Didier Drogba ashindwa Urais wa Shirikisho la Soka la Ivory Coast

Uamaarufu pekee hausaidii kushinda chaguzi.....

Chaguzi ni MIPANGO IMARA ...ya muda mfupi na mrefu.....
 
Umenena πŸ‘
 
Wajumbe sio watu wazuri, kwa hakika kabisa bwana Drogba alilwa pesa na wajumbe na kura hawakumpa
 
Aingie kwenye siasa. Urais wa nchi ataweza kufanikiwa.
 
Hoja ya huyo member NI kituko. Watanzania tumelogwa au maana sio Kwa ufinyu wa fikra kiasi hiki.
 
Jamaa nasikia kipindi anacheza ulaya hata kurudi kwao ilikuwa harudi labda kuwe na mechi za kimataifa halafu alivyostaafu hata uwanjani alikuwa haingii kuangalia team ya taifa halafu karudi anataka uraisi.
 
Kafanyiwa figisu Mbaya sana na mfanyabiashara tajiri mbaya aliyekua anagombania naye. Usicheze na matajiri wa ndani kwenye chaguzi za ndani Afrika
 
Kama hakuwapa pesa wajumbe asilaumu mtu, Africa bahasha ya kaki ndio kila kitu.

Muulize KIRIA na yule aliyetiwa ndani na Jiwe mpaka sasa hana hamu tena ya soka ; eehehe anaitwa Jamal Malinizi!!
 
Baada ya kuwajengea hospitali ya rufaa na kuwanunulia ma CT scanners na MRI scanners hii ndiyo asante wanauompa.

Anajipanga kupata Urais huu ili baadae agombee Urais wa nchi. Kuikosa hii nafasi ni pigo kubwa kwake.
Hivi wewe ni individual au taasisi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…