Dirisha la Usajili lafungwa, Yanga yashindwa kupeleka mwakilishi kwenye kozi maalum

Dirisha la Usajili lafungwa, Yanga yashindwa kupeleka mwakilishi kwenye kozi maalum

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2013
Posts
338
Reaction score
180
jamal malinzi.png

Dirisha la usajili kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza la StarTimes na Ligi Daraja la Pili msimu wa 2016/2017 lilifungwa saa 6.00 usiku wa Jumamosi Agosti 6, 2016.

Hadi dirisha linafungwa, timu kadhaa hazikuwasilisha kabisa usajili wake licha ya kukumbushwa kwa njia mbalimbali na uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Usajili wa msimu huu ni kama msimu uliopita kwamba unafanyika kwa njia au mfumo wa mtandao unaoitwa Transfer Matching System (TMS) ambao (server) yake au chombo chake cha kutunza kumbukumbu kipo Makao Makuu ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) - Uswisi.

Kwa kawaida mfumo huu upo chini ya FIFA na TFF hutoa taarifa kwa FIFA tarehe ya kufungua dirisha la usajili na kufunga.

Mfumo huu uhusisha pande tatu ambazo ni klabu, shirikisho (TFF) na FIFA. Kimsingi kazi ya usajili hufanywa na klabu ambako inajaza fomu kwa njia ya mtandao na hupakia viambatanisho kama vile mikataba ya wachezaji na picha za wachezaji.

Zoezi hili hufanywa na Meneja Usajili wa klabu husika wakati shirikisho hufanya kazi ya kuhakiki na kuidhinisha tu na FIFA huratibu na kuusimamia mfumo mzima.

Kabla ya kutangaza kufunguliwa kwa dirisha la usajili hapo Juni 15, 2016 Shirikisho liliandaa kozi ya mafunzo ya usajili kwa klabu zote 64 zikiwa ni 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara; 24 zitakazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza la StarTimes na timu 24 zitakazoshiriki Ligi Daraja la Pili msimu wa 2016/2017.

Baadhi ya timu hazikutuma wawakilishi, lakini ziko zilizofanya jitihada za kuomba usaidizi kwa kufika ofisini TFF kuomba usaidizi wa kufanya usajili na zilifanikiwa. Kwa Young Africans, licha ya kuwa hapa Dar es Salaam, haikuomba usaidizi wowote na hata walipokumbushwa kuhusu suala la usajili, hawakujibu kitu.

Young Africans ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara mbili mfululizo msimu wa 2014/2015 na 2015/2016, ni moja ya vilabu ambavyo havikutuma mwakilishi kwenye kozi iliyofanyika Uwanja wa Taifa kwa siku tatu mfululizo ikigusa wawakilishi wa madaraja ya Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili.

Meneja wa TMS wa Young Africans ni Katibu Mkuu hakuwahi kupata mafunzo ya TMS.

Hivyo sasa klabu zote ambazo hakuzituma usajili wake, hazina budi kuandaa utetezi utakaokwenda TFF ambao utatumwa FIFA yenye mamlaka ya kufungua dirisha, na utetezi huo ukikataliwa timu husika inabidi ishuke daraja ambalo halimo kwenye usajili wa mfumo wa TMS.

TFF kwa sasa inasuburi barua ya utetezi wa klabu ambazo hazikukamilisha zoezi la usajili ili iutume FIFA. Sambamba na hilo TFF inatathimini mwenendo mzima kisha itatoa taarifa kwa FIFA ili kuangalia namna gani ya kushughulikia maeneo yaliyokuwa na upungufu kwa sasa na baadaye.
 
