Dini na Imani ni vitu viwili tofauti kabisa, tusivichanganye!

Dini na Imani ni vitu viwili tofauti kabisa, tusivichanganye!

Dini......kuuwa ni dhambi

Wanasiasa wanauwa......lazima kukemea

Dini tupendane

Wanasiasa wanaeneza chuki na migawanyiko, lazima wakemewe maana wanaangamiza Taifa

Dini tusiwe waongo, wachonganishi

Wanasiasa waongo, wachonganishi, lazima wakemewe waache uowongo, fitina na ubaradhuli

Dini ni watchman kuhakikisha siasa inakuwa kwa manufaa na faida kwa Taifa

Ndio maana Desmond tutu akiwa askofu alifanya kazi kubwa kukemea uovu enzi za ubaguzi wa rangi south Africa
 
Dini......kuuwa ni dhambi

Wanasiasa wanauwa......lazima kukemea

Dini tupendane

Wanasiasa wanaeneza chuki na migawanyiko, lazima wakemewe maana wanaangamiza Taifa

Dini tusiwe waongo, wachonganishi

Wanasiasa waongo, wachonganishi, lazima wakemewe waache uowongo, fitina na ubaradhuli

Dini ni watchman kuhakikisha siasa inakuwa kwa manufaa na faida kwa Taifa

Ndio maana Desmond tutu akiwa askofu alifanya kazi kubwa kukemea uovu enzi za ubaguzi wa rangi south Africa
Umeenda nje kabisa ya mada
Dini Vs Imani
Wewe umekuja na Dini Vs Siasa
 
Ninavyojua

DINI, ni utaratibu wa kufanya matendo ya aina fulani kila wakati.
Dini ipo kwenye kipengele cha Utamaduni.
Tunaweza kuwatambua Wabudha au Wahindu au Wakristo kwa kuwaangalia wanavyofanya katika maisha yao.
Mwislamu anajulikana kwa kutenda matendo kwa usahihi yaliyoko katika Nguzo Tano za Uislam

Kushahadia
Kuswali
Kutoa Zaka
Kuhiji
Kufunga Ramadhani

Ukifanya haya unavyopasika basi wewe ni Dini yako ni Uislam.
Dini ni kutenda jambo yanayo onekana na wengine.

Ndio maana Yakobo anasema Dini nzuri ni ile ambayo watu wanafanya matendo na kusaidia watu wenye uhitaji, yaani Upendo kwa jirani,
Dini mbaya ni ile inayofanya matendo ya kumkosea jirani.

IMANI, ni tumaini la baadae.
Mfano.
Mtu anaamua kusoma kwa bidii kwa kutumaini kwamba, baadae atapata ajira itakayoboresha maisha yake.
Yayo ni matarajio yake ya baadae, anaamini hivyo. Imani

Mwislam anatenda matendo yaliyoko katika Nguzo tano za Dini yake kwa tarajio la kufika Mbinguni kwa Mungu wake hapo baadae.
Pia kupata Ridhaa na Msamaha toka kwa Mungu wake.
Hivi ndivyo anavyo amini yeye ndani ya moyo wake.

Basi, Dini ni Matendo, alihari Imani ni tumani la matokeo ya matendo yako.
 
Waebrania : Mlango 11

1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

Yakobo : Mlango 1

27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.

Asante sana Bujibuji..... Kwa mukhtasari huu!!
 
Tuache kuandika mada zakipumbavupumbavu tukidhalilisha kizazi hiki.

Viongozi wakiroho wakikaa kimya waumini wakachinjwa wote nani atakaenda huko misikitini na makanisani?

Unaanzaje kutenganisha dini na siasa endapo wanasiasa wanaswali Ama wanasali?

Dini na siasa kuvitenganisha nikuwaambia wanasiasa wasiwe waumini, wasiombewe wala wasiombe ushirikiano misikitini wala makanisani

Je inawezekana?
Uyo Mungu mnaemfuata makanisani na miskitini anakuwa wapi wakati watu wanachinjwa?,au nayeye anaitegemea serikali?
 
Back
Top Bottom