Nanamshukuru Mungu koto nipa ushabiki wa wakumshabikia mtangazaji au Radio, Zaidi ya timu za mpira wa miguu. Nasikiliza E. FM, kipindi Sport HQ jioni saa 18:30 Kuna kipindi jina nimesahau ila watu wasimulia mikasa waliyokutana nayo. Saa 17:00 kipindi cha michezo, J.pili, baada ya michezo kipindi muziki wa zamani, vipindi vingine naweza sikiliza ila sina ratiba navyo. Radio Uhuru kila jumamosi saa 21:30 kuna kipindi kizuri zaidi cha muziki wa kitanzania wa zamani miaka ya 80-90 vipindi vingine naweza sikiliza ila sina ratiba navyo. Radio free Afrika, naanza saa 05:00 mpaka 06:00 BBC, saa 06:30 magazeti, alhamis, saa 22:00 usiku melenia kuna mziki wa zamani hapa tena hiki yule mkurya Wambura Mtani, ameacha kuendeshi hiki kipindi alikkuwa anaweka miziki mizuri sio kuchanganya na zilipendwa kama anavyofanya huyu wa sasa. Vipindi vingine nasikilliza ila sina ratiba navyo. TBC Taifa jioni njema vipindi vingine naweza sikiliza ila sina ratiba. Kuna TBC nyingine wanakipindi cha kavasha ni kizuri ila ratiba yake bado siijui. Radio zingine nasikiliza ila sina ratiba ya vipindi vyao.