SoC02 Dimbwi la ajabu lisilo na mipaka wala eneo maalum linaloangamiza vijana wa Kitanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Ekubanei

New Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
1
Reaction score
1
Ilikua ni mapema sana majira ya saa 2 Asubuhi katika kijiji cha Hatuchekani mkoa wa Magharibi nikiwa katika mazungumzo na mzee Haambiliki, Niliweza kubaini vyanzo vya maji tiririka yanayoelekea katika dimbwi la Ajabu na linalotisha,sikuwahi tambua kama katika nchi ya Tanzania kuna Dimbwi linalotishia hatma za vijana kwa kasi namna ile ila baada ya kuona vyanzo vya maji hayo hakika niliogopa sana na kubaki katika mshangao.

Sikuweza kuvumilia maana nilihitaji kujua ukweli kuhusu Dimbwi hilo na kama hua lipo katika kijiji hicho tu,nililazimika kumsogelea mzee Haambiliki na kuanza kumhoji nae pasipo kusita alifunguka kunieleza ukweli kuhusu Dimbwi hilo mazungumzo yalikua hivi.

Mimi: Samahani mzee hivi vijito navyoviona ndivyo vinavyopeleka maji katika lile Dimbwi na kwanini haliitwi Bwawa wanaita Dimbwi? Na kama vyanzo hivi vyote huelekea katika dimbwi hilo kwanini serikali isichukue hatua kali za kudhibiti vyanzo hivyo na ikiwezekana dimbwi hilo lifukiwe ili lisiendelee kuwatesa vijana kwa kuangamiza hatma zao na nguvu kazi zao?

Mzee: Hahahaha Kijana sio kwamba nakucheka ila ninakushangaa ina maana ulikotoka hujaona vyanzo vya maji vingine vikielekea katika dimbwi hili? Na unafikiri serikali ya Tanzania hailitambui dimbwi hili? La hasha ndani ya serikali wapo wanaonufaika na dimbwi hili kwa asilimia 100 na ndio sababu hakuna wa kuchukua hatua kubadilisha mkondo wa maji wowote usielekee huko,Pia ndani ya serikali wao ambao hawalijui kabisa dimbwi hili na hata vyanzo hawajawahi ona wala kutambua ni vyanzo vya dimbwi hili la ajabu.

Sasa kijana wangu nataka nikufumbue macho kuhusu Dimbwi hili na endapo utalielewa vema hakika utawaonea huruma vijana wenzako na pia hautatamani hata mtoto mdogo achezee moja wapo ya chanzo cha Dimbwi hili.

Mpenzi msomaji wa Jamii forums usiache ku like na kufuatilia habari hii mpaka mwisho ili upate kufunguka asante
 
Upvote 2
Sawa ngoja tuone ni dimbwe gani hilo.

#MaendeleoHayanaChama
 
dimbwi la madawa ya kulevya au
 
Back
Top Bottom