Hao hawafanyi brokering kwa kukutafutia wateja. Ni sawa na wewe upeleke bidhaa zako supermarket.
Wamiliki wa supermarket hawawezi kulazimisha wateja wanunue bidhaa zako.
Muziki wa Nigeria uko Marekani kwa kiasi kikubwa kutokana na kwanza ukubwa wa production yao na pili wingi wa Diaspora huko majuu.
Wanigeria wameteka muziki wa Africa na Diaspora wengi sana nje.
Hata msanii wao akienda kufanya shows nje anapata watu wengi sana, Nigerians plus other Africans.
Juzi tu hapa kuna dogo Mnigeria aliuza album ya Wizkid kimagendo kupitia Apple Music na ndani ya muda mfupi alikuwa ameshapata zaidi ya 100M!
Sasa unadhani Wizkid huwa anakunja pesa kiazi gani.
Soko la bongo fleva bado liko nchi chache sana hasa Kenya, Rwanda, DRC, na nchi nyingine chache sana.