Dira ya Elimu Tanzania

mimi napendekeza kwa kuanzia kuwa na uwazi, hii iwe wazi mfano kwenye website yao.
1. namna na vigezo vya kupima shule, mfano, kwa idadi ya uwiano wa mwanafunzi /mwalimu
madarasa/mwanafunzi,
muda wa masomo/somo
na kadhalika

2. kuwe na utaratibu maalum wa mtaala wa taifa ambao shule zote lazima zifuate. (kama kuna masomo ya ziada ili kuendana na mtaala wa mf. cambridge iwe kama extras)
3. luwe na listi maalum ya shule jinsi zinafyo perform sio kwenye maksi tu za mitihani ya taifa, bali mitihani kwa ujumla.
4. utaratibu wa zamani wamuda wa likizo kwa shule zote urudiwe taifa zima
5. mafunzo ya walimu yawe systematic na yaendane na mabadiliko ya mitaala.
 
Nimesoma Tanzania Daima kuwa TAHLISO inaandaa mgomo nchi nzima kupinga malipo ya ada kwa wanafunzi wa Vyuo kupingana na sheria ya marekebisho ya elimu ya juu ya mwaka 1999.

Lakini kinachokosekana ni sababu za msingi za kukataa kulipia ada. Kikubwa kilichoandikwa na kinaponekana kama hoja kuu ni tofauti zao kati ya TAHLISO na Maghembe!

Huu mgomo ni wanafunzi na familia zao watakaoumia!

Napenda kwa mwenye habari za kina na tamko rasmi na sababu za mgomo huu auweke hewani tuuchambue!

Je chimbuko hasa la mgomo huu ni ugumu wa mikopo, ugumu wa kujigharamia au kuchangia gharama au ni kujibu udhaifu wa Serikali kupambana na ufisadi?

La mwisho nitakalouliza kwa "Wasomi" wetu, pamoja na mgomo huu, je wanakuja na alternative solutions? je wameangalia hali halisi ya uchumi wa Tanzania (keep aside ufisadi stories here!) na kuona kuwa kila mtu anaweza kusoma bure?

I think it is time all cards are placed on the table and TAHLISO better come up with strong argument and solutions that are workable and not run on emotional nitro which will end up in delaying education of millions of Tanzanians!


 
Nadhani la muhimu kuliko yote ni wasomi kugoma rais KIKWETE aachie madaraka! yaani ajiuzulu!

Ng'ang'anieni Kikwete aachie madaraka kwanza na mengine yote mtazidishiwa.

Waberoya
 
Hata kikwete akachia madaraka ndio tutapata solution ?
Nafikili TAHLISO wafikirie jambo jingine la kufanya la kufanya wazazi wa watoto wa Kitanzania kuendelea kufanya Kazi kwa nguvu ili waweze kusaidiana na Serikali katika kuwapa elimu watoto wa Kitanzania. nendeni vijijini mukaone wazazi wanapopata mavuno kwenye mazao yao wanafanya nini kuliko kukaa mjini kushinikiza wanafunzi wagome kwa faida ya nani?😕
 
Hata kikwete akachia madaraka ndio tutapata solution ?
Nafikili TAHLISO wafikirie jambo jingine la kufanya ili kuwafanya wazazi wa watoto wa Kitanzania kuendelea kufanya Kazi kwa nguvu ili waweze kusaidiana na Serikali katika kuwapa elimu watoto wa Kitanzania. TAHLISO kama wataalamu wanafunzi nendeni vijijini mukaone wazazi wanapopata mavuno kwenye mazao yao wanafanya nini kuliko kukaa mjini kushinikiza wanafunzi wagome kwa faida ya nani? sio kukaa na kusoma data kwenye makaratasi na kutuambia tugome hiyo elimu tutaipataje kama tutakuwa wagomaji wa kila kitu na wenzetu wanasonga mbele sie kukaa kugoma tu KALAGHABAHO.😕
 
Mheshimiwa Mchungaji naomba niwasilishe hoja kwamba hawa wanafunzi though hawana solution nyingine zaidi ni wengi sana ambao hawana uwezo wa kulipa ada inayobaki katika asilimia wanazopata.Ukijaribu kuungalia hata uchumi wa nchi unaruhusu serikali kulipia hawa wanafunzi maana fedha zipo.
Suala lingine Mkuu unapotaka watu tujibu hoja kwa hoja siyo kuweka sharti kwamba ufisadi hapa haupo!Ukweli ni kwamba upo na unachelewesha maendeleo ya nchi hii na watu inawauma sana pale ambapo wanaouna wanaibiwa nje nje na watu bado wanaponda raha bila hatua zozozte madhubuti kuchukuliwa!
 
