Didier Drogba ashindwa Urais wa Shirikisho la Soka la Ivory Coast

Didier Drogba ashindwa Urais wa Shirikisho la Soka la Ivory Coast

Mshambulizi wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba, aliangushwa katika raundi ya kwanza ya upigaji kura wa Urais wa Shirikisho la Soka la nchini Ivory Coast ( FIF) kwa kupata kura 21 huku mahasimu wake Diallo (kura 59) na Diabaté (kura 50)

Katika raundi ya pili, Idriss Diallo, mfanyabiashara na mjumbe mkuu wa sasa wa FIF, aliibuka mshindi kwa kumuondoa aliyekuwa makamu wa Rais wa FIF Sory Diabaté kwa kura 63 dhidi ya 61

Uchaguzi wa Jumamosi katika mji mkuu wa kisiasa wa Yamoussoukro uliahirishwa mara kadhaa tangu 2020, hasa kutokana na masuala ya kuhusu kustahiki kwa baadhi ya wagombea, huku Drogba akiwa miongoni mwao.

Chanzo: BBC
Uamaarufu pekee hausaidii kushinda chaguzi.....

Chaguzi ni MIPANGO IMARA ...ya muda mfupi na mrefu.....
 
Mtu kakulia Ulaya uko muda wenyewe wa kuishi nchini kwake sio mwingi mara nyingi yuko nje kwenye mishe zake. Mpira ndio hivyo hana mwamko nao, hana mahusiano na wadau wa soka sasa ataongoza na nani kama sio migogoro tu, wadhamini alikosa maana wadau wa soka wanajua hamna kitu. Then wabongo wanataka awe rais kisa alikuwa mchezaji mzuri
Umenena 👍
 
Wajumbe sio watu wazuri, kwa hakika kabisa bwana Drogba alilwa pesa na wajumbe na kura hawakumpa
 
Aingie kwenye siasa. Urais wa nchi ataweza kufanikiwa.
 
Kuongoza mpira sio kwa sababu ya asante. Kujenga hospitali na kununua CT scanners ndio kunaleta uwezo wa kuongoza mpira? Kwani walikubaliana ajenge hospitali ili apewe urais, hiyo rushwa italipwa kwa njia gani. Waafrika tuna matatizo sana, kwahiyo kule Marekani kina John Hopkins walitakiwa wagombee urais
Hoja ya huyo member NI kituko. Watanzania tumelogwa au maana sio Kwa ufinyu wa fikra kiasi hiki.
 
Jamaa nasikia kipindi anacheza ulaya hata kurudi kwao ilikuwa harudi labda kuwe na mechi za kimataifa halafu alivyostaafu hata uwanjani alikuwa haingii kuangalia team ya taifa halafu karudi anataka uraisi.
 
Kafanyiwa figisu Mbaya sana na mfanyabiashara tajiri mbaya aliyekua anagombania naye. Usicheze na matajiri wa ndani kwenye chaguzi za ndani Afrika
 
Kama hakuwapa pesa wajumbe asilaumu mtu, Africa bahasha ya kaki ndio kila kitu.

Muulize KIRIA na yule aliyetiwa ndani na Jiwe mpaka sasa hana hamu tena ya soka ; eehehe anaitwa Jamal Malinizi!!
 
Baada ya kuwajengea hospitali ya rufaa na kuwanunulia ma CT scanners na MRI scanners hii ndiyo asante wanauompa.

Anajipanga kupata Urais huu ili baadae agombee Urais wa nchi. Kuikosa hii nafasi ni pigo kubwa kwake.
Hivi wewe ni individual au taasisi?
 
Back
Top Bottom