cupvich
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 408
- 247
UTANGULIZI.
Nafungua kamusi yangu ya kiswahili na Kutambua kuwa Neno "DINI" ni neno la kiarabu lenye maana ya jumla ya imani ya binadamu pamoja na mafundisho wanayotoa kuhusu yale ambayo wanayazingatia ama kuyasadiki, yaani mambo ya roho, kama vile kuhusiana na Mungu, maisha na uumbaji ( Kamusi-wikipedia). Nina jaribu kuwaza kwa undani zaidi na kugundua kuwa DINI ni moja ya chanzo kikuu cha ustaarabu kwa mwanadamu. Na kwa hapa kwetu Tanzania Dini ilipanda ndege na kuletwa na wazungu kutoka Ng'ambo.
DINI YA AWALI NA WATAWALA WAKE
Ninaenda mbali zaidi na kugundua kuwa kabla ya dini hii tuliyo nayo kuingia katika Bara letu la Afrika hususan ni nchini kwetu Tanzania, Mababu na mabibi zetu waliabudu Vitu kama vile mawe, miti, wanyama,Jua na kufanya matambiko kama ibada. Pamoja na ibada hizi za asili kiwango cha ustaarabu hakikuwa kikubwa. Lakini pia Katika enzi hizi za kufanya ibada za matambiko bado wanadamu waliweza kuchagua watawala wao na kwa kiasi kikubwa watawala walitenda HAKI, walisimamia Maadili na kuunganisha jamii Zao kuwa kitu kimoja katika kuleta maendeleo, hizi ni Zama ambazo hakukuwa na RUSHWA wala UKANDAMIZAJI katika maisha, Japo binadamu aliishi maisha ya chini sana ila aliwafurahia MACHIFU waliokuwa wakiongoza.
DINI YA NG'AMBO NA WATAWALA WA KISASA.
Dini ilipokuja kutoka ng'ambo ikaja na Ustaarabu kwa Mwanadamu, maarifa yakaongezeka, binadamu hakutaka tena Uongozi wa MACHIFU bali Watawala waliochaguliwa kidemokrasia. Hapo ndipo tukaanza kuwapata MADIWANI, WABUNGE na Viongozi wengine wa aina tofauti tofauti ambao wanachaguliwa kwa ajili ya Kusimamia maendeleo ya mwanadamu ili yaweze kuendana na mabadiliko ya Utandawazi Duniani katika karne hii ya 21 tunayoishi.
Vivyo hivyo nchini kwetu Tanzania, Mfumo rasmi wa kuwapata Viongozi wetu ambao ndio watawala ukatengenezwa kupitia katiba yetu inayotuongoza. Kwahiyo tokea Uhuru wetu mwaka 1961 tumekuwa tukiwapata viongozi wetu kwa kupigiwa kura na wananchi kwa mujibu wa katiba yetu, na tokea Kipindi hicho tumepata viongozi wengi wa kila aina na kila kiongozi amejitofautisha na mwenzake kwa namna moja ama nyingine. Wananchi wamekuwa wakijitokeza kila baada ya kipindi flani ili kuwachagua watawala wao kuanzia mjumbe katika Shina hadi Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
MATARAJIO YA WANANCHI KWA WATAWALA KARNE HII YA 21.
Kwa namna ya pekee Wananchi wamekuwa na Matarajio makubwa kwa viongozi wao waliowaamini na kuwachagua kutokana na Ahadi tele za maendeleo wanazokuwa wanazitoa wakati wa kuomba kura. Ahadi mbalimbali kama vile Uboreshaji wa huduma za afya na Elimu, Kujenga barabara na Vituo vingi vya afya, Kuajiri watumishi wapya katika nafasi mbalimbali serikalini, kuboresha maslahi ya Wafanyakazi, kupeleka maji na umeme Vijijini pamoja na ahadi nyingine nyingi zimekuwa zikitolewa na Hawa watawala wetu kabla ya kupewa dhamana na wananchi kupitia Chaguzi mbalimbali zinazofanyika nchini.
WATAWALA WAAMINIFU NA WANAO WAJIBIKA.