Huo ni uongo taarifa zipo tff siku nyingi .Yanga walimaliza usajili mwezi mmoja uliopita TFF wana majungu
 
Mkuu Jamal Malinzi jitahidini hawa jamaa waisishushwe daraja, maana ubingwa wetu wa 2016/2017 hautakua na maana bila kumgonga ndala nje ndani
 
kwan Nani anapaswa Ku upload hizo taarifa kwenye mtandao? je tff wameandiakia hizo timu barua rasm au ndio kupitia media
 
kwan Nani anapaswa Ku upload hizo taarifa kwenye mtandao? je tff wameandiakia hizo timu barua rasm au ndio kupitia media
TFF wamefanya haya,
1. Kuandika Barua kuzialika timu zishiriki kozi maalumu inayohusu kuupload hayo majina.. Ndala wakachomoa
2. TFF wameendesha hiyo kozi.. Ndala hawakutokea
3. TFF wametuma barua kuhusu deadline ya kutuma majina, Ndala wakaendelea kugoma.
Sasa hapa utaanzaje kuilaumu TFF??
 
Si ndiyo hiyo hiyo TFF mnasema inaibeba Yanga? Leo iweje waseme Yanga haijafanya usajili?

Siku zote Yanga imeweka wazi visa vya TFF dhidi yake. Sasa yule mnunuzi wa mikia kaja na yake. Hakuna njia ya kuizuia Yanga kutwaa ubingwa zaidi ya figisufigisu kama hizi.

Tuone mwisho wa sinema hii itakuwa vipi. Uwanjani lazima Yanga atwae ubingwa tena. Labda kwa njia kama hizi Azam au mikia wataona ndani.
 
Yanga wanafanya mambo kienyeji sana pale yanga inabidi wamapate Baraka Kizuguto ambaye kwa sasa ni meneja WA mashindano na TMS pale TFF ashike mite go cha meneja WA timu pale hayo mambo ya TMS na usimamizi WA timu yawe kwako maana yule Dogo yupo vizuri ana coz 3 za FIFA mambo ya TMS na umeneja afu yule ni yanga damu
 
Si ndiyo hiyo hiyo TFF mnasema inaibeba Yanga? Leo iweje waseme Yanga haijafanya usajili?

Siku zote Yanga imeweka wazi visa vya TFF dhidi yake. Sasa yule mnunuzi wa mikia kaja na yake. Hakuna njia ya kuizuia Yanga kutwaa ubingwa zaidi ya figisufigisu kama hizi.

Tuone mwisho wa sinema hii itakuwa vipi. Uwanjani lazima Yanga atwae ubingwa tena. Labda kwa njia kama hizi Azam au mikia wataona ndani.

Kuna ubabe wa kijinga unaondelea kati ya Yanga na TFF unazidi kuharibu soka la Tanzania.Malinzi anazidi kuharibu soka letu
 
Kuna ubabe wa kijinga unaondelea kati ya Yanga na TFF unazidi kuharibu soka la Tanzania.Malinzi anazidi kuharibu soka letu
Tuweke ushabiki pembeni.... Hili suala lina haribu vipi mpira wa Tanzania nzima.
 
HILI SUALA LA USAJILI SI TATIZO KABISA....

MSIUMIZE VICHWA VYENU KUDHANI KUWA HATA KAMA YANGA WAMEKOSA BASI WATAPATA ADHABU YA KUSHUSHWA DARAJA...

TFF ndio YANGA, a YANGA ndio TFF.
 
TFF wamefanya haya,
1. Kuandika Barua kuzialika timu zishiriki kozi maalumu inayohusu kuupload hayo majina.. Ndala wakachomoa
2. TFF wameendesha hiyo kozi.. Ndala hawakutokea
3. TFF wametuma barua kuhusu deadline ya kutuma majina, Ndala wakaendelea kugoma.
Sasa hapa utaanzaje kuilaumu TFF??
Mhindi ana njama za kuihujumu Yanga iliainunue kwa bei ya kutupa!
 
Tuweke ushabiki pembeni.... Hili suala lina haribu vipi mpira wa Tanzania nzima.

Kazi ya TFF ni kuvisimamia na kuvisaidia vilabu vya soka na vilabu vinapaswa viiheshimu TFF,kwa sasa Yanga hawasikilizi chochote toke TFF .Haya yanayotokea ni matokeo na yasipofanyiwa kazi mengi yatatokea
 
Back
Top Bottom