Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
MALENGO
Patakuwa na kanda za kilimo zitakazotengwa na serikali kwa ajili ya watu, mashirika na makampuni kufanya shughuli za kilimo. Kanda za kilimo zitatengwa kulingana na mazao yanayokubali eneo husika kulingana na tabia ya nchi na udongo. Kanda za kilimo zitabeba mazao yote yanayokubali eneo husika. Kanda ya kilimo cha korosho, nanasi na mihogo inaweza kuwa Mtwara, Lindi, Pwani, na Tanga. Kanda ya kilimo cha matunda Tanga, Morogoro na Mbeya. Kanda ya kilimo cha ndizi, Mbeya, Bukoba na Kilimanjaro, miongoni mwa mazao mengine.
Katika kutekeleza hili, serikali ni lazima iandae mazingira ya kutoleta mvurugano na watu hasa wale wa kipato cha chini. Serikali baada ya kufanya utafiti na kuzitenga hizo kanda itafanya kama ifuatavyo:
I) Kuandaa afisa kilimo wa kutosha kwa kila kata nchi nzima. Kwa kata ambazo zipo mjini hakutakuwa na afisa kilimo. Kila serikali ya mitaa iwe na ofisi ya afisa kilimo. Hapa nazungumzia ofisi zilizo katika maeneo ya kilimo. Maafisa kilimo watakuwa na majukumu ya kuhakikisha kilimo kwa kata yao kinafanikiwa. Hili iliwezekane pawe na afisa kilimo wilaya, mkoa, na taifa. Hawa serikali iandae majukumu yao. Jukumu kubwa ni kuhakikisha kilimo kinafanya vizuri na mazao ya chakula na biashara yanazalishwa kulingana na hesabu walizopewa.
II) Kila mkulima apewe kibali cha kulima kutoka kwa afisa kilimo kata. Kila kata ambayo ipo ndani ya kanda iwe na kibali chake cha kulima mazao fulani. Hivyo kibali kitaeleza ni mazao gani mkulima wa eneo husika anatakiwa kulima. Sio mkulima alime apendavyo bila kufuata kibali kilichowekwa na wataalamu wa kilimo. Mbinu hii italinda zaidi soko la ndani bila kutegemea soko la nje ya nchi. Wakulima wengi hujikuta wanatumia nguvu kubwa kulima kwa jasho na damu na Mungu wakati mwingine huwabariki lakini wanajikuta katika tatizo la soko kwa maana wakivuna wanashangaa kila mtu nchi nzima kavuna mahindi au nyanya na kufanya bidhaa kushuka thamani na wao kupata hasara. Hii ni tofauti na mazao kama korosho ambayo hulimwa katika mazingira maalumu.
III) Miundombinu ya kilimo kuboreshwa nchi nzima. Kuanzia mbolea, dawa, mbegu, mifumo ya umwagiliaji, teknolojia za kisasa za kilimo na upatikanaji wa barabara. Pamoja na maabara ya kilimo kwa kila kanda nchini.
IV) Ikiwa yapo makampuni binafsi ya kilimo yenye viwanda yataona yatahatarishiwa maslahi yao, serikali itaweka na kuwapa utaratibu wa kiwango cha idadi ya mazao yanayotakiwa kuzalishwa kwa mwaka. Kila kampuni lizalishe kulingana na uwezo wake na ikitokea limeshindwa kwa miaka mitatu mfululizo lifutiwe usajili.
