Dilemma,PLEASE HELP!!!!

Dilemma,PLEASE HELP!!!!

YETOOO

Member
Joined
Nov 25, 2011
Posts
83
Reaction score
37
Mimi nilifanya interview kadhaa kwenye makampuni mbalimbali na kila interview nilikua nawauliza kama wana utaratibu wa kutoa majibu kwa waliofanikiwa na wasiofanikiwa.Sasa kama nikijibiwa kuwa tutakujibu baada ya wiki mbili iwe umepata au hujapata ikipita wiki mbili sijasikia kutoka kwao nimekua na tabia ya kuwapigia simu kuwauliza vipi?Je ni vibaya kuulizia majibu ya interview?maana kuna interview tips nilisoma wanasema dont chase the job wait if you are successful you will be contacted.Naomba na maoni yenu pia wadau ili isije ikawa kiherehere changu cha kuulizia kinanikosesha kazi.
Ahsanteni
 
Confidence makes perfect, kutouliza ni utamaduni tu wa watu waliojiwekea, binafsi nilishafanyiwa usaili na wazungu na baada ya mda fulani niliuliza kinachoendelea nikajibiwa vizuri tu na niko kazini. Mkuu ujue kuwa kuuliza sio kwamba ndio utaitwa, itategemea kama umekidhi vigezo vyao. Na pia unaweza kuitwa hata baada ya hizo wiki mbili, inategemea umewavutia kivipi.
 
Mkuu nashukuru kwa mchango wako,hivyo nitaendelea kuuliza kama kawaida maana binafsi napenda kujua mchakato umefikia wapi,walionichanganya ni hao radar recruitments na interview tip yao ya do not chase the job,WAIT.

Confidence makes perfect, kutouliza ni utamaduni tu wa watu waliojiwekea, binafsi nilishafanyiwa usaili na wazungu na baada ya mda fulani niliuliza kinachoendelea nikajibiwa vizuri tu na niko kazini. Mkuu ujue kuwa kuuliza sio kwamba ndio utaitwa, itategemea kama umekidhi vigezo vyao. Na pia unaweza kuitwa hata baada ya hizo wiki mbili, inategemea umewavutia kivipi.
 
[SUP]Ni vema ukawajua waliokufanyia huo usaili, kama wako radhi wewe kuulizia juu ya matokeo ya usaili waliokufanyia au la. Wengine hawajali kama utaulizia na wengine hawapendi. Hivyo ni vizuri ukajua msimamo wa kila mwajiri wako mtarajiwa.[/SUP]
 
Kama ipo ipo na kama haipo haipo tu, uliza ujue unajiwekeaje mipangilio yako mingine maana ynaezaendelea kusubiri ukawa unapoteza muda tu na si kawaida kwa watanzania kuwajulisha watu ambao hawajafaulu usahili.
 
Back
Top Bottom