Dini Dini Dini Dini.....Sasa miye nimeanza kuboreka na hizi threads za dini, Je wewe?

Dini Dini Dini Dini.....Sasa miye nimeanza kuboreka na hizi threads za dini, Je wewe?

Je, Sehemu ya Dini/Imani Ifungwe au Isifungwe hapa JF?!

  • Isifungwe

    Votes: 14 43.8%
  • Ifungwe

    Votes: 8 25.0%
  • Irekebishwe

    Votes: 10 31.3%

  • Total voters
    32
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Kibwetere Mtanzania aibuka

Serikali mkoani Mara, imevunja kambi ya mchungaji wa kanisa la Wasabato wenye msimamo mkali, linalohubiri kushuka kwa Yesu mwezi ujao, hatua ambayo imewafanya baadhi ya waumini wake kuanza kuuza vitu vyao.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Bw. Saveli Maketta, aliliambia gazeti hili mjini hapa kuwa kambi ya mchungaji huyo, Ephraem Mtabi, iliyokuwa katika kijiji cha Kyagata, wilayani hapa ilivunjwa Machi 12 kwa ushirikianao wa jeshi la polisi.

Bw. Maketta alisema kuwa mchungaji Mtabi, mkazi wa mjini Bunda, awali alikuwa ni muumini wa kanisa la Wasabato halisi, lakini baadaye alijiengua na kuanzisha kanisa lake ambalo lina msimamo mkali.

Baadhi ya wananchi wamemfananisha Mtabi na \'Askofu\' Joseph Kibwetere, kiongozi wa Kanisa la Kurejesha Amri 10 za Mungu, ambaye alisababisha waumini wake kujilipua moto nchini Uganda kwa kuamini kwamba mwaka 2000 ulikuwa mwisho wa dunia.

Bw. Maketta alisema alipata habari za kuwepo kwa mchungaji huyo katika wilaya yake, kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Luteni mstaafu Chiku Gallawa, ambaye pia alizipata taarifa hizo kutoka kwa raia wema wakiwemo walimu wa shule na wanafunzi, ambao pia walijiunga na kanisa hilo na kuacha masomo.

``Mchungaji huyo amekuwa akihatarisha amani katika jamii, kwa kuhubiri hivyo, kwani watu watakaposubiri bila kumuona huyo Yesu, kwa siku walizoambiwa, wanaweza kukata tamaa ya kuishi, na hivyo wanaweza kujiua au hata kumuua yeye mwenyewe... Sasa sisi kama serikali tumeliona hilo na kuchukua hatua ya kuvunja kambi hiyo mara moja,`` alisema.

Aliongeza: ``Kuna madai ya baadhi ya wanafunzi waliojiunga na kanisa lake kuacha masomo. Tumesikia kwamba baadhi yao hawakufanya mitihani yao ikiwemo ya kidato cha nne.``

Alisema alimuagiza ofisa tarafa kufanya uchunguzi na tathmini haraka, ili hatua zichukuliwe.

Alisema katika mahubiri yake mchungaji huyo alisisitiza kwamba Yesu atashuka mwezi Aprili mwaka huu, katika kijiji cha Kyagata na kwamba amekuwa akiwataka watu mbalimbali wakiwemo waumini wa kanisa hilo kujiandaa, ili waweze kupaa na mwokozi huyo.

Imeelezwa kuwa kutokana na mahubiri hayo, watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi walihama makwao na kwenda katika kambi ya mchungaji huyo ili kushirikiana naye katika kuhubiri ujio wa Yesu Kristo, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wengine waweze kujiunga na kanisa hilo na kukaa mkao wa kumsubiri.

Taarifa zinaonyesha kuwa baadhi ya waumini wenzake walikwishauza baadhi ya vitu vyao, kikiwemo chakula na mifugo, ambapo pia wanafunzi wamekataa kusoma kwa madai kuwa hawawezi kusoma wakati ufalme wa mwenyezi Mungu umekwisha kutimia na hivyo wanasubiri kupaa mbinguni.

Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Bw. David Saibullu, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mahubiri ya mchungaji huyo yanahatarisha amani na kwamba bila kudhibitiwa mapema, yanaweza kuleta maafa makubwa kama ilivyokwisha kutokea nchini Uganda, ambako waumimi wenye msimamo mkali walijifungia kanisani na kujilipua kwa moto.

Kamanda Saibullu alisema kuwa jeshi la polisi linawashikilia na kuwahoji watu kadhaa, wakiwemo wanafunzi wanne.

Walioshikiliwa ni Edina Joseph na Nimrod Machumu, wanaosoma katika Shule ya Sekondari Lubana ya wilayani Bunda, Eliza Joseph, Shule ya Msingi Migungani, Bunda na Manyama Benabato, Shule ya Msingi Namibu A.

Wengine ni Katibu wa kanisa hilo, Mussa Waitaro, mkazi wa Kyagata, pamoja na wazazi wawili wa wanafunzi hao, ambao ni Joyce Paul na Nyanjura Machumu, wote wakazi wa wilayani Bunda.

Kamanda Saibullu, alisema kuwa Mchungaji wa kanisa hilo kwa sasa yuko safarini mkoani Tabora, ambako inadaiwa kuwa amekwenda kuhamasisha watu wengine waweze kujiunga na kanisa lake.

Source: Nipashe

Na serikali ianze uchunguzi kuhusu baadhi ya madhehebu hapa nchini kwani kuna baadhi yanapotosha ukweli na yatasababisha mgawanyiko nchini...
 
Kwa upande wangu kidogo na-beg kuwa na msimamo tofauti.....!
Mara nyingi watumishi wahubirio kweli huzushiwa maneno ambayo si yao.....! We have to listern to this pastor badala ya kusikia maneno toka kwa RPC,OCD hata KATIBU TARAFA....!
Mengi yamewahi kuzushwa juu ya watumishi wa Mungu kama Z.Kakobe, D. Maboya,Gwajima,Kulola,Lwakatare nk...!
Na katika hili hata jamii inayozunguka hapo inaweza ikawa imepotoshwa vile vile
The only reliable source of this issue is the Pastor himself,elders of the church and current members( sio waasi ambao huweza sema mabaya tu)
Tukishapata haya sasa tunaweza kuwa na ground ya kuanza mazungumzo haya.....! NIMEELEWEKA?
 
Serikali imefanya vibaya maana wanajua haya yaliwahi kutokea uganda basi wangepeleka maaskali kanzu wake mle ndani kudhibiti hali yoyote ile ambnayo ni tofauti. maana Dini ni imani na inawezekana kwa imani na mahesabu ya Dini husika walishauona mwisho wa Dunia kama jinsi wanavyotazamia sio wajinga wale waumini wanafanya wanachokiamini kuwa ni kweli, Namaliza kwa kusema Serikali iwaache tuone huo mwisho ulivyo. Duniani kuna vituko vingi!!!
 
Umesikika Msanii! sasa tulia sikiliza.

Dini tulizonazo tumerithi kutoka kwa wazazi wetu huwezi kuzaliwa na wazazi wakristo na wewe ukawa Mwisilamu ni mwiko, maana mtoto utamlea kwa kumpeleka Madrasa au Sunday School, sasa huko wanafundishwa nini , Vurugu ndio iko hapo. wapo wanaojifunza maadili mema na wapo wanaojifunza ushari kila kukicha badala ya kuchambua kitabu chake anaanza kuchambua kitabu cha mwenzake matokeo ni nini ndio haya tunayoyaona sasa.

Waislamu wanaamini Kuruani imeshuka haikuandikwa hapa duniani, hilo halina ubishi na wakristo hawapingi kwa sababu hawajifunzi kubishana na hawa watu wanapandikizwa ubishi huu ambao sio asili yao. Sasa na wao wakristo wanaposema Yesu ni Mungu ubishi unaozuka hapo utafikiri umewatukana waumini hawa, sijui ni kwa nini wakati wao walisema Kitabu chao kimeandikwa na Mungu na wanaamini hivyo lakini wanashindwa kuamini kuwa Yesu ni Mungu.

