Dida aonyesha jeuri nyingine ya pesa

Dida aonyesha jeuri nyingine ya pesa

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Prizenta wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kinachorushwa na Radio Times FM , Hadija Shaibu ' Dida' ameonesha jeuri nyingine ya fedha baada ya kununua magari mengine mawili kwa mpigo .

Dida amefanya kufuru hiyo ikiwa imepita miezi kadhaa tangu atangaze kuwa ana nyumba mbili maeneo ya Goba na Kigamboni pamoja na kuyaanika magari manne anayomiliki ( Toyota Verossa mbili, Toyota Noah nyeusi na Toyota Vitz .)

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, rafiki wa karibu wa Dida aliyeomba hifadhi ya jina alisema ameshtushwa na kitendo cha shosti wake huyo kununua magari mawili kwa mpigo kiasi cha kumfanya ahisi kuna biashara nyingine anaifanya tofauti na utangazaji .

"Kanunua magari mawili , Toyota Noah na Toyota Brevis New Model. Yaani hata sisi mashosti zake anatufanya tuhisi labda anafanya ile biashara ya unga kama watu wanavyohisi.

"Ni kweli anafanya biashara zake lakini ndiyo apate fedha za kuonesha jeuri hiyo ? Ila kama ni kupambana na maisha , sasa hivi anapambana kikwelikweli, hata akijiita Boss Lady ni sahihi kabisa ," alisema mtoa habari huyo.

Baada ya kupata taarifa hizo , mwandishi wetu alimtafuta Dida ili kujua ukweli wa magari hayo , alipopatikana alifunguka : "Siwezi kujiita Boss Lady kimdomomdomo tu , huwa napenda kufanya kitu watu ndiyo waseme, nimeongeza magari mengine mawili . Moja ni Noah kwa ajili ya biashara zangu na lingine ni Toyota Brevis la kutembelea, " alisema Dida aliyetengana na mumewe, Ezden Jumanne siku chache zilizopita.


Chanzo: GlobalPublishers
 
Na yeye edzen c akamshtak dida wagawane mali wote pasu kwa pasu , aende ustawi wa jamii pale ,haki sawa kwa wote

Maybe anaona aibu sababu alizikuta hizo mali ndio maana ameziacha jinsi alivyozikuta
 
Samahani extreme pack wewe ni binamu yetu Warumi? Tumekumiss kiama

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Nilidhani Deogratius Munishi (Dida) goal keeper wa Yanga, kumbe huyu, huyu tumemzoea.
 
Binamu nimekumis

Halafu si nasikia huyo dida anachepuka na raheem wa times fm? Yani hili sugar mom linayaweza

nipo sana ila siji sana binamu mbea mwenzetu wamemfungia
tobaaa!!!dida anataka kuolewa tena nin....????
 
Wapi maphotoo

Hakuna kukalia uchumi.. lazima utumike ipasavyo
 
Na umbea umerudi kiama hahaha,

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Binamu nilikumis kiama, nkasema apa nikisubir mpaka iishe hakyanan ningekufa binamu, maana nina mchele wa haja nkasema hataa ngoja nirudi kwenye kiti changu
 
Na umbea umerudi kiama hahaha,

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Naona kajikoki kwa umbea kama kifurushi cha extreme pack.Umeona jukwaa limeng'aa kidogo baada ya kurudi mmbea aliyetukuka na asiyekuwa na mpinzani kwenye nyanja ya umbea kwa ukanda huu wa Afrika mashariki na kati.
 
Binamu nilikumis kiama, nkasema apa nikisubir mpaka iishe hakyanan ningekufa binamu, maana nina mchele wa haja nkasema hataa ngoja nirudi kwenye kiti changu

Hahaha welcome back cousin. Me nikasema au wamemgomea bina kufungua account mpya, nikaju utakuwa umelazwa kwa kukosa ubuyu wa jf

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom