Diocres Nestory
New Member
- Jul 26, 2018
- 2
- 1
DIRA YA TANZANIA YETU NA SUALA LA AJIRA KWA VIJANA WASOMI
Ndugu wana JF habari.
Kabla ya kuingia katika kiini cha habari hii nipende kutoa maana halisi ya maneno ya msingi yatakayotumika katika habari hii.
Ndugu msomaji, ajira ni kazi zitolewazo au zifanywazo kwa malipo, inaweza kuwa katika serikali, kampuni au Mtu binafsi.
Neno kazi lina maana ya shughuri yoyote halali inayomuingizia mtu kipato.
Ndugu msomaji, haki ya kufanya kazi na kupata ujira stahiki ni haki ya kikatiba iliyotolewa chini ya ibara ya 22 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Hivyo bhasi ni jukumu la serikali kama chombo kilichopewa dhamana na wananchi kuandaa mfumo bora utakao waanda wahitimu kupata kazi au kupata uwezo wa kuweza kufanya kazi halali zitakazowawezesha kupata mapato ya kuendesha maisha yao ya kila siku.
Ndugu msomaji, Kutokana na mfumo wa elimu uliopo sasa, imekuwa jadi ya walimu wengi kuwekeza nguvu kubwa kutimiza matakwa ya mitaala kama moja ya majukumu yao ya kimkataba, ila jambo la ni aina gani ya ujuzi unaofikishwa kwa mwanafunzi linabaki bila majibu. Matokeo ya hali hii ni kuwa na wahitimu wengi waliochoshwa vichwa na nadharia nyingi pasipokuwa na ujuzi wa kuweza kuwasaidia katika maisha yao baada ya masomo.
Mwandishi maarufu wa kifaransa bwana Victor Hugo alishawahi kusema, afunguaye mlango wa shule ufunga milango ya jera, je hili litawezekanaje katika Tanzania yetu angali wahitimu wengi ni tegemezi na hawana imani ya kesho?.
Ndugu msomaji, Nisieleweke vibaya kwamba naupinga mfumo wetu wa elimu ila mabadiliko ni kawaida ya jamii yoyote ile ya binadamu na ndiyo sayansi ya asiri, hivyo bhasi Mtaala na mfumo wa elimu ulioandaliwa kipindi cha Mwalimu ambapo wasomi walikuwa wachache hamna namna kwamba unaweza timiza mahitaji ya jamii yetu ya leo mwaka 2021.
Ikumbukwe kwamba sisi tunayo mikononi mabadiliko tunayotaka kuyaona kwa sababu tunayo pia serikali makini tulioipa dhamana na yenye kusikia mapendekezo ya umma juu ya mambo yanayohusu maendeleo yetu ya kiuchumi na kijamii.
Kutokana na ilo bhasi namimi kama moja wapo ya jamii ya Watanzania Ili kutatua matatizo ya ajira napendekeze mfumo wa Elimu uwe kama ifuatavyo;
AWALI
Masomo ya awali yachukue mda wa mwaka mmoja ili kumuandaa mtoto katika saikorojia ya shule. Mtoto aanze shule ya awali akiwa na miaka 4.
ELIMU YA MSINGI
Watoto watakaomaliza elimu ya awali wakajiunge na masomo ya msingi ambayo yachukue kipindi cha miaka sita(6).
Ufundishaji wa sasa hivi uimarishwe zaidi na katika ngazi hii ya elimu wanafunzi wafundishwe masomo yote kwa ujumla ikiwemo masomo yote ya sanaa na sayansi ili kumuandaa kijana kuweza kupata uelewa wa msingi wa vitu mbali mbali katika mazingira
ELIMU YA SEKONDARI
Katika ngazi hii ya elimu wanafunzi waainishe categoria au fani watakayosomea na masomo yaendane na fani hiyo hiyo mwanafunzi aliyoichagua.
Elimu ya sekondari katika ngazi hii ichukue kipindi cha miaka mitatu.
Mfano mwanafunzi kama anataka kuwa mwandisi wa majengo masomo yake atakayosoma katika ngazi hii ya elimu yawe ni ya fani ya uhandisi wa majengo.
Baada ya kumaliza ngazi hii ya masomo wahitimu wapewe vyeti mfano; Cheti cha uhandisi wa majengo ngazi ya sekondari.
ELIMU YA SEKONDARI YA JUU
Watakao fuzu katika elimu ya sekondari na wakafaulu kuendelea na masomo wakajiunge na elimu ya sekondari ya juu.
Ngazi hii ya elimu ichukue kipindi cha miaka miwili kama ilivyo sasa ila masomo yatakayofundishwa yawe mwendelezo wa kile mwanafunzi alicho somea akiwa sekondari ya awali.
Mfano, kama alikuwa amesomea cheti cha sheria ngazi ya sekondari basi hapa akasome cheti cha sheria ngazi ya sekondari ya juu.
Mhitimu apewe cheti cha sekondari ya juu katika kada husika.
ELIMU YA JUU
Kwa elimu ya juu mfumo ubaki kama ulivyo sasa.
Wahitimu wa Shahada watakuwa mahiri sana katika kada husika, maana mwanafunzi anaanza kusoma mambo husika katika kada yake kuanzia sekondari na sio kama ilivyo sasa ambapo unakuta mwanafunzi wa sheria anakuja kukutana na sheria mara ya kwanza akiwa chuo.
Hii itachochea uvumbuzi na umahiri wa wahitimu katika fani zao na hivyo vijana wen gi kujiajiri na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wasomi.
Ndugu wana JF, ninahitimisha kwa kusema Serikali ione haja ya kufanya mabadiliko katika mtaala wa elimu kwa namna ya pekee itakayowezesha kuandaa wahitimu kujiajiri, na si kuongeza idadi kubwa ya wahitimu wasio na ajira ambao wengi wao hawana furaha na maisha yao na hatimaye tumaini lao kubakia kukimbilia uhalifu na matendo maovu.
Asanteni.

Upvote
1