Dili: Natafuta watu 5 nishirikiane nao tuanzishe kampuni ya mchezo wa kubahatisha

Dili: Natafuta watu 5 nishirikiane nao tuanzishe kampuni ya mchezo wa kubahatisha

mbagokizega

Senior Member
Joined
Oct 22, 2016
Posts
111
Reaction score
297
Salaam wakuu.

Nimevutiwa na taarifa niliyoisoma kwamba kampuni Fulani inayojihusisha na michezo ya kubahatisha imelipa bilioni mia mbili na milioni mia moja kama kodi kwa kile walichoingiza mwezi September.

Hii inamaanisha wabongo wamechachamaa haswa ktk kucheza kamari manaake kama kodi tu ni kiasi hiko bila shaka jamaa wamekunja mabilioni kadhaa kwa mwezi wakiwapa washindi kiasi kadha huku wao wakibaki na burungutu la maana.

Kwa hali ya kiuchumi ilivyo matumaini ya wabongo wengi kutoka kimaisha kwa njia walizozizoea zimeyeyuka ama watu hawaamini kuwekeza ktk biashara kunaweza kuwaletea matokeo mazuri mana nako kuna mdororo ndio hapo watu wameangukia ktk kuamini kwamba jero zao zinaweza kuzaa milioni sitini au kupitia buku ghafla wavune milioni themanini.

Mi sijui lolote kuhusu uendeshaji wa michezo hii lkn naamini kabisa njia hii itatupa pesa nyingi kwa mda mfupi tena tukiwa na uhakika kabisa ndipo nimejitokeza hapa kuomba nguvu ya watu wa5 tufuate taratibu tuanzishe mchezo huu.hii ni fursa tusiiache ipite.

Ahsanteni
 
yani unamaanisha tufungue kampuni ya kubetisha?
 
Hauna mtaji wa kuanzisha na kufanya marketing
Na pia unaweza liwa hata bilioni ndani ya siku 1
 
Kuanzisha kwake ni zaidi ya billion moja cash....leseni na vibali toka TCRA. System zake ni cheap (system+mobile app ni kama tzs 30M)
 
Back
Top Bottom