Dirisha lenye kutumia vioo na gundi yake

Dirisha lenye kutumia vioo na gundi yake

Hajto

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2013
Posts
5,646
Reaction score
5,606
Habari zenu waungwana, napenda kujua na kufahamu, kuna madirisha yale wanayotumia sana maeneo ya vijijini yenye kuwa na baridi sana, napenda kujua gharama ya vioo vyake hua ni vidogo, mfano kioo cha cm 36 kwa 45 ndio vipo vingi na vingine vikubwa vyake vipo cm 98-33 napenda kujua gharama yake na mahali ambapo naweza kuvipata kwa bei rahisi.

Pili napenda kujua ni vitu gani vinayoweza kushikilia kioo kwenye dirisha je ni gundi aina gani ni nzuri kuna mmoja aliniambia nitumie Silicon na puti, je ni sahihi ama kuna gundi nyingine ambazo ni bora zaidi ya hizo.

Tatu napenda kujua hendo na steyi zake za kufunga na kufungua dirisha ni kiasi gani kwa hapa Dar. Mwisho napenda kujua gharama za rangi ile nyeusi ya kupaka mwishoni baada ya kupaka ile rangi nyekundu, ukubwa wa dirisha ni futi 5 kwa 5 madirisha yapo 8. Akijitokeza mtu na kunipatia size ni rangi ya kiasi gani yenye kutosha kwa madirisha hayo itapendeza sana.

Mfano wa dirisha ni ilo hapo nimeliweka chini.

dirisha.jpg
 
Nimetumia nyumba kwangu, tumia clean silcon na put nyeusi kama put no ngumu inachanganywa na mafuta ya taa, ila rangi tumia rangi nyeusi ya Tina ile ya kuspray kabla ya kubandika vioo, funga handle na stay zipo imara na fake, utazitambua Kwa bei ila fundi wangu alitengeneza hizo stay na handle Kwa kutumia flat bar.
IMG_20210828_180926.jpg
 
Nimetumia nyumba kwangu, tumia clean silcon na put nyeusi kama put no ngumu inachanganywa na mafuta ya taa, ila rangi tumia rangi nyeusi ya Tina ile ya kuspray kabla ya kubandika vioo, funga handle na stay zipo imara na fake,utazitambua Kwa bei ila fundi wangu alitengeneza hizo stay na handle Kwa kutumia flat barView attachment 2044965
Badala ya kwenda mbele wewe unataka turudi nyuma
 
Yanaitwa madirisha ya Z-bar, nikimjengea mama nyumba kule kijijini, nikamwambia fundi atengeneze ya hivyo yeye akatengeneza ya Aluminium hakika alinikera, ila tofauti huwa ndogo sana aluminium.
 
Old is gold, walioweka aluminium wanajuta wanavyoibiwa kila siku, wala wezi hawavunji kioo wanalinyofoa wanaliweka chini wanakata flat bar wanahamisha Hadi kabati
Chaguo ni lako
Siku hizi unaweka grill ya nondo au square pipe. Flat bars haiwezi kuzuia Mwizi ule ni urembo tu.
 
Old is gold, walioweka aluminium wanajuta wanavyoibiwa kila siku, wala wezi hawavunji kioo wanalinyofoa wanaliweka chini wanakata flat bar wanahamisha Hadi kabati
Chaguo ni lako
Haya wanayawekaga vijijini haswahaswa
 
Old is gold, walioweka aluminium wanajuta wanavyoibiwa kila siku, wala wezi hawavunji kioo wanalinyofoa wanaliweka chini wanakata flat bar wanahamisha Hadi kabati
Chaguo ni lako
Kwakweli mimi pia haya ya chuma yatanihusu, hamna namna
 
Back
Top Bottom