Diaspora wa Kenya wafanya makubwa Marekani. Sisi Diaspora Wetu wanafanya nini cha kuonekana huko walipo?

Umemaliza....media hazina contents kabisaa..vululu vululu tu yaan...kaa asubuhi hadi usiku huwezi sikia vya maana🚮
 
Yemen nayo imepiga maendeleo?? Diaspora wetu Ni design ya Le tumboz u know**
 
walio jazana Tanzamia wao wana uraia pacha na Tanzania ndio maana wamejaaa huku? Visingizio vya kibongo
 
Siwalaumu Diaspora wa Tanzania kwa kiasi kikubwa japo wana madudu yao, Tatizo lipo kwa Serikali ya CCM, Watanzania wengi wanapata nafasi za kuingia huko kwa shida sana tena wakiwekewa vikwazo ndio maana unamkuta mtu mchango wake umejikita kifamilia tu, yaani kama anawasaidia ndugu zake inatosha. Kuhusu kuipigania nchi hilo swala tumeliacha kwa Makada na watoto wa viongozi ambao baba na mama zao ndio walamba asali. Huwezi kutokwa na jasho kuipigania nchi ambayo baba yake Wazir anaweza kusimama hadharani akatufokea, nchi ambayo ujinga ndio unaitwa uzalendo.
Tatizo la nchi yetu ni kutowekeza kwenye Akili, uwekezaji wetu umejikita kwenye matukio na kusifiana, yaani Akili kubwa kwa Tanzania ni adui wa Serikali. Kwahiyo huwezi kuishi US, UK na kwingineko halafu ukubali kuendeshwa na akili fupi za CCM.
 
walio jazana Tanzamia wao wana uraia pacha na Tanzania ndio maana wamejaaa huku? Visingizio vya kibongo
Mkuu,

Sasa diaspora ushamkataa kuwa si mbongo, hutaki kumpa uraia pacha awe na uraia wa bongo na huko aliko, halafu akileta visingizio unamsema ana visingizio vya kibongo?

Chagua moja ueleweke umesimamia wapi.
 
Wakenya wako Tanzania wanafanya makubwa na hawana urai Pacha, hebu acheni kujipa matumaini aisee, wakenya wamewekeza sana Tanzania vipi wana Uraia pacha?
Unajua kama Kenya ipo East Afrika umepata kusoma makubaliano ya muungano wa East Afrika?. Kenya shule zao wanafundisha elimu sisi Tanzania tunafundishwa uchawa na uzuzu. Sasa unategemea nini? Urai pacha una manufaa kwa mkaazi anawekeza kwao na ugenini.
 
Hili swali ninajiulizaga sana na sijawahi kupata jibu, tunafanana na wakenya kwa mambo mengi sana! Lakini wapo mbele yetu kimaendeleo katika kila nyanja labda tunawapita kwenye music industry pekee.
Sijaijua sababu!!
Mengine tunafanana kweli, lakini wenzetu kiingereza kinawa boost sana ,sisi tunajificha ficha tukiwa na wageni wanaozungumza English,

Hata huko Qatari wamechukuliwa kama wafanyakazi wa muda kwa mshahara Mdogo kwa kazi ili iwe rahisi kuwasiliana na wageni,

Nilikuwa nchi nyingine ya huko Arabuni , Kiki kuwa a waganda zaiidi ya 500 kwa hilo shirika wakifanya kazi ya ulinzi, na wakenya idadi kama hiyo wakifanya kazi za gardener, restaurant’s, warehousing, na kazi nyingine ndogondogo,

Lakini sababu kubwa ilikuwa ni kuwasiliana na mwajili kwa kiingereza,

Sisi hapa hakuna kampuni kubwa linaloweza kufikiria ku contract Watanzania kwa kazi hizo,

Hata mashirika ya Ndege kama Qatar air na Emirate, na Air hostess wake ya ni wengi, sababu rugha,

Hata mahotel mengine Dubai, Qatar, bahrain, nimekuta wakenya wapo,

Kwa hiyo suala sio diaspora tu , hata rugha inafanya tuweze julikana tupo
 
Wabongo wanachojua ni Uchawa,unafiki na kujipendekeza
 
walio jazana Tanzamia wao wana uraia pacha na Tanzania ndio maana wamejaaa huku? Visingizio vya kibongo
Yeye ana passport ya east africa, ila mtanzania ukichukua uraia wa nje sheria inasema umeukana utanzania kwa hiyo hatakuwa na access tena ya passport ya tanzania, tofaut sana na mkenya aliechukua uraia wa nje yeye anaweza kuja tanzania kufanya biashara kama east african, lakini mtz atakuja kama foreigner kabisa.
 
Wahindi waliotoka Uganda Kenya na Tanzania kila siku nakutana nao kama waswahili wenzangu hapa Uingereza. Wamewekeza India na wanapoenda hawana shida hata moja na mali zao serekali inawalinda. Unafaham hata Rishi Sunak ananyumba India na serekali inamlinda kama Muingereza mwenye asili ya India?

Uasilia umepotelea wapi? Inchi zote hizo zinawalinda wenye asili kwa namna moja ama nyingine. Ila wabongo hawana ulinzi wowote.

Sasa kwa hilo, looser ni nani?
 