V) Wafanyabiashara wa mazao wapewe njia na eneo la biashara na wasajiliwe kwenye mifumo ya kidigitali. Serikali isajili wanunuzi wa mazao na kuwapangia maeneo ya kuuza. Mfano, Taikon nataka kufanya biashara ya mazao, naingia kwenye mfumo maalumu wa serikali najisajili kisha mfumo unanionyesha sehemu gani nikauzie mzigo wangu. Itakuwa kazi ya afisa kilimo kujua kata yake imezalisha kiasi gani cha mazao, wakulima wa eneo husika watamueleza afisa kilimo kuwa wao kila mmoja anakiasi gani anataka kuuza na kipi hakipo kwenye kata husika. Mfumo utakuwa unakuonyesha utoe wapi mzigo ukauze wapi. Na sio watu wapeleke mzigo sehemu mmoja labda Dar huku mizigo mingine ikiharibika kwa kukosa wateja na maeneo mengine kukosa kabisa au kuuziwa nafaka au zao fulani kwa gharama ya juu.
VI) Bei zitawekwa kwenye mfumo na haitaruhusiwa kwa wafanyabiashara kuja na bei yao. Mfanyabiashara ataingia kwenye mfumo na kuona wapi bei anayoimudu na atakayoweza kupata faida.
VII) Serikali kuandaa maonyesho ya kitaifa ya kilimo kwa kila kanda za kilimo. Maonyesho hayo yataambatana na sikukuu ya wakulima.
VIII) Wakulima watakaosajiliwa wataundiwa chama chao, bima yao ambayo zitahusika katika maslahi yao ikiwemo maslahi ya kupewa pensheni kila mwezi watakapozeeka kama wafanyakazi wengine.
IX) Serikali kuweka ghala la chakula la taifa lililoboreshwa.
X) Vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na filamu zenye kuhamasisha kilimo, chakula na lishe bora zitaongezewa nguvu.
Serikali haitafanya kilimo na biashara ila itaweka mazingira wezeshi na rahisi kwa vijana na wote watakaoamua kujiingiza katika shughuli hiyo.
Taifa likishakuwa na chakula moja kwa moja litakuwa na utulivu, amani, na maendeleo. Hatua ya kwanza ya maendeleo kwa binadamu ni kurahisisha upatikanaji wa chakula na sehemu pekee ya kupata chakula ni kwenye kilimo na ufugaji.
B. Kanda ya Ufugaji
Ufugaji wa mifugo kama ng'ombe, mbuzi, kondoo, kuku, bata, sungura, nyuki, samaki, miongoni mwa mifugo mingine ni lazima uwekwe kwa lengo la kutunza na kuhifadhi mazingira na kurahisisha mahitaji ya watu kupata mazao ya mifugo hiyo, na kujipatia kipato.
Nashauri, serikali iweke kanda za ufugaji kwa kuzingatia tabia ya nchi na utamaduni.
Serikali itafanya hivi:
I) Kutakuwa na kanda za ufugaji kwa wafugaji wa kuhamahama. Watachorewa ramani ya wapi pa kulishia mifugo yao. Itakuwa ni kosa kisheria kwa mfugaji au wafugaji au kampuni ya kifugaji kufuga eneo ambalo halijachorwa kwenye ramani ya wafugaji.
II) Serikali itatengeneza mabwawa ya maji yatokanayo na mvua.
III) Serikali itaweka ranchi kuu mbili:
a) Ranchi kubwa - Hii itakuwa porini au nje kabisa ya mji ambapo hakuna muingiliano baina ya mifugo na watu.
b) Ranchi ndogo - Serikali itaanzisha ranchi ndogo ndogo katikati ya majiji ambapo wakazi wa mjini kabisa wanaopenda kufuga watakuwa wakiweka mifugo yao humo. Haitakuwa ruhusa kwa mtu kufuga kuku kwenye nyumba yake akiwa katikati ya jiji. Hizo ranchi ndogondogo zinaweza kupewa hata kampuni binafsi kuziendesha. Wanaokaa nje ya miji ndio watakuwa na ruhusa ya kufuga kuku au bata, au ng'ombe kwa idadi ambayo serikali itaona itafaa ili kutosumbua watu wengine. Litakuwa ni kosa kisheria kusikia sauti ya jogoo akiwika, au kuku au mbuzi au ng'ombe wakizagaa zagaa mitaani katika miji ilhali kuna sehemu ya kuwatunza. Haki za wanyama zitazingatiwa. Ikiwa mtu au kampuni haina uwezo wa kufuga mnyama yeyote haitakuwa ni uhalali wa kufuga kwani itamtesa mnyama huyo na kuleta usumbufu kwa watu wengine.