JF ina mada nyingi mno ni forum pekee ambayo unaweza ukasoma usiku na mchana bila mada zingine kuziona wala kuzipitia hivyo kusema kwamba wachangiaji wameishiwa hoja ndio maana wamekimbilia kwenye Dini Si kweli NGOJA NIKUPE USHAURI WA BULE USIANGALIE THREAD ZA DINI, UTAKUWA NA AMANI.lakini acha watu waseme tunagundua vingi maana akili ya binadamu hukua kwa kujadiri mambo, na Uhuishwa kwa kusikia na hushituka kwa kuona.
 
Hii section ya dini ifutwe...tunakoelekea ni kubaya..Steve D naye alishatoa mapendekezo kama haya!

Nina wasi2 tunakoelekea na thread za dini!
 
Mimi nadhani section ya dini isifungwe kwa kuwa kwa sasa waislam Tunaongoza kwa hoja motomoto na uwezo wa kutetea dini yetu.Yeyote anayetaka section hii ifungwe ni wazi kuwa kashindwa kutetea anachoamini. Hakuna cha kashfa wala nini hii ni kampeni kabambe inayoendeshwa na walioshindwa kwenye maandiko.
 
Mijadala ya dini endapo itatumika vibaya basi na ifutwe,lakini kama itatumika kelimisha walengwa wa dini husika haina tatizo.Mijadala ya dini isimamie katika kuimarisha misingi ya dini yao na sio kuanza kuanzisha madai ya kwamba dini fulani haifai,hii inaweza kusababisha mfarakano wa mkubwa sana katika jamii.

Ikumbukwe kwamba dini ni imani na kila mtu anao uhuru wa kuabudu anapoona ukweli upo na sio kuanza kukashifu dini fulani kwamba eti haifai.

Mjadala huu usifungwe isipokua kukashifiana kusiwepo kwa kuamini kwamba wote hatuwezi tukaacha uislamu na tukahamia ktk ukristu vivyo hivyo wakristu wote hawawezi wakaacha ukristu na kwenda uislamu.

MUNGU ATUONGOZE KWA HILI.
 
Wana JF, hivi imekuwaje, kila nikiamka threads za dini zinazidi kumiminika tu... na ingekuwa bora kweli kama hizi threads zingekuwa si za kukashifiana katika mambo haya ya imani kama inavyoonekana hivi sasa, maana kuna wengine katika mambo haya wanamisimamo mikali usiombe, kujadiliana nao ni kama kupoteza muda haswaa. Hivi sasa, mengi ninayo yasoma ni kuwa dini hii bora zaidi ya hii, dini hii ina mtume bora kuliko dini ile, sherehe hii haina maana kuliko sherehe ile, tukio hilo ni la uongo na hili ni la kweli... mimi nimeanza kuchoshwa na haya mambo. Hivi hawa watu ni WAUMINI wa dini kweli ambazo nyingi naamini zinataka uvumilivu, kusameheana na kufundishana yaliyo mema?!

Unajua nini, kama dini ndizo ziko hivi mimi bora nirudi kwenye dini za makwetu tu, dini za Kibantu kabla Afrika yetu haija vamiwa na wageni na kututawala. Mfano wa dini zile za akina Kinjeketile na akina Mwanamalundi... maana hizi ambazo naziona hazina asili ya Kibantu zinazidi kuandamana kila moja zidi ya nyingine katika kutafuta IMANI YA KWELI.

Kwa kweli ningependa kabisa forum ya dini iwepo kwa ajili ya kubadilishana mawaidha, kutafakari na kupashana habari kuhusiana na imani tulizo nazo, na wale wasio amini kitu basi kusoma habari za imani hizi na wao kuwa na maoni yao BILA KUTUKANANA.

