Dini haiokoi ila Yesu. Mtafute na kumshika Yesu na siyo dini

Dini haiokoi ila Yesu. Mtafute na kumshika Yesu na siyo dini

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
4,014
Reaction score
4,600
Dini ni utaratibu aliouanzisha mwanadamu katika kumtafuta na kumuabudu Mungu wake..

ila YESU ni Mungu aliyejinyenyekeza kujishusha kuvaa mwili wa mwanadamu,kuzaliwa kimasikini katika zizi la ng'ombe,kaishi maisha ya duniani na kuwa rafiki na kukaa pamoja na wanadamu wenye dhambi(Emmanuel) ili hali yeye ni mtakatifu bila kuwahukumu,kutoa upendo na kuwahurumia wanadamu na kuwa tayari kuwa sadaka afe kwa ajili ya kulipia deni za wote wenye dhambi.

Yesu anakupenda wewe mwanadamu mwenye mwili jinsi ulivyo hivyo hivyo ili uje na uchafu wako na dhambi zako hata kama ni nyekundu kama bendera ,anasema njooni kwangu wote msumbukao na kulemewa na mizigo mbalimbali ,nami nitawapumzisha

Mtishweni mizigo yenu ataichukua dhambi ya ulimwengu wote anaisulubisha na kufa nayo pale msalabani ,kwa kupogwa kwake sisis tinapon,anafanyika aibu ,laana..ili sisi tufanyike heshima,na baraka,na tupate uzima wa roho na mwili.

Damu yake imelipa gharama ya dhambi zetu zote ,tunahesabiwa haki kupitia yeye...

jina lake lina nguvu na damu yake kutukomboa na kutuweka huru ,tena huru kwelikweli,tunahesabiwa haki kwa neema kwa imani kupitia kumkiri nankumuamini yeye na kumtegemea yeye.

Turuhusu YESU atusaidie mana peke yetu hatutaweza ,Yeye hujishughulisha sana na mambo yetu.
.Yeye ni njia ,kweli na UZIMA.

Katika hiyo dini yako mtafute YESU mana yeye Yesu ndiye uzima wako.
 
Mit 3:5-6
Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.

Peke yako hutaweza unahitaji Mungu akusaidie.
 
DINI NI NJIA ZA WANADAMU
(njia za wanadamu) huwa ni njema machoni pao wenyewe Mithali 21:2
Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake, bali BWANA huupima moyo.

LAKINI NJIA ZA MWANADAMU(DINI)
Mit 16:25
Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti.

NJIA SAHIHI NI IPI,DINI YA KWELI NI IPI
Yn 14:6
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

KATIKA HIYO DINI YAKO MTAFUTE YESU

Mdo 4:12 SUV
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

Kut 33:15
Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa.
(BILA YESU USIKUBALI)
 
bila msaada wa yule mtu mwenye kung'aa nuru ukiyemuona ndotoni anayeitwa YESU hutaweza peke yako kujiokoa mwenyewe wala hakuna mtu mwingine yeyote awezaye kumuokoa mwanadamu isipokuwa YESU pekee na yeye Yesu ndiye NURU,NJIA ,KWELI NA UZIMA.

usitegemee vitu au watu wengine au viumbe wengine wala usitegemee dini yako wala nguvu zako wala akili zako ...ni YESU PEKEE mwokozi awezaye kuokoa.
 
Back
Top Bottom