Dira ya Taifa ya maendeleo ya 2025-2050 na Katiba mpya kama njia za kujenga upya( Rebuilding). Hakika Rais Samia anastahili pongezi kubwa

Dira ya Taifa ya maendeleo ya 2025-2050 na Katiba mpya kama njia za kujenga upya( Rebuilding). Hakika Rais Samia anastahili pongezi kubwa

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
1,505
Reaction score
4,427
Serikali ikiwa ipo katika mchakato wa matayarisho ya dira mpya ya Taifa ya maendeleo ya miaka 25 ijayo kuanzia 2025-2050 na hapo hapo kukiwa na mkakati wa kuendeleza mchakato wa katiba mpya, kwa hakika nauona mwanzo mpya chini ya Rais Samia.

Rais Samia akiwa anaongozwa na falsafa za 4R zikiwa ni Reconciliation, Resilience, Reforms and Rebuilding. Mpaka sasa kwa mtazamo wangu n 3R ndio zinazotumika ambazo n Reconciliation (Upatanisho) , Resilience ( Uvumilivu) na Reforms( Maboresho) na R ya mwisho ambayo ni Rebuilding( Kujenga upya) naona itaanza kufanya kazi 2025. Kwa nini?

Ili kujenga upya ni lazima pawepo na nyenzo na nyenzo ninazoona zitakazotumika ni dira ya maendeleo na Katiba mpya ambavyo vyote kwa pamoja vitapatikana kabla na kuanza kutumika baada ya 2025.

Mwenye macho haambiwi tazama maana yanayofanyika ni makubwa mno. Rais Samia anastahili pongezi kubwa kwa sababu tusiposema sisi basi mawe yatakuja kusema siku moja
 
Back
Top Bottom