Lakini kwa sasa hiyo sehemu ya dini imebadilika ghafla na kufanywa uwanja wa kugombania waumini. Kwa kweli miye naona hili si jema hapa JF. Hivyo basi naomba ushauri wenu kwa kupiga kura;

JE, SEHEMU YA DINI IFUNGWE ISIFUNGWE au Ifanyiwe marekebisho?!

Ukichagua IREKEBISHWE, naomba uendelee kutoa mawazo yako kwenye thread hii namna ya kufanya marekebisho hayo.

Nitamwomba Admin atengeneze Poll, ili tupige kura zetu kama hili linafaa.

Naomba kutoa hoja. Ahsanteni.

SteveD.
Mimi sikubaliani kabisa na mawazo yako. Kwani naona yanaelekea upande mmoja. Kuna hoja nzito na za maana zilizotolewa ila inaonekana wafuasi wa upande fulani wanapoguswa ndo inakuja hoja ya matusi. Hakuna matusi ila we dare to talk openly. Na kwanza hiyo poll yenu imepitishwa na nani mbona maamuzi ni ya haraka mno wakati wengine wamelala na wengine bado kufika kwenye mitandao?
Acheni hoja zimiminwe na mkishindwa kujibu hoja hizo basi kaeni kimya ama mkubali kushindwa. Hapa hakuna maandamano ila kuna kuheshimu michango ya watu.
 
Mimi nadhani section ya dini isifungwe kwa kuwa kwa sasa waislam Tunaongoza kwa hoja motomoto na uwezo wa kutetea dini yetu.Yeyote anayetaka section hii ifungwe ni wazi kuwa kashindwa kutetea anachoamini. Hakuna cha kashfa wala nini hii ni kampeni kabambe inayoendeshwa na walioshindwa kwenye maandiko.

1. Mimi ni memba wa kudumu kule kwenye zile thread za Deen & Imaan sijaona hizo hoja motomoto unazosema nd. Slave, au labda mwenzangu unasoma maandishi kutoka kulia kwenda kushoto? Mhh..

2. Kwa upande wangu naomba hiyo section ya Deen & Imaan indelee hivyohivyo, najua kuna watu wanakerwa na 'deen'(its actually a cult) & 'mtume' wao muflisi kuanikwa hadharani, wanaleta vituko viingi(wenyewe wanaita ushahidi)..lakini kelele zao tunazidhibiti..taratibu ukweli unaanza kushamiri..
 
Last edited by a moderator:
Wana JF, hivi imekuwaje, kila nikiamka threads za dini zinazidi kumiminika tu... na ingekuwa bora kweli kama hizi threads zingekuwa si za kukashifiana katika mambo haya ya imani kama inavyoonekana hivi sasa, maana kuna wengine katika mambo haya wanamisimamo mikali usiombe, kujadiliana nao ni kama kupoteza muda haswaa. Hivi sasa, mengi ninayo yasoma ni kuwa dini hii bora zaidi ya hii, dini hii ina mtume bora kuliko dini ile, sherehe hii haina maana kuliko sherehe ile, tukio hilo ni la uongo na hili ni la kweli... mimi nimeanza kuchoshwa na haya mambo. Hivi hawa watu ni WAUMINI wa dini kweli ambazo nyingi naamini zinataka uvumilivu, kusameheana na kufundishana yaliyo mema?!

Unajua nini, kama dini ndizo ziko hivi mimi bora nirudi kwenye dini za makwetu tu, dini za Kibantu kabla Afrika yetu haija vamiwa na wageni na kututawala. Mfano wa dini zile za akina Kinjeketile na akina Mwanamalundi... maana hizi ambazo naziona hazina asili ya Kibantu zinazidi kuandamana kila moja zidi ya nyingine katika kutafuta IMANI YA KWELI.

Kwa kweli ningependa kabisa forum ya dini iwepo kwa ajili ya kubadilishana mawaidha, kutafakari na kupashana habari kuhusiana na imani tulizo nazo, na wale wasio amini kitu basi kusoma habari za imani hizi na wao kuwa na maoni yao BILA KUTUKANANA.

