Diaspora ya Tanzania tumesikitishwa sana nchi yetu kurudi nyuma katika masuala ya demokrasia na uhuru wa kujumuika

Diaspora ya Tanzania tumesikitishwa sana nchi yetu kurudi nyuma katika masuala ya demokrasia na uhuru wa kujumuika

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Tulifikiri nchi yetu inatoka katika giza la siku zilizopita ambazo zilighubikwa na uhasama wa kisiasa na matumizi makubwa ya nguvu za dola kuwazuia wapinzani kushiriki siasa.

Tunasikitika kuona yale yaliyoichafua Tanzania ndani na nje ya mipaka yake yamerudi tena;
-utekaji
-kuzuia wanasiasa wa upinzani kufanya mikutano ya hadhara

Soma Pia: Hatma ya Demokrasia Tanzania: Madhara ya Tamisemi Kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Hatua Muhimu kwa Serikali na Upinzani

Kinachotusikitisha sana ni mambo haya yote kutokea ndani ya “ maridhiano “!

Tunamsihi Rais Samia asiruhusu taswira ya Tanzania kuchafuliwa kama ilivyokuwa katika utawala uliopita.

Kukosekana kwa usawa katika Demokrasia ya vyama vingi sio sifa nzuri kwa nchi yetu na jambo hili halina manufaa kwa Watanzania isipokuwa kwa viongozi wachache.

Tunatimaini uongozi wa nchi yetu utajirekebisha katika jambo hili.
 
Back
Top Bottom