Diaspora wafungua kesi ya Kikatiba kupinga sheria inayozuia Uraia Pacha

Diaspora wafungua kesi ya Kikatiba kupinga sheria inayozuia Uraia Pacha

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
WATANZANIA sita waishio nje ya nchi (DIASPORA), wamefungua kesi ya kikatiba Na. 18/2022 katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu, ya Dar es Salaam, kupinga vifungu vya sheria vinavyozuia uraia pacha, wakidai ni batili kwa kuwa vinakiuka haki yao ya kikatiba ya kuwa raia wa kuzaliwa.

---
Suala la kuwa na Uraia wa zaidi ya nchi moja maarufu kama ‘Uraia Pacha’ sasa limechukua sura mpya baada ya Watanzania 6 wanaoishi na kufanya kazi nje ya nchi kufungua kesi ya Kikatiba kupinga sheria inayozuia uraia pacha.

Kesi hiyo ya Kikatiba namba 18 ya mwaka 2022 imefunguliwa Mahakama Kuu Masjala Kuu na Shaban Fundi, Patrick Nyelesa Nhigula, Restuta Kalemera, Nkole Muya, Emmanuel Emmanuel na Bashir Kassam dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Kwa mujibu wa viapo vyao, hawa ni Watanzania kwa kuzaliwa walioondoka nchini na kwenda ughaibuni kwa nyakati tofauti tofauti hususani katika nchi za Marekani, Uingereza na Canada wanakoishi na kufanya kazi ambako pia walishapata uraia.

Wakili wa wadai hao, Peter Kibatala alisema kuwa kesi hiyo tayari imepangiwa jopo la majaji 3 watakaoisikiliza wakiongozwa na Jaji Mustafa Ismail akishirikiana na Jaji Hamidu Mwanga na Jaji Obadia Bwegoge, imepangwa kuanza kutajwa Februari 20, 2023

Katika kesi hiyo wanaiomba Mahakama itamke kuwa vifungu vya Sheria ya Uraia vinavyozuia uraia pacha ni batili wakidai kuwa vinakiuka haki zao za Kikatiba kwa kuwa vinawanyanya haki ya asili isiyonyang’anyika yaani uraia wa kuzaliwa.

Vifungu hivyo wanavyopinga ni pamoja na kifungu cha 7(1) na (2) (c), (4)(a) (6) vya Sheria ya Uraia ambavyo wanadai kuwa vinakiuka haki zao nyingine za Kikatiba.

Katika viapo vyao wanaeleza kuwa wameathirika sana kitendo cha kunyimwa haki mbalimbali katika nchi yao waliyozaliwa kwa kuzingatia kwamba walipata uraia wa nchi hizo kwa sababu za kiuchumi na ustawi wa kijamii.

Wanadai kuwa wao ni Watanzania kwa damu na kwamba wanatamani kuendelea kuwa Watanzania, lakini kwa vifungu hivyo vya Sheria ya Uraia wananyimwa haki hiyo.

Wanadai kuwa wenzao wanaotoka katika nchi nyingine za Afrika Mashariki kama vile Kenya, Rwanda na Uganda, wanaoishi nje ya nchi wanaruhusiwa kuwa hati za kusafiria za Afrika Mashariki kwa kuwa nchi zao zinaruhusu uraia pacha lakini wao hawawezi kupata hati hizo.

Miongoni mwa haki wanazozikosa nchini walikozaliwa ni pamoja na kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi na kwamba wanapotembelea nchini wanaishia kuishi katika nyumba za ndugu zao au hotelini.

Wanataja haki nyingine wanazozikosa kuwa ni pamoja na kutokuchagua viongozi wala kushiriki kugombea nafasi ya umma katika uchaguzi nchini.

Akizungumzia msingi wa kufungua kesi hiyo, Wakili Kibatala alisema kuwa hoja ya hoja zinazotolewa kupinga uraia pacha ni madai kuwa ni hatari kwa usalama wa Taifa.

Hata hivyo, alisema kuwa hoja hizo ni hoja mgando ambazo hazina mashiko huku akitolea mfano wa mtoto wa Rais wa Liberia ambaye anachezea Timu ya Taifa ya Marekani kwa kuwa ana uraia wa nchi mbili na hakuna tatizo.

Alisema kuwa kama kesi hiyo itafika hatua ya kusikilizwa hoja za msingi baada ya kuvuka hatua ya mapingamizi ya Serikali kama yataibuliwa, anaamini kuwa wana hoja za kuishawishi mahakama.
 
WATANZANIA sita waishio nje ya nchi (DIASPORA), wamefungua kesi ya kikatiba Na. 18/2022 katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu, ya Dar es Salaam, kupinga vifungu vya sheria vinavyozuia uraia pacha, wakidai ni batili kwa kuwa vinakiuka haki yao ya kikatiba ya kuwa raia wa kuzaliwa.
Katiba ipi ?
 
Wantanzania wenye akili wwmefungua kesi ya kikatiba

Safi sana
 
Taarifa mpya inaonyesha kwamba Watanzania 6 waishio nje ya nchi ( Diaspora ) , wamefungua kesi ya Kikatiba Namba 18/2022 Mahakama Kuu , Masjala ya Dar es Salaam .

Wanapinga vifungu vya Sheria vinavyozuia Uraia Pacha , Wakidai ni batili kwa kuwa vinakiuka haki yao ya kikatiba ya kuwa Raia wa kuzaliwa .

Wanawakilishwa na Wakili Msomi Peter Kibatala .

Chanzo : MwanaHalisi Digital
 
Lazima Ni machadema hayo ndio wanataka na kukazania suala Hilo ili watoto wao wanaoendelea kula kwa mrija huko wapate fursa hiyo, Maana wanachadema wanachadema wanajifanyaga wazalendo na kuhamasisha watanzania kuandamana kumbe wanajuwa watoto wao wapo huko ulaya na marekani ambako hawawezi kuguswa Wala kufikiwa na Moshi wa mahomu.

Lakini pia hao Chadema huwa wanabeza na kuongea maneno ya kumkatisha Tamaa kwa serikali unapokuwa inaboresha huduma za kijamii Kama Elimu na Afya kwa kuwa wanajuwa watoto wao hawapo hapa nchini na hata wao wakiumwa wanajuwa watatibiwa huko huko,Hii ndio sababu kwa Sasa upinzani unapuuzwa Sana hapa nchini
 
Lazima Ni machadema hayo ndio wanataka na kukazania suala Hilo ili watoto wao wanaoendelea kula kwa mrija huko wapate fursa hiyo, Maana wanachadema wanachadema wanajifanyaga wazalendo na kuhamasisha watanzania kuandamana kumbe wanajuwa watoto wao wapo huko ulaya na marekani ambako hawawezi kuguswa Wala kufikiwa na Moshi wa mahomu. Lakini pia hao Chadema huwa wanabeza na kuongea maneno ya kumkatisha Tamaa kwa serikali unapokuwa inaboresha huduma za kijamii Kama Elimu na Afya kwa kuwa wanajuwa watoto wao hawapo hapa nchini na hata wao wakiumwa wanajuwa watatibiwa huko huko,Hii ndio sababu kwa Sasa upinzani unapuuzwa Sana hapa nchini
We bonge la mshmba ujuwe

Ova
 
Unazijua faida za Uraia pacha ?
 
Back
Top Bottom