Natafuta Ajira
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 9,016
- 24,650
RC alivamia studio akalazimisha kuingilia kazi za watu. Acha kuzunguka mbuyu kaka mkubwa.Kule kwa RC ku creates TV contents, ni yeye kujiongeza, he has always been doing that, na hata sasa hapo Chuga tayari amejiongeza
Amecreate Soon atarushwa hewani.
Ukisubiri Media ndio wakucretie, utasubiri sana
P
You are boring me.Ukiritimba ni kweli upo, fallacies pia zipo, ila pia kuna some logical as well. Kama mtakumbuka enzi za misaada yenye masherti, anayesaidia ndie anaamua asaidie nini, watu hawana maji, barabara wala kituo cha afya, wanaletewa mradi wa bembea za watoto.
Wafadhili ndio walikuwa wanaamua watafadhili nini, Nyerere alikataa, Mwinyi akakubali.
Mkapa akawaelimisha watuulize tuna shida gani na tunahitaji nini ndipo watusaidie, ndipo basket funding ikawa introduced, fedha zote za wafadhili zinaingizwa kwenye kapu moja, na sisi ndio tunaamua tufanyie miradi gani, including general budget support.
Japo beggers can not be chooses, mtu mwenye njaa ya kitoweo, badala ya kumpa msaada wa samaki, ale, akimaliza aombe tena, na tena na tena, hivyo kuwa ni omba omba, mfudishe kuvua samaki, mpatie nyenzo za uvuvi, ajitegemee.
Ndio maana tulishauri Hata Nyerere alikataa, Rais Magufuli usikubali, shikilia msimamo. Tanzania tusikubali misaada na mikopo yenye masharti kuingilia sovereignty yetu
P
Sorry, next time when bored, just ignore!You are boring me.
Hapana, usinipangie, nitakwambia tu ili ujue what is boring.Sorry, next time when bored, just ignore!
P
Take it from me, hakuvamia bali ni alikwenda kibabe kwasababu it wasn't the first time!.RC alivamia studio akalazimisha kuingilia kazi za watu. Acha kuzunguka mbuyu kaka mkubwa.
Paskal mimi siyo mgeni humu ndani.Kauli huumba, kwasababu Mungu na shetani, wote wawili hukaa ndani yetu, ukiwaza mema, ukisema mema na kutenda mema, yote hayo ni ya Mungu aliye ndani yako, hivyo mtu ukimsemea mema, kauli yako inamuumbia mema na yanatokea.
Ukiwaza mabaya, kusema mabaya na kutenda maovu ni shetani aliye ndani yako, hivyo hii kauli yako inaweza kweli kuniumbia kufeli.
Kwa vile mimi ni mtu very honest (ukiondoa mambo
Yetu yale) na kipindi cha TAK, ni kipindi very genuine kusaidia, hakina any ill motives wala agenda zozote, then wish yako ni wish ya kishetani, kikifeli ni shetani
ameshinda, nitakuwa sina jinsi kwasababu kuna wakati Mungu humruhusu shetani kushinda.
P
Tz hii hii ambayo hata kupewa passport wanaona kama vile wanakusaidia sana haijalishi una kila nyaraka. Yani sijawahi kuelewa kwanini eti ukipata safari ndo ukaombe passport.Wanabodi,
Bado niko hapa nchini Marekani kwa ziara binafsi, nimejitahidi kujichanganya na baadhi ya wana diaspora wa Tanzania walioko nchini Marekani, na kujiuliza jee wana Dispora wetu, wanafanya nini cha kueleweka na cha kuonekanika?.
Nimejitahidi kuwasiliana na kile chama cha DICOTA, sikubahatika kupata ushirikiano mzuri, ila nitaendelea kuwatafuta Diaspora wetu waliofanikiwa Marekani, wanafanya nini, na hayo mafanikio yao, yanaifaidia vipi nchi yao ya Tanzania?.
Kwa kupitia juhudi binafsi, nimefanikiwa kumuona dada mmoja wa Kitanzania, aliyehamia Marekani, mwaka 1999, na yuko kule mpaka leo. Huyu dada, naomba nisimtaje jina kwasababu sikumwambia kuwa nitaandika. Nime note Diaspora wa Tanzania waliofanikiwa hapa nchini Marekani, hawapendi kutajwa au kuandikwa wanafanya nini Marekani.
Huyu Dada ni mmiliki wa kampuni inayo fanya biashara ya huduma, services industry, ameajiri watu zaidi ya 50, kila mwezi anawalipa mishahara ya zaidi ya milioni 500.
