Dini au Kabila, kipi kina Maana zaidi katika Maisha ya Mwanadamu?

Dini au Kabila, kipi kina Maana zaidi katika Maisha ya Mwanadamu?

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,564
Reaction score
8,810
Habari zenu wadau.....

Najiuliza kati ya dini na kabila, kipi hasa kina umuhimu na maana zaidi katika maisha ya hapa duniani kwa mwanadamu?

Mtu anazaliwa katika kabila fulani bila kuchagua, hawezi kubadili kabila lake. Lakini dini mtu anaweza kuichagua, kuifuata au hata kuibadili.

Sasa kama kabila ni kitu tunachokuta tayari tumepewa tangu kuzaliwa, wakati dini ni kitu ambacho mtu anaweza kuchagua, ni kipi kati ya hivi viwili kina nafasi kubwa zaidi katika maisha ya mwanadamu?

Na kama vyote vina umuhimu, basi kwa maisha ya hapa duniani, kipi kinapaswa kuwa na maana zaidi kwa mwanadamu?
 
Chenye maana ni Kabila ndio maana Kila kabila lina Imani yake ya Kuabudu ni vile tu, TUMEASI MILA NA DESTURI..!!
 
Back
Top Bottom