Kevo,

tukianza kujibu hoja kwa kusema kuwa wa kuwa UFISADI upo na unalindwa na hivyo pesa zipo kulipia watu 100000, kwa mwaka, tunapoteza dira maana huo UFISADI ni kama Zimwi, unasemekana, lakini haujulikani jinsi ya kukamatika na hakuna hatua ya kisheria imechukuliwa katika miaka 3 tangu vuguvugu la kupambana na UFISADI lianze!

Kinachotakiwa kufanywa na TAHLISO ni kutumia USOMI wao kutatua hili tatizo.

Gazeti la Majira linasema kuwa shida ni mikopo na watu kunyimwa vyeti au matokeo kutokana na mikopo.

Sasa swali mchungaji analoliuliza kwa TAHLISO kwenda Serikali ni hili,
  • Masharti ya Mikopo yanasemaje?
  • Mikopo inalipwa pindi wanapomaliza mhula, mwaka au wakimaliza mafunzo?
  • Je mkopo unapaswa kulipwa vipi? ni miaka mingapi baada ya kumaliza mafunzo mkopo unapaswa uwe umelipwa?
  • Mikopo hii ina riba ya kiasi gani? je inawezekana kwa wale wanafunzi "masikini" kabisa kupewa mikopo bila RIBA?
Najiuliza kama TAHLISO kama wamekaa chini na kufikiria kinagaubaga hili "TATIZO" la ada na mikopo na si kusukumwa na hisia kutokana na yanayoonekana kuwa ni wazi tunafedha, lakini ni wazi hakuna TIBA.

  • Je wamekaa chini na kupeleka mapendekezo Serikalini ya kurekebisha mfumo wa Mikopo ya elimu ya juu hata kubadilisha mfumo wa Utendaji?
  • Je wamewatumia Wawakilishi wao (Wabunge, Wawakilishi) ipaswavyo kwenye Bunge na Baraza la Wawakilishi kulizungumzia hili?
  • Kama "WASOMI" je wamefikiria kwa kina mantiki ya Sheria hii ya 1999 na kujiuliza ni vipi inaweza kufanikiwa au laa kwa kuwasilisha vitendea kazi na vielelezo?
  • Watanzania tumeshupalia sana kusema sisi ni "Masikini" je ni wanafunzi wangapi ambao ni kweli na dhahiri kuwa hata wakimaliza masomo yao hawatakuwa na uwezo wa kulipa deni, kwa kupitia ajira Serikalini, Mashirika ya Umma au Makampuni binafsi?
  • Ni kiwango gani wao Wanafunzi wa Vyuo wa Shahada za Kwanza, Shahada za masters hata Udaktari ambacho wanaweza kujilipia au kukopa kutoka Bodi ya Mikopo hivyo kuendelea na masomo?
  • Je wameshawasilisha rasmi ama kama TAHLISO au kupitia Wabunge na Wawakilishi mapendekezo ya kubadili mfumo wa kutoa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo na hata kupunguza masharti ya kupata mikopo?
  • Mkopaji akishindwa kurudisha mkopo, TAHLISO wanatoa dhamana gani kuhusiana na jambo hili?
Tatizo linakuja kutokana na ufinyu wa mawazo na kuchelewa kwa Tanzania na Watanzania kuamka na kubaini kuwa tupo katika mfumo mpya kabisa wa kiuchumi na kisiasa na hivyo, ni shurti tuanze kuchangia gharama na kujilipia.

Ni kweli kuna baadhi ya Watanzania ambao hawana uwezo kujilipia, hawa wanastahili mikopo au kusomeshwa bure kwa masharti ya utumishi Serikalini au kuendelea kulipiwa shule midhali kiwango chao cha kufaulu kiendelee kuwa cha juu na si chini.

Ubovu wa Sera ya Elimu ya Tanzania ni lile wimbi la kutaka kuongeza idadi ya wanafunzi katika shule za Sekondari, kuongeza idadi ya Wasomi, lakini uwezo wa kubeba Wanafunzi kupitia Vyup vya Serikali ni mdogo. Ama kuendelea kuendesha mambo kutumia mfumo wa kijamaa ambao ulisema wazi kuwa elimu na afya ni bure ni udanganyifu huku tunajua wazi tumeukimbilia Ubepari.

Ningekuwa TAHLISO, ningeanza na mbunge na mwakilishi wangu jimboni, wakishindwa kunitetea Bungeni au Baraza la Wakilishi, then kura yangu hawana!

Nitatoa maelezo zaidi baadaye ya ni jinsi gani TAHLISO wanaweza kuwa Solution ya Tatizo hili na si kuendelea kuwa Tatizo ndani ya Tatizo.
 

Mazao ya kilimo cha mkono? are you serious? Na kwa nini unafikiri Kikwete hata akijiuzulu solution haitapatikana?! President has nothing to do in this matter?

Waberoya
 

sawa rev.nakusubiri.
 
sawa rev.nakusubiri.

Mwita,

Kama nimechemka kuzungumzia Ufisadi unaouleta Ushahidi wa Deloitte and Touce na Ernst and Young, basi angeshapelekwa mtu jela.

Ulichoshindwa kukielewa katika kauli yangu ni hii vita ya kuondokana na unyonge kukosa nguvu kwa kukimbilia kulaumu UFISADI!

Mpaka leo hii na ushahidi wote uliopo, hakuna FISADI hata mmoja aliyefikiswha mahakamani au kufungwa, Serikali na MAFISADI wameendelea kujenga njama za kuhujumu Nchi yetu huku sisi tunaendelea kulia UFISADI!

Ni tusi kubwa la nguoni kusema mimi nimefaidika na UFISADI!

Kinachotushinda sisi ni kuja na mbinu na kauli mpya za kupambana. Umesema kuwa Wabunge wamefuatwa mara kibao, je kwa nini Wabunge hawa wanaendela kuwakilisha majimbo yao ikiwa Wananchi wao wanateseka na matatizo hayatatuliwi?

Wakati MAFISADI wanaendelea kutumia mkao wa kesho kutwa kuvinjari jinsi ya kuendelea kutudhulumu, sisi tunang'angania mkao wa juzi kuendelea kulalamika!

Bottom line ni kuwa Mgomo utafanyika na hayo yatakuwa mafanikio kugoma, lakini si suluhisho kwa Serikali kubadilisha mfumo wa Elimu au bodi ya mikopo- that is reality and at the end the victims and those who suffer will continue to be the Wanafunzi!

Take a different perspective approach and embrace an advice!
 
By the way Mwita, did you have a chance to read "Waraka wa Mchungaji"? If not search for the thread or send me your email address I will forward Waraka to your attention.
 
Mazao ya kilimo cha mkono? are you serious? Na kwa nini unafikiri Kikwete hata akijiuzulu solution haitapatikana?! President has nothing to do in this matter?

Waberoya
Waberoya
Hata kwa kilimo cha mkono watu wanapata pesa nyingi nenda kaangalie wakulima wa pamba,kahawa na mazao mengine ya chakula mimi nimeona watoto wanasomeshwa kwa pesa kidogo hizohizo wanazolalamika kwamba ni kidogo. Tahliso kama shirikisho la wanafunzi wataalamu wanatakiwa watupe suluhisho la matatizo na sio suluhisho la kuzidisha matatizo. Tanzania ili tuweze kuendelea si lazima turudi kuangalia ilikuwaje mpaka tukaanguka ukiwaumeanguka unaponyanyuka lazima ufikilie nifanye nini ili niweze kutembea sawasawa.
 


kwa faida yako na kwa wanajamii forum ni kwamba, wakati muswada wa bodi ya mikopo umeletwa kwa wadau nilibahatika kuusoma kwa kina, na kuuchangia ili kuuboresha.Nilikuwa mmoja wa watu waliopata nafasi ya kuonana na katibu mkuu wizara ya sayansi na elimu ya juu wakati huo, mama Ruth Mollel pamoja na jopo lake akina lubambula ambae yuko bodi ya mikopo sasahivi.Ni watu ambao hawashauriki na hasahasa mawazo ya wanafunzi.

umewahi kujiuliza inakuwaje waziri anatoa masharti mapya ya mikopo ambayo hayapo kwenye sheria?unakumbuka waziri msola alivyoongeza masharti ya utoaji mikopo kinyume na sheria ya bodi ya mikopo?
 
Jamani hawa wasomi wetu kwanini wasijustfy mgomo wao kwa kigezo cha vijicent vya epa?kwamba hela za epa zingetosha kuwasomesha bure?na kwamba fedha za iptl,richimonduli zingewasomesha hata vitukuu?kwamba culprits wote bwafikishwe kunako stahili/jela?jamii ingeelewa,lakini kwahali ilivyo jamii inawaona wao wagomvi,hawana hoja,lakini wakijustify mgomo kwa vigezo hivyo watapata public sympathy and support,naomba kutoa hoja.
 

Rev,

Nimekuelewa vizuri hapo ila suala hapa siyo kwamba hawa wasomi hawapata njia mustakabali za kudai suluhisho la matatizo yao ila wameshaomba vya kutosha kutoka serikalini ndiyo wanachopata ni majibu ya kebehi kutoka kwa Serikali sasa hii iendelee mpaka lini ilhali hawa wanafunzi watakuja kulipa ada zao mara baada ya kumaliza masomo miaka mitatu baadae kama sijakosea!
Serikali imekosa njia madhubuti ya kudai hizo fedha na ndio maana wanashindwa kugharamia masomo ya wanafunzi!
saas kama serikali haiwezi kugharamia wanafunzi wote iweje mwanafunzi anapotaka kuwa private student wanakataa?Eti wanadai hamna private student una jibu la hili Mkuu?
 

Good observation sir!

Lazima wasomi wetu watafute Kigongo cha justification. Kiwe very clear, solind and conclusive. Kama hakipo bora kuvuta muda na kuangali namna nyingine. Kwenda kufanya attempt na kufail kutawapa mafisadi nguvu kubwa ambayo hawakuwa nayo mwanzoni. Na hakuna nayetaka hilo kutokea.

Ikiwezekana Kigongo hicho waki internalise kiwe na phylosofical, political and all social traits... kiende ndani kabisa na mbali katika kujenga na kusimamisha hamasa ya kijamii na watanzania wote waone manatiki kubwa na ya kudumu.

Kumekuwa na mogomo mingi nchini lakini imeandaliwa in shalow way...ni kweli kuna aina ya mgomo au mass rally of some sort inatakiwa Tz ili kuamasha ari ya kizalendo na utaifa wetu ambao hataimaye itapelekea solutions nyingi kwa pamoja.

Na mgomo au movement kama hiyo iungwe mkono na jumuia mbalimbali za kiajamii...si mara leo wasomi...kesho bank ya makabwela, mara wafanyakazi wa bandari etc....No ....Kuna mgomo au movement inatakiwa.... hilo halipingiki...lakini ni ipi na vipi..we have to really get prapared and go for it once and for all...na nikwenda wote kwa pamoja sio vipande vipande...

Kuna kishindo kikubwa kinatakiwa toka kwa umma wa Watanzania kwa uongozi na viogozi wote waliopo. Ili ikiwezekana watambue nguvu ya WATU!!
 
Nawaunga Mkono Wanafunzi.

TAHLISO na HESLB (bodi ya mikopo) wakae chini na wafanye kazi pamoja. Tatizo Bodi ya mikopo ni wababe

Hela zote wanafunzi wanazokopeshwa... wanalipa zote, iwe asilimia 60,80 au 100!

Pili, HESLB hawatumii vigezo halali kucategorize makundi (wanaotakiwa kukopeshwa % 60,80 au 100). Wapo watoto wa masikini wanakopeshwa 60% na wapo wanafunzi wa matajiri wanakopeshwa 100%. Pia wanafunzi hawana nafasi ya kukata rufaa kama ameangukia kwenye kundi asilomudu.


Mwanafunzi akimaliza masomo anatakiwa kulipa huwo mkopo. Huyo mwanafunzi akiajiriwa atakatwa mshahara. Haijalishi serikali imempatia ajira au amejitafutia ajira kwa juhudi zake binafsi.

Kinachoudhi zaidi, serikali ni kandamizi. Serikali ni kandamizi kwa sababu Mwanafunzi analipa mkopo, pia anakatwa kodi ya mapato ya pay as you earn (PAYE). Bado tena huyu huyu mlipa kodi ananunua bidhaa (mahitaji muhimu hivyo automatically anatoza VAT)

Sasa serikali iseme yenyenye inachangia nini.....Serikali inatakiwa iwafafanulie wananchi kuwa inachangia nini.

Ugomvi hapa ni confusion.
 


Mwita,

Naomba utupe huo muswaada wa mikopo kama ulivyousoma tuuchambue ili tuwe sehemu ya suluhisho na utatui wa tatizo.
 
nimeiona mada hii ni nzuri sana hasa kwa sisi tunaopata ugali wetu kwa kufundisha wanafunzi. ninahitaji kutulia ili niweze kuichangia kwa mapana na marefu kadri ya uwezo wangu. kwa hiyo naiweka kiporo kwa leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…