Dada kanikaribisha kwake, ana kaa mtaa wa kitajiri, anamiliki nyumba, kubwa ya ghorofa tatu na ana magari 5 ya kifahari, ikiwemo Benzi ya G Wagon na gari ya Kimarekani ya Tesla inayotumia umeme. Hesabu ya haraka haraka ya thamani ya magari ni zaidi ya Shilingi Bilioni 1 ya Kitanzania.
Huu ni mfano mmoja tuu wa Mtanzania aliyefanikiwa Marekani, ametoa ajira kwa watu, na kutengeneza faida kubwa. Nilipomuuliza kwanini asiwekeze Tanzania, alinijibu anasubiria uraia pacha, ndipo aje kuwekeza Tanzania.
Imetokea tuu mimi ninamfahamu huyu Dada, mpaka kule kijijini kwao, Sanya Juu Moshi, ambako mimi nimefika, na kabla sijakwenda Marekani, nilipita hapo kwao Sanya, sasa hali niliyoiona ya umasikini wa hapo kijijini kwao, nikilinganisha na maisha ya kitajiri na kifahari anayoishi Marekani, ni mbingu na nchi!.
Hivyo huu ni wito kwa serikali yetu kuharakisha mkakati wa uraia pacha, ili Diaspora wa Tanzania waliofanikiwa ughaibuni, waje kuwekeza nyumbani Tanzania na kurudisha shukrani nyumbani Tanzania na sio kupiga tuu mapicha kurungishia mandinga yao makali ya ma G-Wagon na ma Tesla!.
Mtu Mtanzania ana magari matano ya kifahari, nchini Marekani, anaendesha kwa kubadilisha tuu magari, halafu ile hospitali ya Kibon’goto pale Sanya, kuna wamama wajawazito, wanajifungulia chini kwa kukosa, kitanda, ile G-Wagon moja tuu, ingejaza vitanda hospitali nzima, au ma deski shule nzima!.
Nimetembelea maeneo mbalimbali ya Marekani labda nitaona mafanikio ya kuonekanika ya Diaspora wa Tanzania, zaidi ya huyu dada kunikaribisha kwake, sikufanikiwa kuona kitega uchumi chochote cha Mtanzania nchini Marekani, kila rais wetu akija Marekani ni kukutana na Watanzania waishio Marekani, na kubadilisha mawazo tuu, Rais wa Kenya akija Marekani ni anafungua miradi ya Diaspora wa Kenya.
Muda aliokuja Marekani, huyu mdada wa Tanzania, ule mwaka 1999, ni muda huo Mkenya Kevin Onyona, alihamia Marekani, na kuajiriwa na Home Depot, kampuni ya kimataifa ya uboreshaji wa nyumba ya Marekani. Sasa hivi Kevin ni mmiliki ya migahawa ya Swahili Village ambayo ni mojawapo ya mikahawa bora zaidi ya vyakula vya Kiafrika nchini Marekani.
Kevin Onyona alianzisha mlolongo huo mwaka wa 2016, na leo inajivunia migahawa mitatu. Miaka sita baadaye, ametumia migahawa yake kujenga uhusiano halisi kati ya utamaduni wa Kiafrika na dunia nzima. Mkahawa mkuu wa Swahili Village oko Rhode Island Ave, Beltsville. Migahawa mingine miwili iko Washington DC na New Jersey. Mgahawa wa Washington DC ulifunguliwa na aliyekuwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kiongozi gani wa Kitanzania aliwahi kufungua mradi wowote wa Diaspora wa Tanzania nje ya Nchi?
Wito kwa Diaspora wetu, najua kuna uwezekano kuna mambo makubwa mazuri ya kuonekanika Diaspora wa Tanzania wanafanya, lakini hatuyaoni na hatuyajuo, hivyo natoa wito kwa Diaspora wetu, anekanikeni basi, inaumiza kila siku unaona diaspora wa wenzetu, na kujiuliza diaspora wetu wako wapi na wanafanya nini?.
Sasa mimi mwandishi wakp wa habari na mtangazaji wa kujitegemea, Pascal Mayalla, , anayeandaa vipindi vya TV, Redio, makala magazetini na kwenye mitandao ya kijamii, nikifanya kazi kupitia kampuni ya PPR, www.ppr.co.tz, ambayo sasa imetua rasmi nchini Marekani kwa kufungua ofisi, nimejotolea kuandaa vipindi vya mchango wa diaspora wa Tanzania kwa maendeleo ya taifa.
Kipindi Kipya cha TAK
TAK ni kipindi kipya cha TV chenye lengo la kuiangazia Tanzania Kitaifa, Kikanda na Kimataifa kuhusu mambo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, ambayo yanaihusu Tanzania kwenye medani za kimataifa, kama issues za Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola, issues za kikanda na kimataifa, AU, SADC, AfCFTA, Bunge la Afrika, Bunge la EAC, Jumuiya ya Africa Mashariki, EAC na mambo mengine ya kimataifa. Kipindi hiki kitaimulika Tanzania kwenye mikutano ya kimataifa, ukiwemo mchango wa Diaspora wa Tanzania, na wakati huo huo kuangazia fursa mbalimbali za kimataifa kwa Watanzania kuzichangamkia.