Kaka mayala sio kila kinachofanyika lazima kitangazwe!!!Mbona watanzania wanafanya mengi tu huko nje!!!Hatuna sababu ya kujinadi vingine haviitaji kutangazwa au kuonyeshwa!!!!Mfano nikiwa nawafanyia kazi MOSSAD mpaka nijitangaze?
Ajabu kufungua mgahawa nacho ni kitu cha kupost humu kuna watanzania wanafanya makubwa mno nje, mleta post hana exposure ushamba unamsumbua
 
Acha kulinganisha akili na matapishi, hizo nchi zinathamini watu wao hata kama hawana uraia pacha, bongo ukiwa diaspora hata kufungua account ya Bank ni issue, kwa sasa hata kama una hela zako ukitaka kiwanja cha kujenga au kufungua business ni almost impossible labda udanganye danganye , watu gani mnakataa hela tena dollar ambayo sasa hamna, ila waarabu, wahindi na mabeberu wanawapiga na wanachota wanavyotaka, Kenya wanajitambua na kwa sasa sekta inayoongoza kuingiza fedha za kigeni Kenya ni diaspora hata utalii wao na chai havifikii, na pesa ya diaspora inaingia moja kwa moja kwenye Economy ya nchi inakuwa na faida mara mbili kwa Taifa, lakini inajulikana maskini wana madharau ya kijinga sana
 
Tukiacha ushabiki na kulishwa maneno kama majibu ya maswali yote mawili kwako ni "Ndiyo" basi unatakiwa kuunga mkono dual citizenship kwa wazawa wa Tanzania



1. Je unataka Watanzania wazawa ambao wako nje (Disapora) wapate haki sawa kwenye jumuia ya Africa mashariki kama wenzao wa Kenya na nchi nyingine? Kwa sheria za sasa diaspora wa kenya ana haki nyingi Tanzania kuliko diaspora ambaye ni mzawa wa Tanzania kwasababu diaspora wa Kenya anakuja kama Raia wa Kenya na huyu wa Tanzania anakuja kama mgeni/tourist.



2. Je unataka Watanzania Dispora huko walipo wawe ha haki sawa kama diaspora wa nchi nyingine?.



Hakuna Mtanzania namjua mimi amewahi kukana Uraia. Kukana Uraia ni utaratibu ambao una kuwa na barua ha hati ya kukana au kiapo cha kukana. Sifahamu mtu ambaye amekana Uraia wa Tanzania. Sheria ya Tanzania ndiyo inalazimisha neno Kukana na hii ndiyo kesi iliyopo mahakamani.



Uraia wa huko wanapoishi utawasaidia mambo ya msingi kama

(1) Kupata kazi nzuri

(2) Kupata bima za maisha

(3) Kuweza kusomesha watoto

(4) Kuhakikisha uwekezaji wao unalindwa kisheria.



Ngoja niwape mfano mdogo mimi binafsi mke wangu ambaye hakuwa na Uraia wa USA alikuwa na kuumwa sawa baada ya kumleta kutoka Tanzania. Tulipoenda Hospitali wakasema ni lazima afanyiwe operesheni haraka sana Vipimo tu vilikuwa $30,000 lakini operesheni ilikuwa $235,000. Mimi kwasababu ya bima yangu ambayo nisingeweza kuipata kama nisingekuwa Raia nililipia $3,000 tu na sio $265,000 ambazo ni gharama halisi. Hata Watanzania wenzangu wasingeweza kunisaidia.



Hizi ndiyo sababu kubwa za diaspora kuchukuwa Uraia wa nchi nyingine. Huwezi kukaa sehemu unafanya kazi usaidie familia nyumbani halafu tena kuna haki huna wakati wenzako wa kenya ambao mnashindana kwenye kazi hizo hizo wana haki zote. Hivyo badala ya kulishwa maneno tuwaulize kwanza diaspora ni kwanini wamechukuwa Uraia wa nchi wanazokaa na majibu kwa wanaojua sio ya kibinafsi bali ni ya kifamilia.



Hii ndiyo sababu umeona mabalozi wengi wa Tanzania wanaunga mkono kwasababu wanaelewa maisha halisi ya huku.

Nakuunga mkono, mimi na wife wangu kwanza tulihamia UK, kisha US, mimi nimeendelea kuwa Mtanzania, mwenzangu ni US subject, nilipopata ile ajali, nimetibiwa na support from her!.



Watanzania wengi wanaojilipua, wanajilipua kwasababu ya circumstances na sio kuukana Utanzania wao. Turuhusu dual citizenship!.



Tukiruhusu dual citizenship, diaspora wetu, watafanya mambo makubwa kama diaspora wa India, Nigeria, Ghana na Kenya.

Haya mambo ya diaspora tumeyaongea sana humu

Wana Diaspora, naomba ushirikiano wenu; tukutane, tujadili Tanzania ikusaidieje ili uisaidie nchi yako?
Msikilize Mwana Diaspora Huyu. Asema Mazito na Ya Msingi Kuhusu Diaspora Watanzania
https://www.jamiiforums.com/threads/diaspora-wa-kenya-wafanya-makubwa- Sweden P
 
Wengi wao ni matapeli,mtu anawaosha wazee anaweza fanya kipi Cha maana?
 
Niko hapa US kwa ziara binafsi, nimejaribu kutafuta vitu vya kuandika kuhusu Diaspora wetu, sikupata, hivyo hili swali kuhusu diaspora wetu, bado liko valid!。 Diaspora Wetu Wanafanya Nini cha Kuonekanika Huko Ughaibuni?. Diaspora Mliofanikiwa, Onekanikeni Kupitia TAK na Rudisheni Tanzania Japo Kidogo!
P
 
Kenya wamewapa watu wao walio nje haki ya kuwa na uraia pacha.

Nyie mnakataa halafu mnawang'onga kuwa ni "diaspora wetu".

Acheni ujinga.
Mchakato wa uraia pacha unaendelea na soon utakamilika.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…