti alivyotunukiwa medali ya heshima na malkia wa uingereza sisi hatukuwa na cha kujivunia maana yule sio mtanzania mwezetu ingawa alizaliwa Tanzania.
 
Hii ya umma wa waTanzania kufuatilia Diaspora ya kiTanzania wakati wala vumbi wanafanya kila aina ya juhudi ndugu zao katika diaspora wabeba box wasitambulike nyumbani iwe kwa sheria ya hadhi maalum au uraia pacha, nguvu hii ya kufuatilia maisha ya diaspora wanaitoa wapi ?

TOKA MAKTABA :

 
26 September 2011
- Tanzania's Foreign Affairs and International Co-operation minister Bernard K. Membe talks to VOA "Straight Talk Africa" host Shaka Ssali about the controversy surrounding the delay in the passage of the law to allow Tanzanians to hold dual citizenship.

Source :VOA News
 
Chila hizi nchii duu especially Yemeni😂😂😂😂😂 Umenipanga mdogo wangu😂😂
Kwann kaka?

Tuna nchi zime tuacha mbali sana...

Na nchi nyingi zina diaspora mfano mdogo Ethiopia ambao hawana uraia pacha...

Ukienda ktk nchi zenye uchumi wa juu na wana tukopesha na wapo ktk zile G8 sijui G ngapi

Kuna Japan

Kuna china ambayo tuna wategemea kwa mengi...

Twende N. Korea ambayo tuna pata misaada kutoka kwao pia... na wametuzidi mbali vilevile, kwa technology na mengine kibao

Twende Qatar sijui Saudia UAE nk ndio kabisa...

Rudi ktk nchi zilizopo ulaya mashariki ambazo pia zina tupiga tafu vilevile, Ukraine imetuwezesha kwa mengi, upande wa mikopo, elimu, afya nk

Poland vilevile...

Kuna mengi sana...
 
Wapo wengi, wakina Yusuf wa denmark

Yupo yule mwanamichezo wa Ujerumani aliyeshinda medali kibao...

Ni wengi mno...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…