Kipindi hiki kitarushwa kwenye local channels za TV za Tanzania, DSTV, Star Times na kwenye online media.
Mimi kama Mtanzania Mzalendo, ninaumia sana kila ninapoona diaspora wa wenzetu wanafanya mambo makubwa ya kuonekanika, na kujiuliza Diaspora wetu wanafanya nini?, mbona hatuwaoni?, hivyo napenda kuona Tanzania tunafaidika na mchango wa wana diaspora wetu wenye exposure kubwa huko walipo, kuitumia kulisaidia taifa letu kisiasa, kiuchumi cha kijamii.
Paskali
Rejea za Mwandishi Kuhusu Diaspora
- Wana Diaspora, naomba ushirikiano wenu; tukutane, tujadili Tanzania ikusaidieje ili uisaidie nchi yako?
- Diaspora wa Kenya wafanya makubwa Marekani. Sisi Diaspora Wetu wanafanya nini cha kuonekana huko walipo?
- Msikilize Mwana Diaspora Huyu. Asema Mazito na Ya Msingi Kuhusu Diaspora Watanzania
- Je, Diaspora wetu wana mchango wowote kuisaidia Tanzania kisiasa? Wana any influence kwenye siasa za nchi yetu? Angalia Diaspora wa India
- Diaspora: Mkakati wa diaspora katika dual citizenship
- Kutoka Sea Cliff Hotel, Zanzibar: Kongamano la Nne la Diaspora
- Weekend Story! (Diaspora Vs Struggling Model)
- Balozi Dr.Wilbroad Slaa kuwa mwenyekiti tamasha la diaspora Sweden
Duh....!, yaani nikaombe funds kwa diaspora!.Hii ndio nia ya Paskal anataka kuomba funds za project zake.
Yup. Utaomba funds.Duh....!, yaani nikaombe funds kwa diaspora!.
Kwa taarifa yako nafanya kwa kujitolea, sijaomba funds kwa yeyote!. Angalia tarehe ya bandiko hili Wana Diaspora, naomba ushirikiano wenu; tukutane, tujadili Tanzania ikusaidieje ili uisaidie nchi yako?
P
Nitaomba funds za nini?.Yup. Utaomba funds.
Unaweza usiwe mgeni, lakiniPaskal mimi siyo mgeni humu ndani.
Updates for deals uncleNilishajiondokea Tanzania imekuwa muda kidogo Sasa, nilipata kazi Czech Republic. I'm now enjoying my life to the fullest na sipo interested kurudi home kabisa. I'm now experiencing the difference
Kauli yangu itatimia.Unaweza usiwe mgeni, lakini
Ukawa hujui kuwa kauli huumba!. "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia
P
Unataka nikupe strategy ya kuomba funds?Nitaomba funds za nini?.
P
Kwanza hongera, pili lengo la maisha ni kuyapatia na kuyawezea, maisha popote.Nilishajiondokea Tanzania imekuwa muda kidogo Sasa, nilipata kazi Czech Republic. I'm now enjoying my life to the fullest na sipo interested kurudi home kabisa. I'm now experiencing the difference
Amen, na iwe as you wish, kwasababu, this is not my first time kutaka kufanya kitu cha kusaidia na kikapigwa chini. Angalia hapa nilishauri nini jf, Vipindi Maalum vya JF kwenye TV: Naomba Maoni Yako!Kauli yangu itatimia.
Mkuu, Nimefurahi kuona type 1 unawaheshimu pia.Kwanza hongera, pili lengo la maisha ni kuyapatia na kuyawezea, maisha popote.
Ila kuna two types of life,
1. Living for yourself, 2. Living for others.
Wale waoishi for themselves, wanajijali wao tuu na familia zao, wakifanikiwa ni wao, waki fail ni wao, hapo unaweza kuta wewe uko vizuri sana, ila ndugu zako na jamaa zako kijijini kwenu, lives in stinken object poverty, yaani umasikini
uliotopea, and yet, unajisikia raha. Hawa kupiga picha za show off ma G-Wagon na ma Tesla makes them happy.
Wengine, they live for others, wakifanikiwa, wanaita ndugu zao, jamaa na marafiki, halafu wale ambao they made it big, wanakumbuka kwao, asili yao, nchini kwao, kijijini kwao and make it a different!. Hawa kitendo cha kusaidia wengine kwao is more gratifying than kuonekana wana nini.
TAK inawatarget zaidi wale
Type 2, huku tukiwaheshimu type 1.
P