TRIPLE H
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 651
- 349
Wakuu,
Habari zenu?
Katika zama na nyakati tofauti tofauti katika maeneo mbalimbali duniani kumekuwepo na mijadala inayohusisha imani na dini na mara nyingi vitu hivi viwili watu wengi wameshindwa kuvitofautisha.
DINI ni mfumo rasmi wa kitaasisi wenye lengo la kusadikisha watu juu ya mambo fulani fulani ya kiroho na kwa kawaida mtu awaye yote anapozaliwa anafuata dini ya wazazi/walezi wake kama ambavyo anafuata ukoo au kabila lao. Anakuzwa katika mentality kwamba dini hiyo ni bora zaidi kuliko dini zingine na walio wengi ukiigusa dini yake wanahamaki mno kiasi cha kutukana, kugombana na hata kupigana ikibidi. Hawa wanaweza kujitoa muhanga kutetea dini yao. Wako kila mahali duniani na wapo kwenye dini zote ulimwenguni.
Imani ni tofauti na dini.
Hii ni hali ya mguso wa ndani anayoipata mtu KWA KUSIKIA na kuanza kuifuatilia kibinafsi ili kuona kama aliyoyasikia ndivyo yalivyo au ni uzushi mtupu!
Mtu huyu hufuatilia kila kitu Kuhusu JAMBO HUSIKA na akijiridhisha UAMUA mwenyewe kutoka ndani KUAMINI juu ya jambo hilo na kulifuatilia ili kujiongezea uzoefu!
Mtu anayeamini kwa uhakika juu ya kitu/mtu/Mungu/mungu fulani SI MWEPESI WA KUBISHANA ila ni mjenzi wa hoja kusadikisha wengine na asipokubaliwa U-RELAX tu pasipo magomvi ya aina yoyote.
Ndio maana watu wa imani zaidi ya moja waliokomaa katika imani zao MARA NYINGI (si mara zote) huweza kuvumiliana na kuishi pamoja kwa amani na upendo, lkn wana-dini/washika-dini waliobobea ni ngumu kuishi pamoja kwa kuwa kila mmoja anaendeshwa na falsafa ya 'Mwamba ngoma.... '
Je, wewe ukijitathmini, unajiona MSHIKA DINI au MWAMINI?
Kuna ushirika, umoja, taasisi, elimu unayoipigania hata ikibidi kughalimu uhai wako mradi kisiguswe au una amini kibinafsi katika kitu/elimu/jambo/supernatural nk kwa namna ambayo hata ukipingwa na kukataliwa kiasi gani unaoana poa tu?
Utaelewa ukitafakari.