Kevo,
tukianza kujibu hoja kwa kusema kuwa wa kuwa UFISADI upo na unalindwa na hivyo pesa zipo kulipia watu 100000, kwa mwaka, tunapoteza dira maana huo UFISADI ni kama Zimwi, unasemekana, lakini haujulikani jinsi ya kukamatika na hakuna hatua ya kisheria imechukuliwa katika miaka 3 tangu vuguvugu la kupambana na UFISADI lianze!
Kinachotakiwa kufanywa na TAHLISO ni kutumia USOMI wao kutatua hili tatizo.
Gazeti la Majira linasema kuwa shida ni mikopo na watu kunyimwa vyeti au matokeo kutokana na mikopo.
Sasa swali mchungaji analoliuliza kwa TAHLISO kwenda Serikali ni hili,
- Masharti ya Mikopo yanasemaje?
- Mikopo inalipwa pindi wanapomaliza mhula, mwaka au wakimaliza mafunzo?
- Je mkopo unapaswa kulipwa vipi? ni miaka mingapi baada ya kumaliza mafunzo mkopo unapaswa uwe umelipwa?
- Mikopo hii ina riba ya kiasi gani? je inawezekana kwa wale wanafunzi "masikini" kabisa kupewa mikopo bila RIBA?
Najiuliza kama TAHLISO kama wamekaa chini na kufikiria kinagaubaga hili "TATIZO" la ada na mikopo na si kusukumwa na hisia kutokana na yanayoonekana kuwa ni wazi tunafedha, lakini ni wazi hakuna TIBA.
- Je wamekaa chini na kupeleka mapendekezo Serikalini ya kurekebisha mfumo wa Mikopo ya elimu ya juu hata kubadilisha mfumo wa Utendaji?
- Je wamewatumia Wawakilishi wao (Wabunge, Wawakilishi) ipaswavyo kwenye Bunge na Baraza la Wawakilishi kulizungumzia hili?
- Kama "WASOMI" je wamefikiria kwa kina mantiki ya Sheria hii ya 1999 na kujiuliza ni vipi inaweza kufanikiwa au laa kwa kuwasilisha vitendea kazi na vielelezo?
- Watanzania tumeshupalia sana kusema sisi ni "Masikini" je ni wanafunzi wangapi ambao ni kweli na dhahiri kuwa hata wakimaliza masomo yao hawatakuwa na uwezo wa kulipa deni, kwa kupitia ajira Serikalini, Mashirika ya Umma au Makampuni binafsi?
- Ni kiwango gani wao Wanafunzi wa Vyuo wa Shahada za Kwanza, Shahada za masters hata Udaktari ambacho wanaweza kujilipia au kukopa kutoka Bodi ya Mikopo hivyo kuendelea na masomo?
- Je wameshawasilisha rasmi ama kama TAHLISO au kupitia Wabunge na Wawakilishi mapendekezo ya kubadili mfumo wa kutoa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo na hata kupunguza masharti ya kupata mikopo?
- Mkopaji akishindwa kurudisha mkopo, TAHLISO wanatoa dhamana gani kuhusiana na jambo hili?
Tatizo linakuja kutokana na ufinyu wa mawazo na kuchelewa kwa Tanzania na Watanzania kuamka na kubaini kuwa tupo katika mfumo mpya kabisa wa kiuchumi na kisiasa na hivyo, ni shurti tuanze kuchangia gharama na kujilipia.
Ni kweli kuna baadhi ya Watanzania ambao hawana uwezo kujilipia, hawa wanastahili mikopo au kusomeshwa bure kwa masharti ya utumishi Serikalini au kuendelea kulipiwa shule midhali kiwango chao cha kufaulu kiendelee kuwa cha juu na si chini.
Ubovu wa Sera ya Elimu ya Tanzania ni lile wimbi la kutaka kuongeza idadi ya wanafunzi katika shule za Sekondari, kuongeza idadi ya Wasomi, lakini uwezo wa kubeba Wanafunzi kupitia Vyup vya Serikali ni mdogo. Ama kuendelea kuendesha mambo kutumia mfumo wa kijamaa ambao ulisema wazi kuwa elimu na afya ni bure ni udanganyifu huku tunajua wazi tumeukimbilia Ubepari.
Ningekuwa TAHLISO, ningeanza na mbunge na mwakilishi wangu jimboni, wakishindwa kunitetea Bungeni au Baraza la Wakilishi, then kura yangu hawana!
Nitatoa maelezo zaidi baadaye ya ni jinsi gani TAHLISO wanaweza kuwa Solution ya Tatizo hili na si kuendelea kuwa Tatizo ndani ya Tatizo.