Dida Shaibu aonesha jeuri ya pesa

Dida Shaibu aonesha jeuri ya pesa

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Huu ndo mjengo na baadhi ya magari anayomiliki mtangazaji wa times FM , Dida Shaibu...

================================
================================

Monday, August 4, 2014
DIDA WA TIMES FM AONESHA JEURI NYINGINE YA PESA


Hadija Shaibu ‘Dida’ akiikagua gari yake.
Zimemtembelea! Prizenta wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kinachorushwa na Radio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’ ameonesha jeuri nyingine ya fedha baada ya kununua magari mengine mawili kwa mpigo.Dida amefanya kufuru hiyo ikiwa imepita miezi kadhaa tangu atangaze kuwa ana nyumba mbili maeneo ya Goba na Kigamboni pamoja na kuyaanika magari manne anayomiliki (Toyota Verossa mbili, Toyota Noah nyeusi na Toyota Vitz.)

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, rafiki wa karibu wa Dida aliyeomba hifadhi ya jina alisema ameshtushwa na kitendo cha shosti wake huyo kununua magari mawili kwa mpigo kiasi cha kumfanya ahisi kuna biashara nyingine anaifanya tofauti na utangazaji.

IMG20140731WA0009.jpg

Prizenta wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani, Hadija Shaibu ‘Dida’ akipozi kwenye gari yake mpya.

“Kanunua magari mawili, Toyota Noah na Toyota Brevis New Model. Yaani hata sisi mashosti zake anatufanya tuhisi labda anafanya ile biashara ya unga kama watu wanavyohisi.

“Ni kweli anafanya biashara zake lakini ndiyo apate fedha za kuonesha jeuri hiyo? Ila kama ni kupambana na maisha, sasa hivi anapambana kikwelikweli, hata akijiita Boss Lady ni sahihi kabisa,” alisema mtoa habari huyo.

IMG20140731WA0002.jpg

Gari jingine la ‘Dida’ aina ya Toyota Noah.
Baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Dida ili kujua ukweli wa magari hayo, alipopatikana alifunguka:

“Siwezi kujiita Boss Lady kimdomomdomo tu, huwa napenda kufanya kitu watu ndiyo waseme, nimeongeza magari mengine mawili. Moja ni Noah kwa ajili ya biashara zangu na lingine ni Toyota Brevis la kutembelea,” alisema Dida aliyetengana na mumewe, Ezden Jumanne siku chache zilizopita.


Chanzo: DJSek Blog
 

Attachments

  • 1394459549689.jpg
    1394459549689.jpg
    68.2 KB · Views: 2,209
  • 1394459578274.jpg
    1394459578274.jpg
    30.1 KB · Views: 1,724
  • 1394459593896.jpg
    1394459593896.jpg
    35.7 KB · Views: 1,824
  • 1394459609760.jpg
    1394459609760.jpg
    54.7 KB · Views: 1,632
Mh! Nje na utangazaji anafanya ujasiriamali upi mwingine?
 
Kwapesa gani ingekuwa hivyo watangazaji wote wa times wangekuwa matajiri na kila mtu angekimbilia times fm, yeye na Ezden wote watangazaji tu.
 
Ivi nynyi mnaamini ilo gazeti la udaku aaaaahaaaaaa kazi kweli kweli uyo anapanga mwananyamala hana hata nyumba naiyo range alipiga nayo picha tu akiwa huko china..izo tetesi za sembe zipo mda tu sasa sijui kama kunaukweli au vipi lakini yanamwisho hayo siku yake haijafika tu kama nikweli anafanyaizomambo atadakwa tu
 
Inawezekana ni vyake Dida namjua ni mjasiriamali uwa anaenda china kufata mzigo na nyie muende china trip moja tu inabadilisha maisha yako

Ingekuwa kwenda China trip moja kuwa hivyo kila mtu si angeenda, nazani wale punda wangeacha biashara ya kubeba sembe na hata huyo aliyekamatwa angeenda trip 3 tu si angekuwa bilionea.
 
Izo ni ofisi za timesfm watanzania mnanini nyinyi aaaaahaaaaa ana gari moja tu verosa kweli shigongo anajua kuchota akili za watu ..i knw here anapanga mwananyamala hana zaidi
 
Back
Top Bottom