Differences between Kalenjin, Luo,Kisii and Kikuyu men

Differences between Kalenjin, Luo,Kisii and Kikuyu men

Hilo la mila kwetu zinafanyika sana. Kuanzia Kusini mpaka Kaskazini, Mashariki mpaka Magharibi, hapo Dar tu kuna Kijiji cha Makumbusho, makabila huwa na mikutano yao ya kukumbushana jadi zao. Kila sherehe ya harusi kuna nyimbo za jadi, tunataniana pia.

Huu utamaduni wa kutaniana baina ya makabila ni jambo kubwa pengine kuliko Nchi yeyote ya Afrika, na tafsiri ya kutaniana maana yake Mtu kabila A anajua mila na desturi zake na za kabila B. Huwezi kuwaita hawa Watu wamepoteza utambulisho wao. Pengine ukiona Watu wanachapa Kiswahili ukadhani wamepoteza uasili wao lakini kama Taifa tunajali pia Utaifa wetu kww sababu kwa picha kubwa kwa idadi ya Watu 40+ lazima ku-sacrifice sehemu ya ubinafsi wetu ili tuishi vyema kwa Ustawi wetu na Watoto wetu.

Umezungumzia habari ya 'kukutana bila kuvunja sheria', najua hapa una uelewa mdogo. Sheria si kila kitu kwenye maisha, kuna kanuni za maisha kama Taifa ambazo hazijaandikwa popote. Kama Watu hawatangamani vizuri sheria haina maana kabisa.

Hapa tunazungumzia Taifa. Taifa ambalo Mkikuyu anajiuliza kama anaweza kwenda kuishi Homabay au Siaya and Luo vice versa. Au Mkalenjini kwenda kuishi Ukikuyuni bila kujishuku.

Na hapa si kwamba hakuna fursa ya maisha, ni kwa sababu anahofu kama ataishi kwa utangamano na wenyeji wake akiwa pekee au na familia yake! Sasa hilo si Taifa kwa maana yake

Sent using Jamii Forums mobile app

Unavyochanganya tuhuma zako dhidi ya Kenya na kuhamisha goli hadi sielewi ni haswa shida, simamia kimoja ili tutiririke na kuwekana sawa.
Kenya haina sera wala sheria inayomkataza Mkenya kuishi popote, tupo na watu waliohamia makazi yanayoishi makabila mengine na wameishi pamoja kama jamii kwa miaka ming tu.
Sio kwamba nakana hakuna ukabila huku, upo tu lakini sio kwa jinsi huwa mumeaminishwa kwamba eti tunaishi kwa kukatana mapanga kila uchao, matatizo ya ukabila huku husababishwa na wanasiasa kipindi cha uchaguzi, wanasababisha chuki kwa kuwalipa vijana kuwavuruga baadhi ya wanaoishi ndani ya makabila mengine. Maana tu baada ya uchaguzi, hizo vurugu huisha na watu wanatengamana bila matatizo yoyote.

Mwanasiasa huwa na undugu na shetani, anaweza kusababisha chochote ilmradi ashinde uchaguzi, kwa mfano huko kwenu kipindi cha uchaguzi albino huchinjwa sana, mwaka huu tumeona visa vya watoto kuchinjwa na kunyofolewa viuongo, haya ni matukio ya kawaida kwenu mnapokaribia uchaguzi. Ndio hivyo na huku, kipindi cha uchaguzi kuna baadi ya wanasiasa hutumia chochote ili ashinde tu.

Unyanyasaji wa kikabila sio pale watu wa asili moja wanakusanyika na kuongea yao kwa kutumia lugha yao, bali ni pale mnatumia kabila kuchuja baadhi ya watu. Kwa mfano uteuzi serikalini au kwenye nafasi zozote za ajira, hilo ni tatizo huwa linatukumba mara moja moja na ndio maana nikasema sio kwamba nakana hatuna matatizo ya ukabila, japo sio kwa jinsi huwa mnaimba, japo pia tunawazidi kwa hilo tatizo, maana na kwenu lipo pia ila kima kimya, kwa mfano nilisoma sehemu jinsi utawala wa leo ulivyojaa Wasukuma kwenye kila nyadhifa tofauti serikalini, wengi wanaamini hiyo imesababishwa na ukanda maana rais ametokea huko kwa jirani na Wasukuma na mara nyingi hupenda kujihusisha na Usukuma.
 