Lakini kwa sasa hiyo sehemu ya dini imebadilika ghafla na kufanywa uwanja wa kugombania waumini. Kwa kweli miye naona hili si jema hapa JF. Hivyo basi naomba ushauri wenu kwa kupiga kura;

JE, SEHEMU YA DINI IFUNGWE ISIFUNGWE au Ifanyiwe marekebisho?!

Ukichagua IREKEBISHWE, naomba uendelee kutoa mawazo yako kwenye thread hii namna ya kufanya marekebisho hayo.

Nitamwomba Admin atengeneze Poll, ili tupige kura zetu kama hili linafaa.

Naomba kutoa hoja. Ahsanteni.

SteveD.

...Great Stuff SteveD.

Naunga mkono hoja, hako ka section kanaboa!

IMANI kila mtu na yake, ndio maana ikasemwa, "mimi nina Dini yangu, nawe una yako!", ukiona watu wanahitalafiana mpaka wakaanza kutukanana na kudhalilisha dini za wenzao na mitume ujue IMANI ishawapungukia hao!. wanafuata 'USHABIKI', kama wale washabiki wa Lords Resistance Army, Al Qaeda, Kibwetereism, Branch Davidian (waco fire!) nk!!!

nitarudi...
 
...Ndugu, wazo jingine lililonijia kutokana na kuthamini michango ya wale wanaopinga mawazo yangu ya: kufungwa jumla jumla, kufungwa kwa siku kadhaa katika wiki,au lile la kuruhusu mada moja kwa siku kwa member; ni kwamba:

... labda basi wachangiaji wa mada za imani/dini zilizo na msimamo mkali na zenye kuleta utata au kuonekana zinakashifu au kudharilisha imani/dini za wengine - wawekewe mtego maalum; yaani waombe kwa Admin u-membership utakao waruhusu wao kuchangia mada hizo katika mrengo huo, hivyo kuifanya forum ya dini/imani au kipengele chake kiwe cha baadhi ya watu fulani tu. Na kwa maana hiyo kipengele hicho (forum/subforum) isionekane kwa watazamaji na washiriki wa JF kwa ujumla, mithili ya forum ya 'mambo ya kikubwa'. Ambako member ni lazima a-apply kwa admin kuangalia au kupost huko. Ahsanteni.

SteveD.
 
... mithili ya forum ya 'mambo ya kikubwa'. Ambako member ni lazima a-apply kwa admin kuangalia au kupost huko. Ahsanteni.

SteveD.

Hapo utakuwa unakosea mheshimiwa..masuala ya deen na imaan sio optional ya nyongeza..Hapa tunazungumzia na kujadili mustakabali wa roho za watu, iweje tuiweke kihivyo?

Hapo sio mzee..
 
Hapo utakuwa unakosea mheshimiwa..masuala ya deen na imaan sio optional ya nyongeza..Hapa tunazungumzia na kujadili mustakabali wa roho za watu, iweje tuiweke kihivyo?

Hapo sio mzee..

Mtindio, nashukuru kwa hoja yako. Nimetoa wazo hilo kutokana na kuona maneno mengi ya kukashifiana ambayo wewe ukiwa mmojawapo na wengineo wengi wapinzani wako mnayaendekeza. Kwa kweli mara nyingi mimi sioni hekima, unyenyekevu, busara au mwonjo wowote wa ucha Mungu kwenye mengi mnayoshindania. Ndiyo maana nikatoa hilo wazo likiwa mojawapo ya mapendekezo mbalimbali niliyokwishatoa.