IV) Kutakuwa na machinjio za kisasa ambapo mifugo itakuwa inachinjwa hapo. Wenye bucha wote sharti wawe wamesajiliwa na chombo maalumu cha serikali.
V) Mazao ya mifugo kama nyama, ngozi, na mifupa yatawekewa bei elekezi.
VI) Wafugaji wote ambao kazi ya ufugaji watakuwa na chama chao, bima yao na uzeeni watakuwa wakipewa pensheni.
VII) Kitaundwa chombo maalumu cha serikali kinachosimamia na kuendesha shughuli za ufugaji wa samaki.
VIII) Vitaanzishwa vituo vya maziwa na wauza maziwa wote wawe wamesajiliwa.
IX) Kutakuwa na masoko yaliyoboreshwa ya mifugo kama kuku, sungura, bata, samaki n.k.
X) Kila eneo lililotengwa kwa mifugo atakuwepo afisa mifugo.
XI) Serikali itajenga maabara na hospitali kwa ajili ya kutibu wanyama na kufanya tafiti.
XII) Kitaundwa chombo cha kusimamia na kulinda haki za wanyama wa kufugwa.
C. Kanda ya Misitu na Uoto wa Asili
Maeneo ya misitu yatakayotengwa yataongezwa. Upandaji wa miti utahamasishwa. Misitu na miti itakua katika makundi mawili:
I) Misitu na miti ya porini pasipokuwa na makazi.
II) Misitu na miti ya kwenye makazi ya watu. Serikali itahamasisha wananchi kupanda miti na kila kata itapewa idadi ya miti ya kupanda kwa mwaka. Kila kata itatenga maeneo ya kuotesha miche ya miti.
Serikali itaongeza maeneo ya misitu kwa:
Viwanda vitajengwa kulingana na vyanzo vikuu vya malighafi kama vile madini, kilimo, misitu na bidhaa kutoka kwenye mbuga za wanyama pori na vinginevyo.
Serikali itafanya hivi:
I) Kuongeza uwezeshi kwenye elimu ya ufundi na VETA. Hii ni kuhakikisha vijana wengi wanapenda na kujiunga na vyuo hivyo ili baadae wawe na utaalamu wa kutengeneza bidhaa, viwanda vikishajengwa.
II) Kujenga jengo au kugeuza moja ya majengo katika kila mji ambalo mafundi watachukua maeneo na kufanya kazi zao za uzalishaji. Mathalani fundi seremala, fundi cherehani, fundi viatu, fundi magari, fundi hodari wa kutengeneza vifaa vya kilimo kama matrekta, wavuvi wa samaki n.k. hawa wote wawe na jengo lao rasmi.
III) Kila mwaka kuandaa maonyesho ya viwanda vidogo na kutoa tuzo kwa ubunifu na uhodari wa kazi zao.
IV) Serikali kuweka sheria za kodi na vibali rahisi kwa viwanda na bidhaa zinazoagizwa nje ya nchi.
MASOKO, BIASHARA NA UJASIRIAMALI
Serikali itaweka njia rahisi kwa kila raia kufanya biashara au ujasiriamali rasmi na inayolipa kodi.
Serikali itafanya hivi:
I) Tin number itaunganishwa na mfumo wa kifedha wa simu ya kila raia aliyefikia umri wa kulipa kodi. Biashara yeyote ile mtu akifanya kwa kutumia mfumo wa kifedha wa simu kodi itakatwa moja kwa moja na kuingia mfuko wa serikali.