Ni ukweli usiopingika kuwa baadhi ya Watawala hawa ambao wameaminiwa na wananchi wanafanya kazi kubwa sana ya kuwaletea wananchi maendeleo na wamekuwa wakishirikiana na wananchi bega kwa bega katika kuleta Maendeleo na hivyo kufanya maana halisi ya KIONGOZI au MTAWALA. Isingekuwa watawala Wenye maadili, wachapakazi, na Walio na hofu na Mungu, Tusingekuwa na Maendeleo makubwa ambayo tunayo tokea uhuru wa nchi yetu. Hawa hawa WATAWALA waaminifu ndio wamepeleka UMEME hadi vijijini, wamejenga miundo mbinu mikubwa na kwa gharama kubwa, wamepeleka maji Vijijini, wamejenga madarasa na kuboresha huduma za afya katika hospitali na Vituo vyetu vya afya. Na hadi sasa hawa watawala waaminifu wanaendelea kujenga miradi mikubwa. Hakika tunajivunia Watawala hawa ambao wana hofu ya Mungu.
DINI INAPOGEUKA KICHAKA CHA KUJIFICHA KWA WATAWALA WASIOWAAMINIFU NA WASIOWAJIBIKA
Kwa upande mwingine wapo WATAWALA ambao Bila aibu wamekuwa wakitumia DINI kama kichaka cha Kujificha pale wanaposhindwa kuwaletea Maendeleo wananchi. Wamekuwa wakijifanya wastaarabu siku za ibada ili kuficha Maovu yao na kutaka kujenga imani kwa Wananchi ambao waliwachagua na kuwapatia majukumu ya kufanya. Wamegeza Nyumba za ibada kuwa maonesho kiasi cha kuondoa utukufu wa Mwenyezi Mungu, Huku wakisahau kuwa yupo Mungu anayewaona na kuzifahamu njia zao watokapo na waingiapo.
Viongozi katika Nyumba za ibada bila aibu na pasipo kumuogopa Mungu wamegeuza Mahali patakatifu kuwa mahali pa siasa, mahali ambapo Watawala hujificha na Kumtania Mungu aliyewaumba wazi wazi pasipo hata kuogopa. Hii si sawa kabisa. Katika karne hii ya ishirini na Moja nyumba za ibada zimekosa heshima na utukufu na kusababisha malaika wa Mwenyezi Mungu kuondoka. Hivyo ibada zetu kuwa batili. Siasa imeingia kanisani na kutawala, siasa ndiyo inatoa maamuzi kanisani, siasa ndiyo inachagua viongozi katika Vyumba zetu za ibada, siasa imesababisha migogoro mikuwa katika makanisa na misikiti yetu. Hii yote ni kwasababu ya Kuwaruhusu WATAWALA kuingilia DINI. Haishangazi kuona watawala wakimiliki wajukwaa makanisani au Misikitini.
Wamesahau kabisa lile andiko la HABAKUKI 2:20 kwamba " Bwana yuko ndani ya kanisa dunia yote na inyamaze kimya" na lile la Suurat Al-maida aya ya pili lisemalo" Enyi mlio amini! Msivunje hishima ya alama ya Dini ya mwenyezi Mungu wala mwezi mtakatifu,.........Msikiti mtakatifu kusikupelekeeni kuwafanyia uadui........" . Ni kweli kwamba serikali haina dini lakini watu wake wana dini na wamegawanyika katika madhehebu Mbalimbali.
HITIMISHO
Umefika wakati sasa NYUMBA ZA IBADA ziheshimiwe na watawala, zisiwe vichaka katika kujificha na kutenda maovu kwa Mwenyezi Mungu. Viongozi wa Dini watekeleze majukumu yao pasipo kuingiliwa na Kupangiwa nini cha kufanya katika Nyumba za ibada. Nyumba ya ibada inapo heshimiwa huleta utukufu kwa Mungu na hivyo Mwenyezi Mungu kusikia maombi ya Waja wake. Nyumba za ibada ni chanzo kikubwa cha USTAARABU WA BINADAMU hivyo haina budi kuzitunza na kuziheshimu kwa manufaa yetu sote.
Rejea.
1. Kamusi ya kiswahili
2. Biblia takatifu kitabu cha Habakuki 2:20
3. Qur'an Tukufu Suurat Al-maida aya ya pili
Wenu, Mwita Nm.

Upvote
13