Ukabila hautakwisha Kenya hata nikijifunza inshomire (nimesoma) kwa Kihaya. Usifananishe Tz na Kenya kabisaa. Acha mara moja.
Ukabila wa Kenya nafuu ukilinganisha na ukabila Tanzania ,wanaccm vs watanzania.The country is deeply polarized- kwa hili magu amefanikiwa mia kwa mia.
 
Unavyochanganya tuhuma zako dhidi ya Kenya na kuhamisha goli hadi sielewi ni haswa shida, simamia kimoja ili tutiririke na kuwekana sawa.
Kenya haina sera wala sheria inayomkataza Mkenya kuishi popote, tupo na watu waliohamia makazi yanayoishi makabila mengine na wameishi pamoja kama jamii kwa miaka ming tu.
Sio kwamba nakana hakuna ukabila huku, upo tu lakini sio kwa jinsi huwa mumeaminishwa kwamba eti tunaishi kwa kukatana mapanga kila uchao, matatizo ya ukabila huku husababishwa na wanasiasa kipindi cha uchaguzi, wanasababisha chuki kwa kuwalipa vijana kuwavuruga baadhi ya wanaoishi ndani ya makabila mengine. Maana tu baada ya uchaguzi, hizo vurugu huisha na watu wanatengamana bila matatizo yoyote.

Mwanasiasa huwa na undugu na shetani, anaweza kusababisha chochote ilmradi ashinde uchaguzi, kwa mfano huko kwenu kipindi cha uchaguzi albino huchinjwa sana, mwaka huu tumeona visa vya watoto kuchinjwa na kunyofolewa viuongo, haya ni matukio ya kawaida kwenu mnapokaribia uchaguzi. Ndio hivyo na huku, kipindi cha uchaguzi kuna baadi ya wanasiasa hutumia chochote ili ashinde tu.

Unyanyasaji wa kikabila sio pale watu wa asili moja wanakusanyika na kuongea yao kwa kutumia lugha yao, bali ni pale mnatumia kabila kuchuja baadhi ya watu. Kwa mfano uteuzi serikalini au kwenye nafasi zozote za ajira, hilo ni tatizo huwa linatukumba mara moja moja na ndio maana nikasema sio kwamba nakana hatuna matatizo ya ukabila, japo sio kwa jinsi huwa mnaimba, japo pia tunawazidi kwa hilo tatizo, maana na kwenu lipo pia ila kima kimya, kwa mfano nilisoma sehemu jinsi utawala wa leo ulivyojaa Wasukuma kwenye kila nyadhifa tofauti serikalini, wengi wanaamini hiyo imesababishwa na ukanda maana rais ametokea huko kwa jirani na Wasukuma na mara nyingi hupenda kujihusisha na Usukuma.

Huwa sihamishi magoli. Hoja zangu huwa mtawalia, siandiki nisichokijua.

Unafurahisha kweli unaposema matatizo ya ukabila yanasababishwa na Wanasiasa kipindi cha uchaguzi! A mere execuse, Wanasiasa tayari wanajua kuna mbegu ya ubaguzi wa Kikabila ndiyo maana wanatumia kuchochea migawanyiko zaidi japo pia walishiriki pakubwa kuipanda na wanajua mmeshanogewa.

Kwamba baada ya uchaguzi huwa mnatengamana hapo hujazungumza ukweli wote ni kwamba moto huwa upo mioyoni chini kwa chini, ndiyo maana nikakupa mfano wa kama Mkikuyu anaweza kuishi Siaya au Homabay kwa amani hata kama si uchaguzi. Hili la kwamba hakuna sheria wala sera ya kubaguana nimeshakueleza ni kichaka cha kujificha tu. Utangamano hauletwi na sera wala sheria.

Kwamba Wasukuma wapo kila nyadhifa Serikalini ni uongo tu, angalia demographic sidhani kama utashangaa kukuta Wasukuma katika baadhi ya nyadhifa, hayo mambo huzungumzwa na Wapinzani wa Rais aliyepo madarakani. Kila mpinzani wa aliyepo madarakani huwa na kasumba ya kutazama jambo lolote kutengeneza udhaifu lakini mwisho wa siku hakuna ukabila kama tatizo.

Ingekuwa kuna ukabila kama unavyouweka kwa idadi kubwa ya Wasukuma Tanzania pengine kungekuwa na tatizo kubwa sana.

Mkubali ukabila Kenya ni tatizo kubwa sana. Na ndiyo maana mnawapenda sana hao Wanasiasa wanaopenda hizo 'blocks' za Kikabila!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom