Dira ya vijana 2025; mambo haya matatu

Dira ya vijana 2025; mambo haya matatu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

2025 Twende pamoja na mambo haya matatu;
1. Afya
2. PESA
3. FAMILIA

1. AFYA
a) Kula chakula Chenye lishe bora kwa kuzingatia Umri wako.

b) kunywa Maji ya kutosha kulingana na jinsia, umri na uzito wako.

c) Angalau kwa siku lala Masaa nane.

d) Kama hufanyi Kazi za nguvu Fanya mazoezi ya Viungo.

e) Kwa wiki Hakikisha unafunga Mara moja bila Kula. hii ni nzuri kwa afya ya mwili na Roho.

f) Tenga Lisaa limoja kila siju la kutafakari. Lisaa hili uwe mbali na vitu vya mitandao na electronic. Ikiwezekana uwe maeneo ya asili

g) Fanya maombi angalau mara mbili kwa Siku.

h) kwa siku Tenga Nusu saa la kuhakikisha unaangalia au kusoma au kufanya vitu vinavyokuchekesha Sana. Hakikisha uwe unacheka Sana.

I) Punguza Sumu mwilini au vyakula au vinywaji vyenye sumu mwilini. Kama pombe, sigara.

2. PESA
a) Boresha mazingira ya Kazi yako.
b) Anzisha mradi mpya kama ulikuwa nao Mmoja. Uanze polepole na kidogokidogo.

c) kuza jina lako au la biashara yako. Fanya watu wakujue ili soko Lako lizidi Kukua.

d) Iunganishe Kazi au biashara yako iwe Digital. Usifanye analogia.

e) Ongeza kiwango cha Akiba yako

f) Ongeza wadau wenye Tija kwenye biashara yako Ongeza connections.

h) Punguza matumizi yasiyo ya lazima na epuka matumizi hatarishi ya fedha kama Wanawake.

I) Kila pesa utakayoipata Hakikisha inalenga kununua Asset ulizozipanga kwa mwaka 2025.
Mfano kununua Kiwanja au Shamba n.k.

3. FAMILIA.
a) Yote unayofanya unafanya kwa sababu ya Familia yako( Ufalme unaoenda kuanzisha)

b) hivyo, Jambo lolote litakaloathiri Ufalme wako lazima uliepuke. Kama Michepuko ambayo kimsingi haiwezi kumzidi Mkeo kwa lolote lile. Tamaa zako tuu.

c) Ikiwa Mke au Mume anakusumbua na mmeshindwa kufika muafaka ni wakati wa kumuacha mapema ili asiharibu Muda na nguvu zako za kujenga Ufalme wako.

d) Familia yako lazima iwe na Sheria zilizowazi.
Usiongoze Familia kama kichwa cha mwendawazimu. Yaani kile unachofikiri Basi ndio kifanyike.
Unda Sheria za HAKI, upendo, na akili zitakazoongoza familia yako.
Wewe kama mfalme lazima uwe mfano kuzifuata Sheria hizo.
Kuzifuata Sheria au agano mlilowekeana ni dalili ya kujiheshimu.

e) Fanya maridhiano na familia yako ikiwa kuna Jambo lilikuwa haliendi sawasawa na wewe ndiye chanzo cha tatizo Hilo.
Huo unaitwa Uwajibikaji.

f) Huna muda mwingine wa kuifurahisha familia yako(Mkeo na watoto) zaidi ya wakati huu. Usisubiri Kesho au Mwaka usioujua.

g) Jenga Umoja ndani ya familia yako.
Njia kubwa ya Baba kujenga umoja katika familia yake ni kuwa kitu kimoja na Mkewe.
Huwezi wafundisha watoto Umoja ambao hawakuuona kwako na Mkeo.

Ikiwa Mkeo unamhofia ni Bora umpe Talaka ili watoto wasiharibike, wasiwe kama ninyi.

Watoto wote ambao hawana umoja na hawapendani ni matokeo ya Baba na Mama zao kutokuwa wamoja na kutokupendana.

h) Watunzeni Wazazi Wenu.
Kutunza wazazi wako na wamkeo ni kumfundisha mtoto wako wajibu wakuja kuwatunzeni ninyi siku mkiwa Wazee au siku mkiwa na Hali ngumu.

f) Lazima mjenge Imani Moja.
Huwezi Jenga familia zenye miungu wawili au madhabahu MBILI.
Kama unaamini katika mizimu tafuta Mke anayeamini mizimu.
Sio wewe mizimu alafu mke kwa Mwamposa.
Hiyo haiwezi kuwa Familia. Kwa Sisi Watibeli ni Bora kuivunja hiyo ndoa mapema kabla mambo hayajawa Mengi.

Huwezi muongoza Mke ambaye haamini katika miungu au Mungu wako.
Mwanzoni tuu mtaanza vizuri lakini katikati hapo mtapasuana.
Mtasumbua watoto

g) Mtoe Dhabihu na Sadaka za ulinzi wa Familia.
Kila Ufalme unalindwa na nguvu Fulani. Hata serikali zina Siri nzito ambazo huwa nguzo ya ulinzi kwa serikali husika.

Lazima utoe Sadaka au Dhabihu kwa miungu ili ilinde Mipango na malengo ya familia yako.
Mambo hayajiendei tuu.

Sio umeoa Mkeo au Kuolewa ukadhani umemaliza. Utapasua matairi mapema Sana.
Mnaanza vizuri, mnaopendana vizuri,
Mnaelewana vizuri lakini mara paap! Unashangaa ngome imevamiwa Ufalme hauna ulinzi utawala wenu umedondoshwa ndani ya Mwaka tuu kama utawala wa Bashadi Al Assad.

Kama Mungu anamajeshi,
Kama Computer zina Anti Virus,
Kama Serikali inamajeshi ya ulinzi na usalama.

Kwa nini wewe ufikiri upo Salama Sana kuanzisha Ufalme wako duniani na kizazi chako bila kukiwekea ulinzi?

Kitu chochote cha thamani lazima kiwekewe Ulinzi Mkali.

Wakati falme zingine zikidondoka, wewe usiwe wale wanaokuambia Siku hizi ndoa hazidumu.
Sema za wengine ndio hazidumu lakini Ufalme wako utadumu daima. Na kusema huko kuendane na vitendo.

Kama Mwanaume, na mfalme ni jukumu Lako kuilinda Familia yako kiuchumi, kimwili, Kihisia, Kiroho, kiakili na Kwa namna yoyote Ile.

Lazima uwe na backup ya MIUNGU yenye nguvu Sana kukusaidia katika Jambo hilo.
Kama inavyokusaidia katika biashara au mambo mengine basi vivyohivyo ingia mikataba ya ulinzi ya watoto na kizazi chako.
Na ulinzi wa watoto wako utakuwa imara kakiwa na Baba na Mama imara.

Usirudie Makosa.

HAPPY NEW YEAR MABIBI NA MABWANA.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom