Dick Sound: Milionea aliyeanza kuuza maji, kufunga muziki Magomeni

Kutoa rim org iliyokuja na Gari kutoka Japan/UK halafu nikaweka jiko la mchina kutoka kwa dick siwezi aisee.

Ila wamasai hapa mjini hawajawahi kuisha.
 
31-20 umepata ngapi mkuu?
 
Hivi kumiliki nyumba moja na magari ya kifahari ni utajiri? Hayo magari ya kifahari yanamuingizia sh ngapi?

Gari si ni usafiri tu au? Yaani kumiliki nyumba ya kuishi na usafiri... Basi hata mimi ni milionea, nianzishie uzi.
 
Matajiri wa bongo wote walianza kuuza maji kuuza mitumba mafundi viatu mara vuup milionea.Tunaambiwa binadamu alotokana na nyani ila mpaka leo hamna nyani aneyebadilika kuwa binadamu.
 
Uzuri dogo ana connection na watu maarufu wote unaowajua ww tanzania hii so kufanikiwa easy tuu. Kazi kubwa ya kujivunia ni kufanikiwa kujenga connection baaas
Hizi connection ndizo zinawapa michongo isiyojulikana yenye pesa ndefu nje ya kufunga muziki magari inayojulikana na wengi.
 
Labda mwanzisha uzi na jamaa wamekuwa wote tangu utotoni.
 
Dick ni mtu poa mno...anacheka na kila mtu na kuwaheshimu watu wa rika zote.

Nimemfahamu miaka mingi kidogo enzi hizo🥲anaishi na mdogo wake P maskini sinza kumekucha😀😀mie kumbe nimekula chumvi e.

Kati ya lile group Lao la watu wa geregi watatu wametoboa ikiwepo Dick mwenyewe,Radi huyu anamaduka yake ya spare za magar pale sinza kumekucha anapesa huyu masta (maisha haya aise..ukiwa na ndoto inayoishi ndani yako lazima utoboe)Magoti(smart key) nae yuko vizuri sana wote hawa wanakoneksheni ndefu mjini kupitia biashara zao.Abdul & Husein sijui wanavyoendelea.

Nimejikuta naikumbuka sinza kumekucha miaka hiyo kitambo mnooo😃😃(mie nae mhenga)😜
Nikirudi Dar nikamsalimu Dick kwakweli.
R&M ni watu wangu wa karibu mno..karibuni ofisini kwao Sinza kumekucha Kwa huduma za magari
🧚‍♀️🧚‍♀️
 
Dick hana miaka 31.
Atakuwa kabakiza miaka michache kufika 40 lkni kusema eti Kwa sasa ana 31😀😀big no
 
Dah umenikumbusha huyo jamaa Radi, mm huwa nanunua spare parts hapo kwenye duka lake nikienda kufanya service gari yangu hapo garage za Sinza, mtu poa sana anakuuzia spare na kukushauri pia ubora, uimara na utofauti wa kati ya spares zinazofanana so uchaguzi unabaki kuwa ni wako. Hata Magoti namjua ni fundi sana huyo jamaa kuna kipindi nilikuwa nikienda garage kwake nakuta hadi gar za Diamond, uzuri umeme wa magari anaujua na mechanics pia anaijua yaani gari sijui iwe na tatizo gani mpk imshinde.
 
Usisahau pia Magomeni ndio makao makuu ya wauzaji na wasafirishaji wa dawa za kulevya Tanzania.
Umeshamaliza ubishi mkuu. Huo ndio uhalisia wa Mambo.
 
Naona alijiongeza na kuanza kuuza ma rim ya kichina pale kwake.
Ile biashara yake imevamiwa na mafundi wana njaa zaidi ya fisi yaani hawaachi hela na siku hizi bidhaa za kichina zilivyoshamiri mteja anaangaliwa tu anataka mziki wa bei gani?Lumumba pale zipo mpaka radio za Sony za 60K na amplifier 90/80K so jamaa wanapiga winga tu yeye na umaarufu wake kama hajakuwa mbunifu atajikuta akirudi kwenye kuchomea circuits kwenye radio mbovu.

Ile biashara imeshakuwa kichaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…