Dini za kilokole na imani za ajabu

Dini za kilokole na imani za ajabu

Girland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Posts
2,489
Reaction score
4,253
Imeandikwa: MTAIJUA KWELI NAYO KWELI (Siyo uongo) ITAWAWEKA HURU, kumekuwepo ongezeko kubwa la makanisa na madhehebu mbalimbali huku kila moja wakija na vimbwanga vyake.

Achana na maji ya upako, yanayotumika na makanisa au Chumvi, au Uvumba na vitu vingine kedekede ifuatayo ni list ya vimbwanga.

1. NYWELE ZA WAUMINI, ndiyo! Waumini wa kanisa la Prophet Suguye waliagizwa kwenda na nywele ili ziombewe na wabarikiwe.

2. WAUMINI KUOGESHWA NA SODA katika video inayotrend katika mitandao ya kijamii anaonekana mchungaji akiwamiminia soda vichwani huku waumini wakipanga foleni ndefu kusubiri huduma.

3. WANAWAKE KUOGESHWA NA MCHUNGAJI nchini Ghana Pastor mmoja alidai kupokea maagizo kutoka kwa Mungu akimuelekeza kuwaogesha wanawake ili kuondoa mikosi. Baada ya kuoga walipewa nguo za ndani mpya 😃😃

4. WAUMINI KUCHAPWA VIBOKO imagine waumini wanalala kifudifudi madhabahuni, halafu mchungaji kiongozi na msaidizi wake wanawalamba viboko (kumpiga pepo aliye ndani yao)

Wajuvi wa mambo mtueleze je, mmewahi kusikia hivi vimbwanga na Je ni maelekezo ya Mungu?

Screenshot_20221209-165747.png
 
Alaumiwe nani?? ni wakati sasa wa masihi mkuu kurudi aje awachukue wake mana hakuna ambacho hatujaona.
 
Hivi hujiulizi kwanini imani hizo haziibukii kwenye makanisa ya zamani eg. Catholic.

Kanisa hasa imani hizi za pentecoste zimevamiwa na waabudu shetani Masons, illuminat na occultism. Ingawa hizo zote ni department tofauti ila founder wake ni mungu wa dunia hii ambaye mission yake kubwa ni kuua, kuharibu na kuangamiza.

hana shida na dhehebu lako ila anashida na imani yako. Biblia inasema, hawa chalartans watakuwa na nguvu ya ukengeufu na watapotosha wengi yamkini hata wateule.
 
cha kufurahisha....waumini wanaoenda kwenye hayo makanisa wanatoka kwenye dini/dhehebu lako 😂.
 
Hivi hujiulizi kwanini imani hizo haziibukii kwenye makanisa ya zamani eg. Catholic.
Kanisa hasa imani hizi za pentecoste zimevamiwa na waabudu shetani Masons, illuminat na occultism. Ingawa hizo zote ni department tofauti ila founder wake ni mungu wa dunia hii ambaye mission yake kubwa ni kuua, kuharibu na kuangamiza. Yeye hana shida na dhehebu lako ila anashida na imani yako. Biblia inasema, hawa chalartans watakuwa na nguvu ya ukengeufu na watapotosha wengi yamkini hata wateule.
Wamewezaje kuingia makanisani??
 
cha kufurahisha....waumini wanaoenda kwenye hayo makanisa wanatoka kwenye dini/dhehebu lako 😂.
😂😂😂Ni imani tu mkuu, wakati unashangaa ndio kwanza watu wanajaa.
 
Back
Top Bottom