Dimba la Amani Complex Zanzaibar lafungwa kwa muda kufanyiwa ukarabati

Dimba la Amani Complex Zanzaibar lafungwa kwa muda kufanyiwa ukarabati

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetangaza kuufunga kwa muda wa miezi miwili Uwanja wa New Amaan Complex kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa wa eneo la kuchezea (pichi), kwa kung’oa nyasi za zamani na kupanda mbegu mpya za nyasi.

Uamuzi huo unalenga kuandaa uwanja huo kutumika kama uwanja wa mazoezi kuelekea Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, ambapo Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) linatarajiwa kufanya ukaguzi na kuanza vipimo rasmi kuanzia Januari 2027.

Mchakato wa Ukarabati na Sababu Zake Katika eneo la New Amaan Complex kuna jumla ya viwanja vitatu—viwili vya mazoezi na mmoja mkubwa wa mashindano.

Akizungumza kuhusu maandalizi hayo, Kamishna wa Idara ya Michezo Zanzibar, Ameir Moh’d Makame, alieleza kuwa mchakato wote wa kung’oa nyasi zilizopo, kupanda mbegu mpya, kuota hadi kuanza kukatwa utachukua takribani miezi miwili.

Athari kwa Timu za Zanzibar na Mipango Mbadala Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), Hussein Ahmada Vuai, amethibitisha kupokea taarifa hizo huku akibainisha kuwa nyasi zilizopo zimeshatumika kwa miaka miwili na zinahitaji kuboreshwa ili kukidhi vigezo vya CAF.

uwanja.png
 
Waufungie tu ili timu za Tanganyika zipunguze kiherehere.
 
Back
Top Bottom