Dickon Ambundo Is More Prolific Than P. O. Sakho

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Nimemtazama sana P.O SAKHO akicheza soka katika mazingira tofauti tofauti hapa Tanzania.

Na pia nimekuwa nikimfuatilia Ambundo tangu akiwa Gor Mahia na Dodoma FC.

Hawa ni washambuliaji wa pembeni ambao wanatofautiana pakubwa sana.

Mmoja ana sifa ya adoptability kuliko mwengine. Yaani anaweza kucheza mpira katika mazingira tofauti tofauti yawe ya mvua, manundu manundu au kwenye kapeti na akakuhakikishia ushindi.

Mwingine uwezo wake anauonyesha vyema katika kapeti zaidi.

Mwingine haogopi kumfuata adui na kumchopoka ila mwingine ana pendelea zaidi kukokota mipira diagonally pale anapokabwa.

Mwingine hatengenezi nafasi za kutosha ila akipata nafasi ana uwezo wa kuitumia kiufanisi. Ila mwingine amejaa umachachari tu.

Mwingine anapokuwa kwenye situation ya 1 v1 yuko predictable sana ndio maan ani rahisi kum-contain ila mwingine ni versatile na hivyo sio rahisi kwa walinzi kujua nini atafanya anapokiwa 1v1.

Kwa upande wangu .....Nitamchagua Ambundo na kumuweka Benchi Sakho.
 
Nimemtazama sana P.O SAKHO akicheza soka katika mazingira tofauti tofauti hapa Tanzania.

Na pia nimekuwa nikimfuatilia Ambundo tangu akiwa Gor Mahia na Dodoma FC...
Sakho anacheza sana na jukwaa tofauti yake na Morrison ni ndogo Sana, akikutana na wanaume awezi kufurukuta ataishia kupiga chenga na manjonjo ambayo ayana madhara
 
Subiri Babra fc waje kukutolea povu
[emoji23][emoji23][emoji23]hii ni vita ya Makolo vs Mautopolo ngoja sisi watazamaji tuone mtaishia wapi wafia timu za bongo
 
Sakho anacheza sana na jukwaa tofauti yake na Morrison ni ndogo Sana, akikutana na wanaume awezi kufurukuta ataishia kupiga chenga na manjonjo ambayo ayana madhara
Wenye timu yao wakikusikia mnamkosoa kipenzi chao wanayemuimba. Kwasasa wachezaji watatu wa Simba wanaopenda kucheza na jukwaa, kuna Morrison, Inonga na Sakho.
 
Sakho anacheza sana na jukwaa tofauti yake na Morrison ni ndogo Sana, akikutana na wanaume awezi kufurukuta ataishia kupiga chenga na manjonjo ambayo ayana madhara
Asante kwa kuliona hili.
 
Mpira wa bongo hua ni wa ajabu sana. Wakishakujua staili yako ya uchezaji kwisha habari yako. Huyo sakho anapenda vyenga na makeke ya kunyonga baiskeli. Hapo beki visiki hawakuachi salama.

Ligi kuu hana anachokifanya. Mfano mwingine ni Morrison mzee wa vyenga na ujanja maandazi wa kuanzisha mipira haraka. Niambie kama siku za hivi karibuni tangu janja yake igundulike amefanya nn. Labda amewaokota tu red arrows lkn baada ya kumjua kwisha habari yake.
 
Nakuona Mwakalebela unautani na Thimba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…