OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 457
- 773
Naendelea kusoma Dira ya Taifa ya 2050 ambayo inazinduliwa leo. Jambo moja la msingi ni wapi tunapata hela za kutekeleza yaliyomo kwenye dira. Dira imeelezea masuala ya kodi na moja ya matarajio ni kuwa na uchumi jumuishi utakaoongeza uwiano wa makusanyo ya kodi na pato ya taifa.
Uwiano wa kodi na pato la taifa ndio kipimo cha ukusanyaji bora wa kodi nchini. Unakuwa unakusanya kodi vizuri ikiwa uwiano huo ni zaidi ya 15%. Ukiangalia bajeti ya Tanzania ya 2025/26 imeweka trend za uwiano huo kuwa haujavuka 15% kwa muda mrefu sana, infact hatujawahi kuwa vizuri kwenye ukusanyaji kodi.
Sasa kwenye dira ningependa kuona wanalenga kukuza uwiano huu hadi kufika asilimia ngapi ili tuone namna utegemezi wa fedha za nje na mikopo unapungua. Hata hivyo dira hii iko kimya katika jambo hili muhimu kwenye utekelezaji wa chochote.
Moja kati ya study ya ActionAid imeonesha kuwa tukiondoa misamaha mibovu ya kodi na kufanya mambo kadhaa, uwiano wa kodi kwa pato la taifa utafika 28% ambapo tutakuwa na uwezo mkubwa wakugharamia huduma zetu.
Swali jepesi, kwanini hakuna figure ya uwiano huu? Mbona iko figure ya life expectancy, ipo figure ya per capita japo ni ya ajabu. Kwanini hakuna figure ya wazi ya Uwiano wa kodi kwa pato la taifa ili tuone uelekeo kwa usahihi?
JE WALIOANDIKA HAWAKUWA NA WACHUMI KABISA?