TANZIA Diego Maradona afariki dunia

TANZIA Diego Maradona afariki dunia

Mwamba wa Soka umeanguka safari njema isiyo na bugudha Diego A. Maradona, upumzike kwa raha na Amani
 
Goodbye Diego.. [emoji1480]
images%20(21).jpg
 
Nilikuwa natizama video clip zake YouTube ...Tuacheni masihara huyu marehemu alikuwa anauchezea mpira Kama vile mlafi anavyochezea tonge la ugali ... Ukimtazama akiwa anacheza ndani yake unamuona Messi na ronaldinho hawa jamaa kuna style nyingi mnooo za uchezaji wameiga kwa maradona nyingi sana...

Zamani nilikuwaga nadhania kwamba ile style ya kuupanda mpira nakuzunguka Ni ya zidane lakini baada ya kuangaliwa clip za maradona niliishia kupigwa na butwaa mambo yanayo fanywa na wachezaji wengi wa siku hizi kuanzia skills dribling upigaji faulo Kasi ya ukiambiaji control maradona Alisha zifanya kitambo ... Itoshe tu kusema kwamba maradona alikuwa anaishi mbele ya muda
 
Wachezaji wote wamerithi kwa huyu mwamba, japo wengi wao wameshindwa. May be Messi ndio ameweza.
 
Kweli kila kitu ..ukimtazama unamuona Messi na ronaldinho binafsi nilikuwa namkubali Sana messi lakini baada ya kuona zile clip za maradona nashawishika kusema kwamba hakuna wakufikia level yake
 
Mwamba hatunaye tena.

Alikuwa na miaka 60.

Masikitiko makubwa.

Rais wa Argentina katangaza siku 3 za maombolezo.

-----
Wasifu Wa Hayati Maradona
-----
Mmoja wa wachezaji waliobarikiwa, Argentina ilijivunia kipaji cha kipekee, madoido ya ajabu akiwa uwanjani, maono na kasi vilivyovutia mashabiki wengi.
Lakini pia alisababisha hasira na goli lake alilolipa jina 'Hand of God' ambalo lilizua utata pamoja na kutumbukia katika utumiaji wa dawa za kulevya na mapungufu mengine yaliyojitokeza baada ya kustaafu soka.

Mfupi lakini imara - Nyota wa kandanda​

Alizaliwa miaka 60 iliyopita huko Buenos Aires eneo la kitongoji duni, Diego Armando Maradona aliepuka umaskini wakati akiwa kijana kwa kuwa nyota wa mpira wa soka ambaye kuna wale wanaomchukulia kuwa bora zaidi akilinganishwa na mchezaji Pele wa Brazil.
Mchezaji huyo wa Argentina, aliyefunga magoli 259 katika mechi 491 alizoshiriki alimshinda mpinzani wake wa Marekani Kusini katika kura ya maoni ya kuamua mchezaji wa karne ya 20 kabla ya Fifa kubadilisha sheria za upigaji kura na wote wawili wakatunukiwa hadhi hiyo.

Maradona alionesha uwezo wa hali ya juu kutoka akiwa mtoto na kuwa chanzo cha timu ya vijana ya Los Cebollitas kuwa kidedea kwa kupata magoli 136 bila kufungwa na timu yoyote kando na kujitokeza kwake kama mchezaji wa kimataifa akiwa na umri wa miaka 16 pekee na siku 120.

Akiwa mfupi na imara, futi 5 na inchi 5 pekee, uchezaji wake haukuwa wa kawaida. Lakini ujuzi wake, wepesi, maono, jinsi alivyodhibiti mpira, alivyopiga chenga na kupitisha mpira kwa wengine kwasababu ya kukosa kasi na wakati mwingine hata kuwa na matatizo ya uzito wa kupita kiasi.

Huenda alikuwa na kasi ya ajabu mno akiwa uwanjani karibu na mahasimu wake lakini alikuwa na wakati mgumu kukwepa changamoto.

Goli maarufu la 'Hand of God' na 'Goli la Karne'​

Maradon alimfunga kipa wa England kwa kufunga na mkono na goli hilo lilikubalika mwaka 1986

Maradona alifunga magoli 34 kwa kushiriki mechi 91 kama mchezaji wa Argentina na
Yeye ndio chanzo cha nchi yake kuibuka na ushindi katika kombe la dunia mwaka 1986 nchini Mexico na kupata fursa kuingia fainali miaka minne baadaye.

Katika robo fainali ya mchezo wa awali kulijitokeza utata ambao kumbe baadaye ungekumba maisha yake. Mechi dhidi ya England ilikuwa na mkwaruzano uliopitiliza kidogo huku vita vya Falklands kati nchi hizo mbili vikiwa ndio vimetokeo miaka minne tu nyuma. Na kumbe hilo lingesababisha hali uwanjani kuzua wasiwasi zaidi.

Dakika 51zikiwa zimekatika na hakuna timu iliyoona lango la mwingine, Maradona aliruka na mlinda lango wa timu pinzani Peter Shilton na kufunga kwa kupiga mpira hadi kwenye neti.

Baadaye alisema goli hilo lilitokana na "Maradona kuupiga mpira kwa kichwa kidogo na mkono wa Mungu". Dakika nne baadaye, alifunga kile kimekuwa kikitambuliwa kama 'goli bora la karne' - baada ya kuchukua mpira mwenyewe na kuanza mbio kwa kasi ya ajabu ambako kuliacha wachezaji kadhaa wakimfuata nyuma kabla ya kumzunguka Shilton na kufunga bao.

Maradona alikuwa mchezaji nyota katika klabu ya Napoli ambapo alifunga magoli 81 katika mechi 188

"Lazima tu ungesema ulikuwa mchezo mzuri. Hakuna shaka yoyote na goli hilo. Kulikuwa tu na mchezaji nyota wa mpira wa soka," alisema mchambuzi wa BBC Barry Davies.

England ilikuwa nyuma kwa bao moja lakini Argentina ikafaulu na Maradona akasema "ilikuwa zaidi ya kushinda mechi, ilikuwa ni suala na kuwatoa nje Waingereza".

Shujaa kwa Napoli lakini akatumbukia katika matumizi ya dawa za kulevya
Maradona alivunja rekodi ya uhamisho mara mbili - akiondoka timu ya vijana ya Boca Juniors mji wake wa nyumbani na kujiunga na timu ya Barcelona, Uhispani kwa kima cha pauni milioni 3 mwaka 1982 na kujiunga na klabu ya Italia ya Napoli miaka miwili baadaye kwa kima cha pauni milioni 5.

Waliomlaki walikuwa ni mashabiki zaidi ya mashabiki 80,000 waliomsubiri uwanja wa Stadio San Paolo alipowasili kwa helikopta. Shujaa mpya.

Alichezea klabu bora katika taaluma yake nchini Italia akishangiliwa na wafuasi wake wakati huo akiwa kichocheo cha kupata mataji ya kwanza ya Ligi mwaka 1987 na 1990 na pia katika kombe la Uefa mwaka 1989.

Sherehe ya kufurahia ushindi wa kwanza ilidumu kwa siku tano huku mamia ya maelfu ya watu wakijitokeza lakini Maradona alionekana kuchoshwa na sherehe hizo.

"Huu ni mji mzuri lakini napata shida, hata siwezi kupumua kwa amani. Nataka kuwa huru na kutembea. Mimi ni kijana kama mwingine yeyote yule," alisema.

Hata hivyo hakuwezi kujitenga na sakata ya uhalifu ya Camorra, akatumbukia katika utumiaji wa dawa za kulevya na kufunguliwa kesi mahakamani ya kutafuta atambuliwe rasmi kama baba.

Baada ya kushindwa bao 1-0 na Ujerumani mwaka wake wa mwisho Italia 90, alipatikana na kashfa ya utumiaji wa dawa zilizopigwa marufuku mwaka uliofuata na kupigwa marafuku kucheza soka kwa miezi 15.

Hata hivyo, alirejea tena kwenye ulimwengu wa soka katika Kombe la Dunia la mwaka 1994 nchni Marekani.

Lakini pia alifanya watazamaji kuwa na wasiwasi jinsi alivyosherehekea goli akiwa kama kichaa mbele ya kamera na kutolewa nje katikati ya mechi baada ya kubainika kuwa ametumia dawa iliyopigwa marufuku ya ephedrine.

Matukio ya Maradona​

  • 1977: Alijitokeza katika mchuano kati ya Argentina v Hungary
  • 1982: Alijiunga na Napoli baada ya kuwa Barcelona kwa miaka miwili ya mafanikio makubwa
  • 1986: Alishinda Kombe la Dunia akichezea Argentina
  • 1990: Alikuwa mshindi wa pili wa Kombe la Dunia akichezea Argentina. Kombe la pili la Ligi Napoli
  • 1991: Alipigwa marufuku ya miezi 15 baada ya kuthibitishwa kutumia dawa zilizopigwa marufuku
  • 1994: Alicheza katika kombe la dunia kwa mara ya nne lakini akatolewa nje baada ya kuthibitishwa kutumia dawa zilizopigwa marufuku
  • 1997: Alistaafu kucheza soka baada ya kuthibitishwa kutumia dawa zilizopigwa marufuku kwa mara ya tatu
  • 2010: Alikamilisha miaka miwili ya kuwa kocha wa Argentina baada ya kutolewa katika robo fainali ya Kombe la Dunia

Maisha baada ya kustaafu​

Baada ya kupatikana tena ametumia dawa zilizopigwa marufuku, miaka mitatu baadaye alistaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 37 lakini akaendelea kuandamwa na matatizo.

Maradona alihukumiwa kifungo cha miaka miwili na miezi 10 kilichocheleweshwa kwasababu ya kufyatulia risasi wanahabari hewani .
Tabia yake ya kutumia dawa za kulevya na pombe ilimsababishia matatizo mengi ya kiafya. Aliongeza uzito na kuna wakati fulani alikuwa na kilogramu 128. Mwaka 2004 akapata mshtuko wa moyo uliosababisha apelekwe katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Pia alifanyiwa upasuaji wa kupunguza tumbo lake kumsadia kukabiliana na tatizo la uzito wa kupindukia na kutafuta hifadhi Cuba wakati anakabiliana na utumiaji wa dawa za kulevya.

BBC Swahili

Dah, shujaa mwenye mpira wake katutoka...huyu mwamba aliufanya mpira uonekane mwepesi sana, aliufanya anavyotaka na ulikuwa unamtii, kiukweli alileta burudani haswaa ambayo kwangu mimi sijaona mchezaji yeyote alieweza kufanya maajabu hayo, hadi Messi alipoletwa duniani akatuburudisha kwa mara nyingine

Wachezaji wangu bora wa muda wote,

Messi✔
Maradona✔
 
Unashoboka kinoma hadi unatamani ungekua mke wao.
 
🙏
 
Back
Top Bottom