Diaspora wafungua kesi ya Kikatiba kupinga sheria inayozuia Uraia Pacha

Wewe jikite kusomesha watoto wetu, kutwa kuchwa upo humu kwenye siasa ndio maana mtihani inafutwa kila kukicha...
Hii ya uraia pacha, na sijui CIA, MOSSAD sio mitaala ya NACTE....
Asilimia 50 ya marais wa NCHI YETU ni walimu hadi ukombozi ulifanywa na walimu,Sasa kwanini mi nijidharau nikae Mbali na maswala ya NCHI Hii!!?


KILA mwaka ufaulu unapanda,na Mimi napandisha uelewa wa maswala MTAMBUKA ya nchi YANGU!
 
Kesi imeisha hiyo. Dead on arrival.
hao majaji ni pure serekali.
 
uraia pacha unakatwazwa kwa sababu za kiusalama,utakuta mtu ni mzaliwa wa TANZANIA,lakini pia ni raia wa USA matokeo yake anatumika kama agent au jasusi la CIA kuivuruga nchi aliyozaliwa!!!
 
Suala la ardhi kwa wana diaspora wakitaka kumiliki ardhi Tanzania mijini na vijijini

From 24:25"
Land holding patterns in Tanzania, both rural and urban areas


Katiba mpya itakayo zungumzia mambo muhimu yote ikiwemo uraia na umiliki ardhi pia. Ili nchi iaminike kwa uwekezaji mdogo, uwekezaji mkubwa umiliki ardhi ni suala la kipaumbele. Ili nchi iendelee inahitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa safi na Uongozi bora.

Watu ni raia wote iwe wenye uraia pacha, wakulima, wadau wa maendeleo, wafanyabiashara, wafugaji wav8vi n.k na hawa wote wanahitaji Ardhi inayomilikiwa kusheria kupitia hatimiliki , Siasa Safi iliyo wazi transparency na Uongozi bora endelevu usiobadili badili mambo ya msingi yanayogusa watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora .

Ardhi ni mtaji (capital) kujenga kiwanda/ kulima/ kuombea mkopo/ kujenga makazi n.k , ardhi ni urithi / utambulisho na suala la umiliki ardhi halitakiwi tu wapate wenye nguvu ya kifedha au kupitia vyeo vya kiutawala bali hata wananchi wa kawaida wa vijijini na diaspora ya 'wabeba box' walindwe kwa kupewa hati miliki za ardhi .


18 December 2022
Kijiji cha Mbigiri
Wilayani Kilosa
Morogoro, Tanzania

 
uraia pacha unakatwazwa kwa sababu za kiusalama,utakuta mtu ni mzaliwa wa TANZANIA,lakini pia ni raia wa USA matokeo yake anatumika kama agent au jasusi la CIA kuivuruga nchi aliyozaliwa!!!
Mbona akina Makamba, Pina Chana wamepewa mpaka ubunge na uwaziri, au kila mtu adanganye? Maana Tz, uongo, rushwa na kuoinda Sheria ndio maisha ya kila siku. Sasa waTz wengine hawataki kuvunja Sheria, mambo yawekwe wazi kikatiba.
 
Huo uTanzania wanautoa wapi wakati tiari ni raia wa hayo mataifa mengine? semeni "wamarekani wenye asili ya Tanzania..."
Kama ulivyosema wenye asili. Asili ya mtu inapotea aje?
 
Hao naona kama wanatwanga maji kwenye kinu

Ova
 
CelebAfrica Ep 4: Utata wa uraia pacha kwa baadhi ya nchi kama Croatia, Germany, Panama, South Korea, Slovakia n.k pia nchi kama Mareakani haitambui kanusho la uraia hivyo hunyangaywi passport yako

Katika kipengele hiki kifupi, Mubelwa Bandio anakupitisha kwenye baadhi ya nchi ambazo licha ya kutoruhusu uraia pacha kwa wazawa wake, bado zina namna ya uraia pacha ambao zaidi ni kwa wageni, wawekezaji na watu wanaopokea uraia wa mataifa yao bila kupoteza uraia wa nchi wanakotoka.

Kipengele hiki ni sehemu ya kipindi cha CelebAfrica kinachoonekana kupitia Clouds Plus TV (DSTV 294) kila Jumamosi kuanzia saa kumi na mbili kamili jioni kwa majira ya Afrika Mashariki
Source : Kwanza Production
 
Watoto wa mawaziri na mawaziri wengi wapo na passport za nchi mbili, Tanganyika na US, UK ama kwengineko ila hawataki wanyonge wawe na sehemu mbili
 
Mfano nani mwenye uraia pacha??
Magabacholi wote wana uraia pacha ukiachia Wazanzibari wenye uraia wa Zenj na wa Tanzania. Pia, hata waziri wetu wa zamani wa mambo ya nje Mulamula siwezi kumsemea.
 
Ahsante sana Bagamoyo,
Mimi nimesoma hii hukumu yote nimemaliza,

Tatizo kubwa kwetu Watanzania, mtu yupo tayari kuchangia, kubisha, lakini ukimpa ushahidi kama huu ili ajiridhishe, anaona ni upotezaji wa muda,

Ahsante sana tena
 
Upo sahii
 
New York US

URAIA PACHA, URAIA WA HADHI MAALUMU NA HAKI YA ULIPOZALIWA


Diaspora | Tanzanian Fighting for Dual Citizenship and Birthright, Hajji Khamis -New York, US
Source : Swahili villa online tv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…