TANZIA Diego Maradona afariki dunia

Mwamba wa Soka umeanguka safari njema isiyo na bugudha Diego A. Maradona, upumzike kwa raha na Amani
 
Nilikuwa natizama video clip zake YouTube ...Tuacheni masihara huyu marehemu alikuwa anauchezea mpira Kama vile mlafi anavyochezea tonge la ugali ... Ukimtazama akiwa anacheza ndani yake unamuona Messi na ronaldinho hawa jamaa kuna style nyingi mnooo za uchezaji wameiga kwa maradona nyingi sana...

Zamani nilikuwaga nadhania kwamba ile style ya kuupanda mpira nakuzunguka Ni ya zidane lakini baada ya kuangaliwa clip za maradona niliishia kupigwa na butwaa mambo yanayo fanywa na wachezaji wengi wa siku hizi kuanzia skills dribling upigaji faulo Kasi ya ukiambiaji control maradona Alisha zifanya kitambo ... Itoshe tu kusema kwamba maradona alikuwa anaishi mbele ya muda
 


Wachezaji wote wamerithi kwa huyu mwamba, japo wengi wao wameshindwa. May be Messi ndio ameweza.
 
Wachezaji wote wamerithi kwa huyu mwamba, japo wengi wao wameshindwa. May be Messi ndio ameweza.
Kweli kila kitu ..ukimtazama unamuona Messi na ronaldinho binafsi nilikuwa namkubali Sana messi lakini baada ya kuona zile clip za maradona nashawishika kusema kwamba hakuna wakufikia level yake
 

Dah, shujaa mwenye mpira wake katutoka...huyu mwamba aliufanya mpira uonekane mwepesi sana, aliufanya anavyotaka na ulikuwa unamtii, kiukweli alileta burudani haswaa ambayo kwangu mimi sijaona mchezaji yeyote alieweza kufanya maajabu hayo, hadi Messi alipoletwa duniani akatuburudisha kwa mara nyingine

Wachezaji wangu bora wa muda wote,

Messi✔
Maradona✔
 
Unashoboka kinoma hadi unatamani ungekua mke wao.
 
🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…