insuperable
JF-Expert Member
- Jan 27, 2019
- 299
- 243
Haya ndiyo tunaita kutwanga maji kwenye kinu. Elimu ya Tanzania inatakiwa kufumuliwa na kusukwa upya na siyo kuendelea kuzalisha wasomi uchwara kwa ajili ya kujipatia umaarufu wa kijinga. Tuna matatizo makubwa zaidi ya hivi vi-scolarship ambavyo havifiki hata elfu moja. Ni mjinga tu atakayeshangilia ujinga kama huu.Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefungua dirisha la maombi ya SAMIA SCHOLARSHIP kwa wanafunzi 640 waliopata ufaulu wa juu kwenye masomo ya sayansi katika mitihani ya Kidato cha Sita 2022. Majina ya wanafunzi hao yanapatikana kuanzia leo katika tovuti ya wizara www.moe.go.tz na ya Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu www.heslb.go.tz.
Aidha wanafunzi hao wataanza kuomba ufadhili huo kuanzia kesho Septemba 28, 2022 kupitia tovuti ya Bodi ya Mikopo ya Mikopo https://olas.heslb.go.tz kwa siku 14.
Akitoa tangazo hilo leo Septemba 27, 2022 jijini Dodoma Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema wanafunzi hao watafadhiliwa kwa asilimia mia moja kwa kipindi cha miaka mitatu hadi mitano kulingana na programu husika walizodahiliwa.
Amefafanunua kwamba wanafunzi hao ni wa Tahasusi za sayansi ambazo PCB, PCM, PGM, CBG, CBA, PMC na CBN.
"SAMIA SCHOLARSHIP itagharamia kwa asilimia mia moja masomo ya Chuo Kikuu kwa wanafunzi ambao wamepata udahili katika fani za Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Tiba katika cyuo vikuu vya hapa nchini vinavyotambulika na Serikali ," amesema Prof.
Mkenda Ameendelea kusema kuwa, ufadhili huo utazingatia viwango na miongozo ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa kugharamia ada ya mafunzo, posho ya chakula na malazi, vitabu na viandikwa, mahitaji maalum ya vitivo, mafunzo kwa vitendo, utafiti, vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na bima ya Afya.
Prof. Mkenda ametaja masharti saba ya ufadhili huo ikiwemo kiwango cha ufaulu wa mnufaika kisiwe chini ya GPA 3.8 katika mwaka wa masomo na chini ya hapo ufadhili utasitishwa. Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulgullam Hussein amepongeza hatua ya Serikali kutoa ufadhili huo ambapo kwa upande wa Zanzibar ufadhili wa aina hiyo pia umetolewa kwa wanafunzi 30 hivyo kuongeza fursa kwa watoto wa Kitanzania kupata elimu ya juu.
View attachment 2369695
Source: Chief Government Spokesperson / Msemaji Mkuu wa Serikali on LinkedIn: Dirisha la Maombi ya Samia Scholarship Lafunguliwa Na Mwandishi…
''Kufauru'' ni nini wewe nanga? Tanzania imejaa vilaza kama wewe ambao kazi yao kuimbishwa mapambio ya kijinga huku nchi ikizidi kudidimia.Ndio maana wanachukuliwa waliofauru sana ili wakaendelee kufauru zaidi.
Sasa ukilaza wangu uko wapi boss. Kutukana tu bila kuwafundisha wanaokosea haitoshi. Kaa chini andika hoja nzito za kuwafundisha unaohisi ni vilaza sambaza mitandaoni ili waelimike na ukilaza uwaondoke.''Kufauru'' ni nini wewe nanga? Tanzania imejaa vilaza kama wewe ambao kazi yao kuimbishwa mapambio ya kijinga huku nchi ikizidi kudidimia.
Mimi kwa uelewa wangu hili la scholarship ni zuri sana. Linakwenda kuwaamusha watanzania katika masomo ya sayansi.Haya ndiyo tunaita kutwanga maji kwenye kinu. Elimu ya Tanzania inatakiwa kufumuliwa na kusukwa upya na siyo kuendelea kuzalisha wasomi uchwara kwa ajili ya kujipatia umaarufu wa kijinga. Tuna matatizo makubwa zaidi ya hivi vi-scolarship ambavyo havifiki hata elfu moja. Ni mjinga tu atakayeshangilia ujinga kama huu.
Hayo uliyoyaona ni majina ya walio qualify kuipata hiyo scholarship. Mchakato unaofuata ni kuapply kwenye mfumo.Ninacho jua ni kuwa selection kwa ajili ya 2022/2023 Mama Samia Scholarship program tayari imeisha fanyika, majina tayari yapo, na kinacho ngojrwa ni kukamilisha paper works ndogo ndogo tuu, sasa mleta uzi sijakuelewa unaposema dirisha litafuliwa sijui tarehe 28
Na kwa uelewa wako wa ''ufauru'' basi una haki kabisa.Mimi kwa uelewa wangu hili la scholarship ni zuri sana. Linakwenda kuwaamusha watanzania katika masomo ya sayansi.
Kama ulikaa darasani mpaka ukahitimu iwe darasa la saba, sekondari au chuo, na hujui kuandika maneno rahisi kabisa ya kiswahili, mimi nitasaidia nini? Rudi usome tena utaona kosa lako.Sasa ukilaza wangu uko wapi boss. Kutukana tu bila kuwafundisha wanaokosea haitoshi. Kaa chini andika hoja nzito za kuwafundisha unaohisi ni vilaza sambaza mitandaoni ili waelimike na ukilaza uwaondoke.
Pamoja na yote hayo, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Tuseme tu ukweli Mama anaupiga mwingi sana.Kama ulikaa darasani mpaka ukahitimu iwe darasa la saba, sekondari au chuo, na hujui kuandika maneno rahisi kabisa ya kiswahili, mimi nitasaidia nini? Rudi usome tena utaona kosa lako.
Ujinga wa kwanza huuBora tu uombe zako mkopo wa HESLB usome kwa kurelax,ukipiga first class ni poa tu.
Unaweza omba hio hela ya Samia,bahati mbaya ukapiga 3.5,jamaa wakaanza kukuambia eti,huruhusiwi kuomba tena
Mjinga wa pili huyuHata atoe nini 2025 lazima ajambe cheche! Hakuwekwa pale magogoni kuwa li picha tu la kuongozwa kwa remote! Hoves kabisa!!
Mjinga wa 3 huyuNi gpa ndog ikiwa utajipangiaa ila kwa masomo ya sayanc ni shid san mpk msul ukaze
Good initiative.Cha muhimu sustainability iwepo....Kisha pia ifanyike nje ya mchakato ikianzi.mwanafunzi akiwa shuleni.Nilipitia mchakato wa scholarship za harvar na mit.Hata usipofaulu ila zinakupa challenge ya maana.NECTA bado ni mtihani wa kiwango cha chini kupima.upeo wa mtuSerikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefungua dirisha la maombi ya SAMIA SCHOLARSHIP kwa wanafunzi 640 waliopata ufaulu wa juu kwenye masomo ya sayansi katika mitihani ya Kidato cha Sita 2022. Majina ya wanafunzi hao yanapatikana kuanzia leo katika tovuti ya wizara www.moe.go.tz na ya Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu www.heslb.go.tz.