II) Wajasiriamali wote wa kipato cha chini watajisajili katika mfumo huu na serikali itawapa vitambulisho vyao vya biashara.
III) Wajasiriamali wote wanaolipa kodi na wanatumia mfumo wa Tin number watalipwa pensheni wakati wa uzeeni. Watakao shindwa kulipa kodi ya kipato kwa miaka mitatu mfululizo watafutiwa usajili.
IV) Maeneo ya pembeni mwa barabara nyakati za jioni yatatumika kwa wajasiriamali na machinga kwa usimamizi maalumu wa serikali.
V) Kuweka mfumo maalumu kwa madalali, mawakala, wasimamizi na mameneja binafsi. Kwa mfano mnada wa wanyama wafanye kazi zao kwa utaratibu na kila mmoja anayehusika na madalali asajiliwe rasmi na serikali.
VI) Bodaboda hazitaingia highway isipokuwa wenye mafunzo na kupewa leseni ya kuendesha highway.
MAHUSIANO, NDOA NA FAMILIA
Sheria za kudhibiti mahusiano, ndoa na familia zitaboreshwa kwa mujibu wa sheria na haki za binadamu.
Serikali itafanya hivi:
I) Sheria ya ubakaji itabaki palepale adhabu miaka 30.
II) Biashara ya ukahaba iruhusiwe na watakaoifanya wasajiliwe na walipe kodi.
III) Mwanamke kubeba mimba pasipo ridhaa ya mwanaume liwe kosa kisheria. Hili halitawahusu wale waliolewa au walio kwenye uhusiano wa kimapenzi.
IV) Sheria ya kuruhusu kutoa mimba itungwe hasa mimba zilizo katika mazingira maalumu kama ubakaji. Mwanamke aliyechokozwa asitoe mimba kwa ridhaa ya mwanaume wake ni uhalifu na adhabu ya uhalifu huo iwe kali ili kuogopesha.
V) Sheria ya baba atakayeshindwa kutunza watoto apewe adhabu kali.
VI) Kila mwanafamilia sharti afanye kazi. Hii ni kuhakikisha mtu asitegemee kuwa mzigo wa familia nyingine na kumfanya mzazi mmoja kuwa kicheche na kuwa msumbufu wa wengine.
VII) Sheria za kugawa mali zitazingatia mchango wa kila mmoja ndani ya ndoa. Si kweli kuwa mwanamke au mwanaume kugawa mali nusu nusu bila kujua yupi kati yao alikuwa na mchango mkubwa zaidi.
VIII) Haki za watoto wa nje ya ndoa zitazingatiwa kulingana na sheria za asili. Hii ni kusema ni kipi kinachoeleweka ndani ya mila na desturi za eneo husika au jamii hiyo.
Mtibeli
MALENGO
- Kurahisisha maisha ya watu katika uzalishaji na shughuli zao za kila siku.
- Kukuza uwezo wa mtu mmoja mmoja kuchangia nguvu, maarifa, ujuzi na kipaji katika ujenzi wa taifa.
- Kuboresha na kuhakikisha haki na sheria za kulinda utu wa raia vipo kwa ukamilifu katika katiba.
- Kuwaandaa watu na kutunza mazingira na kukabiliana na matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi.
- Kubadilisha mtazamo wa wananchi katika kuunda ulimwengu wa wakati ujao.
- Kuweka mpango wa ongezeko la watu lenye tija.
- Kuwa na sera ya taifa kwa kila sekta itakayotumiwa na vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria.
- Kuyatenga maeneo ya nchi kijiografia kulingana na asili, tabia ya nchi, maumbile ya dunia, n.k. mathalani:

- Kupanda miti ya misitu na maua ya asili katika vyanzo vya maji, na vyanzo vya mito na vijito.
- Kupanda miti na maua ya asili katika maeneo oevu, mashamba na mapori.
- Kuzuia uharibifu wa miti na maua asilia kwenye vyanzo vya maji.