Kama nilivyosema kuna baadhi ya mliowachangiaji huko hoja zenu zilizo nyingi zimekaa ki-fundamentalist (naomba mnisamehe kwa kutumia neno hili), hivyo katika kuepusha kuwakwanza wasomaji wengi na wacha Mungu walio moderate, nimependekeza hilo wazo, ya kuwa forum ya dini inaweza kuwekewa subforum yake ambayo mtu itabidi akubaliane na masharti ya kuwa atakachokisoma kule kinaweza kumfedhehesha, kumpandisha jazba n.k. Vitu ambavyo vikiandikwa kwenye majukwaa au kuongelewa kwenye open forum kama vilivyo vingine vitaacha adha mioyoni mwa waumini wengine.

Mtindiowaubongo, kama utakumbuka sawasawa, kabla ya jukwaa la mambo ya kikubwa kulikuwa na jukwaa la games/sports & entertainment, member fulani fulani walikuwa wanajaribu kuweka hata picha za ngono kwenye hilo jukwaa. Mpaka hapo lilipo tenganishwa na kuwa na majukwaa kama matatu hivi, la mambo ya kikubwa, la michezo na la entertainment. Hapa utakubaliana nami kwamba kuna member wengi waliomba ruhusa ya kuweza kuingia kwenye mambo ya kikubwa na kuweza kudiscuss kule without limitations, but at the same time watu tuliwezeshwa kuweka picha zenye rather ya 'ku- entertain' kwenye jukwaa la entertainment na kuepusha shari maana kuna picha nyingine zenye kuintatein ziko off-scale, hivo ni xrated na inabidi pelekwa kwenye mambo ya kikubwa.

Natumaini umenielewa, samahani kwa maneno mengi.

SteveD.
 
Mtindio, nashukuru kwa hoja yako. Nimetoa wazo hilo kutokana na kuona maneno mengi ya kukashifiana ambayo wewe ukiwa mmojawapo na wengineo wengi wapinzani wako mnayaendekeza. Kwa kweli mara nyingi mimi sioni hekima, unyenyekevu, busara au mwonjo wowote wa ucha Mungu kwenye mengi mnayoshindania. Ndiyo maana nikatoa hilo wazo likiwa mojawapo ya mapendekezo mbalimbali niliyokwishatoa.

Asante kwa reply.

Suala la 'kukashifu' hilo nafikiri tulishalimaliza, kwani kuna kipindi kuna kijimtu aliwa-pump mods ili wa-press ban, niliomba tu-define 'kashfa' na 'matusi', tukashindwa kufikia muafaka..Kama tatizo ni 'kashfa' na 'matusi' ni vyema tulifanyie hili kazi na kuona mwisho wake, kuliko kulifanya jambo la deen na imaan kuwa jambo linastahili passwords na limited access..

Shukrani..
 
Imani za kidini ni zaidi ya vituko vinavyojadiliwa hapa. Japo sijapitia hoja nyingi sana kwa sababu hakuna chakujifunza kwenye hoja hizo, chache nilizopitia hapa hazina uhusiano na kile tunachojaribu kujadili. Hoja nyingi zinajaribu kujadili au kupata majibu ya maswali ya dini za kiislamu na kikristo. Lakini watoa hoja na wajibu maswali wanaandika vituko ambavyo kwa kweli vinashusha hadhi ya Forum, nia ya mijadala na hata kukashifu ukweli wa imani zenyewe. Sidhani kuna haja ya kuvumilia jambo lolote linalopotosha ukweli. Ni hatari kwetu. Wengi wetu tunataka kutumia ubabaishaji wa ufahamu wa juu juu kujaribu kuonyesha kwamba tuna ufahamu mkubwa sana wa maswala ya imani. Na hivyo kubahatisha kutoa hoja au kukashifu dini za wengine bila sababu
Ningeomba kuwakilisha ombi la kufuta mijadala hii ya dini. Ili kama kuna wale walio na haja ya kujua ukweli kuhusiana na maswala ya imani wajifunze kwa wazazi, makanisani, misikitini, vyuoni na kwingineko. Wale walio na imani wabaki na imani zao bila kujisikia kukashifiwa. Kwa kweli sioni uwezekano mkubwa sana wa mtu kumjua Mungu kupitia JF
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom