SoC04 Dira ya maendeleo 2050, bila ya sera madhubuti zenye uwajibikaji ni kazi bure

SoC04 Dira ya maendeleo 2050, bila ya sera madhubuti zenye uwajibikaji ni kazi bure

Tanzania Tuitakayo competition threads

ngatungas

Member
Joined
Sep 16, 2021
Posts
5
Reaction score
13
Bila shaka ni kwamba tunahitaji dira ya maendeleo itakayotuongoza kwa kipindi cha muda fulani,ili kufikia Malengo thabiti yenye maslahi mapana kwa nchi.

je tuna sera imara ambazo zitawabana viongozi na watoa maamuzi ili waende sambamba na Dira hiyo bila kukiukwa??! jibu ni HAPANA.

UWAJIBIKAJI NA VIONGOZI.
Tuna tatizo la viongozi kuwajibika,maana wengi wao wamekuwa ni watu wa kusifia kiongozi mkuu wa Nchi hata pale ambapo ni utekelezaji wa kawaida kimajukumu ya kiserikali.

Vitu kama Barabara, Maji, Hospital bora, Elimu inayoboreshwa na Huduma za kijamii ni wajibu wa serikali na sio zawadi ama Maombi.

Na kitu kibaya hatuna mfumo wa kuwapima viongozi wanaochaguliwa kufanya maamuzi kuanzia ngazi ya chini kabisa kabla ya chaguzi.

Viongozi hawa wasio jua tofauti kati ya wajibu na JUHUDI BINAFSI ndio tunawategemea wasimamie Dira ya Maendeleo ya Nchi?!


ILANI YA VYAMA VYA SIASA WAKATI WA UCHAGUZI VINAONGEA NINI KUHUSU DIRA YA MAENDELEO?

Tunawategemea wanasiasa watuongoze kufika Nchi ya Ahadi.

lakini je? wakati wa chaguzi, wanaongea nini kuhusu hiyo Dira?? na Namna gani wataitekeleza kwa kipindi chao cha uongozi?

Jibu nadhani ni hapana.

Kila chama kinaongeaga juu ya vile muonekano wao wa kiuongozi wanaona utafaa.

Sasa kama ni hivyo, tuna uhakika gani wa utekelezaji madhubuti wa Dira ya Maendeleo kikamilifu bila kuwa na SERA imara zitazo tuongoza vyema?

DIRA ZA KUKAMILIKA KWA MUDA MFUPI.

Lazima kuwepo na sera za dira kukamilika kwa muda mfupi na muda mrefu.

Dunia inabadilika kwa kasi sana, tunaweza tukawa na Dira ya miaka mingi isiyo na tija kama tusipoenda chanya na mabadiliko ya Ulimwengu.

Dira inapaswa itatue matatizo ya Wananchi na kutoa solution ya matatizo kadri ya mabadiliko yanavyokuwepo.

DIRA ZA MAJIMBO/MIKOA.

katika utekelezaji pia wa sera hizi lazima tuweze kugawa Dira kimajimbo.

Maana si kila jimbo linachangamoto zinazofanana.

Na pia kuwa na Dira za kimajimbo ni rahisi kuwapima Wabunge katika utendaji wao.

kwamba kila mbunge itabidi ajinasue kwa Namna anavyotelekeza na kusimamia utekelezaji wa Dira katika jimbo lake.

Na iwe ni kipimo cha uwezo wake binafsi.

kadhalika kwa Mawaziri wa kila wizara, wanapaswa kupimwa kwa vile wanavyotatua utekelezaji wa Dira katika wizara zao husika.

Na Raisi wa Nchi itambidi aweze kutoa au kuteua Mawaziri kulingana na utekelezaji wao wa Dira wizarani. na sio kiurafiki au kukidhi matakwa ya kisiasa.

VIPAUMBELE VYA DIRA KATIKA BAJETI KUU YA KILA MWAKA HUSIKA.
katika kuhakikisha utekelezaji wa Dira husika, itabidi wakati wa vipindi vya Bajeti kuu ya serikali bungeni, kuwepo na Mswada mpana wa Namna gani Serikali inatenga Fedha na Sheria husika kuhakikisha ufanisi wa Dira kwa kipindi kizima cha mwaka wa fedha husika.

Na Sera madhubuti zinapaswa ziwepo katika kuhakikisha fedha husika zinaenda katika Jambo husika kikamilifu.

CAG/TAKUKURU.
Na ni vizuri hata kwa vyombo husika vya ukaguzi wa matumizi ya serikali na kuzuia rushwa yahusike katika utekelezaji wa Dira Ya Maendeleo.

Maana lazima kuwe na ripoti kamili ya kiutendaji wakati wa utekelezaji wa Dira hiyo na kuainisha walakini unaopatikana na kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wale wote wanaofanya uzembe na ubadhirifu katika utekelezaji wake.

Hivyo Umuhimu wa kuwa na sera thabiti na zenye Maslahi mapana mwa nchi ni muhimu katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo 2050.

Ahsante!..
 
Upvote 1
Back
Top Bottom